Posts
Showing posts from August, 2019
SHAIBU NINJA AFIKA SALAMA MAREKANI, AFURAHIA MAPOKEZI YAKE
- Get link
- X
- Other Apps
UFAFANUZI JUU YA MCHEZAJI SHAIBU NINJA KUSAJILIWA MAREKANI LA GALAXY
- Get link
- X
- Other Apps
Wadau wengi wa Soka hapa Zanzibar na Tanzania Bara wanahamu sana kujua juu ya hatma ya Beki wa zamani wa Yanga Abdalla Haji Shaibu (Ninja) kuhusu kwenda kucheza Soka nchini Marekani. Ni kweli Ninja sasa yupo Marekani kwenye timu ya La Galaxy ambapo amekwenda kwa mkopo, na baada ya kufanyiwa vipimo vya afya na mambo mengine La Galaxy wamelazimika kumuweka timu ya La Galaxy II (Timu B) na baada ya kuonekana anahitaji kuzowea mazingira na kupata uzoefu kidogo kwenye timu hiyo B kisha watampandisha kucheza timu kubwa ambayo inashiriki ligi kuu Soka Marekani, timu ambayo anacheza Zlatan Ibramovic. Ninja tayari ameshaanza mazoezi kwenye timu hiyo B na uzuri kwamba timu hiyo B wakati mwengine wanachanganyika kufanya mazoezi na timu kubwa kwasababu muda wowote mchezaji wa timu B akionyesha kiwango hupandishwa timu kubwa. Ninja amepewa jezi no 51, hivyo naomba Watanzania wafahamu kuwa kijana wao alikusudiwa kwenda kwa mkopo kwenye timu kubwa lakini kutokana na kutofanya mazo...
WANA JESHI WA ANGOLA KUTUA SAA 7 USIKU KUWAVAA KMKM CAF CL
- Get link
- X
- Other Apps
Wapinzani wa timu ya KMKM kwenye Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika Clube Desportivo 1 De Agosto wanatarajiwa kutua Zanzibar saa 7 za usiku (leo kuamkia kesho Jumatano) wakitokea kwao Angola kwaajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza utakaochezwa Agost 10, 2019 saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan. Timu hiyo ambayo ni ya Jeshi la Angola itawasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume na kupokelewa na wenyeji wao ambao ni KMKM. Wawakilishi wengine wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya Malindi wanatarajia pia kuwapokea Wapinzani wao timu ya Mogadishu City Club (MCC) kutoka Somalia kwaajili ya mchezo wao utakaochezwa Jumapili Agost 11, 2019 kwenye uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni ambapo MCC licha yakucheza ugenini (Amaan) itakuwa ndio mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza baada ya kuliomba Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kucheza michezo yote miwili wa nyumbani na ugenini ichezwe Zanzibar....
WASOMALI WANAOCHEZA NA MALINDI CAF WAMEOMBA MECHI ZAO ZOTE KUCHEZWA ZANZIBAR
- Get link
- X
- Other Apps
Wapinzani wa timu ya Malindi ya Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya Mogadishu City Club (MCC) kutoka Somalia wameliomba Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) michezo yao yote miwili wa nyumbani na ugenini ichezwe Zanzibar. Mchezo huo utachezwa Jumapili Agost 11, 2019 kwenye uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni ambapo MCC licha yakucheza ugenini (Amaan) itakuwa ndio mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza. Katika kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Malindi MCC leo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya FC Heegan kwenye uwanja wa Benadir majira ya saa 10:00 za jioni. Timu hiyo itasafiri kutoka Somalia kwenda Zanzibar Agost 7, 2019 ambapo MCC inawakilisha Somalia kwenye Mashindano hayo baada kuifunga kwa penalty HorseedSC 4-3 kwenye kombe la Daa (FA CUP) kufuatia kwenda sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 ambapo na Malindi wamepata nafasi hiyo baada ya kuichapa JKU kwa Penalty 4-3 kufuatia dakika 120 kutoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa fai...
BALOZI SEIF USO KWA USO NA RAIS WA ZFF, WAPEWA USHAURI WA KUKUZA SOKA ZANZIBAR
- Get link
- X
- Other Apps
Seif Kombo Pandu kushoto na Kulia ya Balozi Seif Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameushauri Uongozi Mpya wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} kusimamia vyema Sheria pamoja na Kanuni ilizojiwekea za kuendesha Mpira wa Miguu ili kuepuka migogoro inayoweza kuviza viwango vya Soka Nchini. Amesema wapo baadhi ya Viongozi waliowahi kushika madaraka ndani ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar lakini walishindwa kuzitekeleza sheria hizo na hatimae walifikia hatua ya kupelekana Mahakamani jambo ambalo linakwenda kinyume na uendeshaji wa Vyama vinavyosimamia na kuendesha soka Kitaifa na Kimataifa. Akizungumza na Uongozi Mpya wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} hapo Afisini kwake Vuga, Balozi Seif Ali Iddi amesema vurugu zilizokuwa zikishuhudiwa kutokea ndani ya Uongozi wa iliyokuwa ZFA kipindi cha nyuma zilichangia kudorora kwa kiwango cha Soka hapa Nchini. Balozi Seif amesema Uongozi huo wa sasa unapaswa kuelewa kwamba wao ndio watakaobeba lawama z...