Posts

Showing posts from September, 2019

WANAMICHEZO ZANZIBAR WAMZIKA IBRAHIM JEBA

Image
Mamia ya Wananchi, Mashabiki na Wapenda soka wamejitokeza katika mazishi ya aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Azam Fc, Mtibwa Sugar na Chuoni Ibrahim Rajab Juma (Jeba) ambae amefariki jana na kuzikwa leo Kijijini Kwao Ndijani Mseweni Mkoa wa Kusini Unguja. Maziko hayo yalianzia nyumbani kwao Magomeni Mzalendo na Kusaliwa Msikiti wa Maandalizi Magomeni Mpendae ambapo ndugu jamaa na marafiki wa marehemu walijitokeza kwa wingi kwenye safari yake hiyo mwisho. Mchezaji huyo ambae pia aliwahi kucheza timu ya Taifa ya  Marehemu Ibrahim Jeba ameacha Mke mmoja. Mungu amlaze mahala pema peponi amin.

IBRAHIM JEBA AMEFARIKI DUNIA

Image
Ibrahim Rajab (Jeba) mchezaji wa zamani Mtibwa Sugar na Azam fc amefariki Dunia jioni ya leo Hospitali ya Mnazi Mmoja. Ibrahim Jeba Mendieta msimu huu alikuwa ameshaanza mazoezi na timu yake ya Chuoni kwaajili ya kutumika tena kwenye ligi kuu Soka ya Zanzibar. Maziko yatakuwa kesho saa 7 mchana nyumbani kwao Magomeni Mzalendo na kuzikwa Kijijini kwao Ndijani. Mungu amsamehe makosa yake na amuingize pepon amin.

LIGI KUU ZANZIBAR YAANDELEA KWA KISHINDO

Ligi Kuu Soka ya Zanzibar imeendelea tena leo kwa kuchezwa michezo miwili kwenye viwanja viwili tofauti majira ya saa 10 za jioni. Katika uwanja wa Mao Mlandege wameanza vyema ligi hiyo baada ya kuwafunga Chipukizi mabao 3-1 ambapo mabao ya Mlandege yamefungwa na Yahya Haji (Karoa) akifunga mabao 2 na jengine likifungwa na Khamis Abdallah (Terry) huku bao pekee la Chipukizi likifungwa na Abdallah Mohd. Na katika uwanja wa Amaan timu ya Maostadh wa Chuoni ikatoka na ushindi wa mabao 3-2 baada ya kuwafunga timu ya Machomane. Ligi hiyo itaendelea tena Jumatano kwa kuchezwa mchezo mmoja kati ya Polisi dhidi ya Malindi majira ya saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.

MALINDI YAANZA VIBAYA NYUMBANI

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Malindi wameanza vibaya nyumbani baada ya kukubali kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Almasry ya Misri mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan. Mabao ya Almasry yamefungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27, 39, Hassan Ibrahim dakika ya 32 na Saidou Simpore dakika ya 52 huku bao pekee la Malindi likifungwa na Ibrahim Ali (Imu Mkoko) dakika ya 42. Mchezo wa marudiano utachezwa Septemba 29, 2019 huko Misri ambapo Malindi anatakiwa kushinda 4-0 ugenini ndipo asonge mbele.

ZANZIBAR IMEPANGWA TENA KUNDI MOJA NA TANZANIA BARA CECAFA

Image
Timu ya Taifa ya Vijana ya Zanzibar U-20 imepangwa kundi moja na ndugu zao Tanzania bara kwenye Mashindano ya Vijana ya Cecafa U-20 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 21, 2019 huko Uganda. Timu hizo zimepangwa kundi B pamoja na Kenya na Ethiopia ambapo kundi A wamo wenyeji Uganda, Eritrea, Djibouti na Sudan huku Burundi ikipangwa kundi C pamoja na Sudan ya Kusini na Somalia. Baada ya Zanzibar na Tanzania Bara kupangwa kundi moja Watanzania wengi watayakumbuka Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup mwaka 2017 huko Machakos nchini Kenya ambapo pia walipangwa kundi moja na Zanzibar ikawachapa Tanzania bara mabao 2-1.