WANAMICHEZO ZANZIBAR WAMZIKA IBRAHIM JEBA
Mamia ya Wananchi, Mashabiki na Wapenda soka wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Azam Fc, Mtibwa Sugar na Chuoni Ibrahim Rajab Juma (Jeba) ambae amefariki jana na kuzikwa leo Kijijini Kwao Ndijani Mseweni Mkoa wa Kusini Unguja. Maziko hayo yalianzia nyumbani kwao Magomeni Mzalendo na Kusaliwa Msikiti wa Maandalizi Magomeni Mpendae ambapo ndugu jamaa na marafiki wa marehemu walijitokeza kwa wingi kwenye safari yake hiyo mwisho. Mchezaji huyo ambae pia aliwahi kucheza timu ya Taifa ya Marehemu Ibrahim Jeba ameacha Mke mmoja. Mungu amlaze mahala pema peponi amin.