Posts

Showing posts from April, 2018

TIMU ZA VIKOSI ZAENDELEA KUTESA KWENYELIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Image

ZFA YAITUPIA LAWAMA CECAFA, SASA YAAMUA KUKATA RUFAA

Image
Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimepania kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ya kuiondoa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys). Akizungumza na Waandishi wa Habari Makamu wa Rais wa ZFA Unguja Ali Muhammed Ali amesema kuondoshwa Karume Boys katika Mashindano ya Cecafa ya Vijana yanayoendelea nchini Burundi imesababishwa na Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye kwa kuwa hakuwasiliana na ZFA kuhusu uchanganuzi wa kanuni inayohusiana na umri wa kucheza kwenye Mashindano hayo. Amesema wao wapo tayari kufanyiwa uchunguzi wowote juu ya kadhia hiyo huku akizidi kumtupia lawama Musonye kwa kusema anahusika moja kwa moja Zanzibar kuondoshwa kwenye Mashindano hayo. Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 huku Zanzibar ikuwape...

ZFA ITAMWAGA MBOGA KESHO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZANZIBAR KUONDOLEWA KATIKA MASHINDANO YA CECAFA BURUNDI

Image
Baada ya jana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo kutoa taarifa juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi, hatimae Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimevunja ukimya na kesho kinatarajia kuongea na Waandishi wa Habari juu ya kadhia nzima iliyowakumba vijana wa Zanzibar nchini Burundi. Mkutano huo utafanyika saa 4:00 za asubuhi katika ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan ambapo viongozi wakuu wa chama hicho watakuwepo katika mkutano huo. Jana Katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Omar Hassan (King) alisema ikithibitika kuwa ZFA wao ndio wenye makosa mpaka Karume Boys wakaondoshwa katika Mashindano basi wajiwajibishe. Zanzibar imeondoshwa katika mashindano hayo na kupewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa katika mashindano, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa k...

SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA ZFA IKITHIBITIKA KUWA WAO NI SABABU YA KUONDOSHWA KARUME BOYS CECAFA BURUNDI

Image
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo leo imetoa taarifa na ufafanuzi juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi. Katibu mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan (King) ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kadhia hiyo iliyotea kwa Vijana wa Zanzibar huko nchini Burundi ambapo amesema ikithibitika kuwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wao ndio wenye makosa mpaka Karume Boys wakaondoshwa katika Mashindano basi wajiwajibishe wenyewe kwa kujiuzulu. "Kama itakuwa kosa lao ZFA na kama Mimi nimo ZFA basi ntakaa pembeni, naamini na wao wenyewe watatumia busara ya hali ya juu kukaa pembeni". Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 ...

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU TIMU YA KARUME BOYS ITATOLEWA KESHO

Image
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo kesho inatarajia kutoa taarifa na ufafanuzi juu ya timu yake ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) ambayo imeondolewa kwenye Mashindano ya CECAFA U-17 yanayoendelea nchini Burundi. Karume boys imeondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini ya Dola 15000 pamoja na kufungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002.  Katibu mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan (King) atatoa taarifa na ufafanuzi punde kesho majira ya Mchana katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Mjini Unguja ambapo Wizara hiyo itapokea Barua kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) . Karume boys ilikuwa icheze jana mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sudan katika uwanja wa Gitega mchezo ambao haukuchezwa baada ya Sudan kupeleka malalamiko yao kwa CECAFA na mchezo huo ukafutwa. Wakati huo huo katika kun...

MSIMAMO WA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA PEMBA

Image

MSIMAMO WA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Image

VETERANI ZANZIBAR WAPATA MBELEKO YA RC MJINI

MASHINDANO YA KIMATAIFA YA RESI ZA BASKELI KUFANYIKA KESHO ZANZIBAR

Image
Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale imeandaa Mashindano ya resi za Baskeli kwa lengo la kuutanganza Utalii Visiwani Zanzibar. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ikuhusiana na matayarisho hayo   katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Dk   Vuai Iddi   amesema mashindano hayo yatajumuisha waendesha baskeli vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika, hivyo amewata wananchi kujitokeza kushangilia pamoja na kujionea uhondo wa mashindano hayo. Amesea mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la taifa na   wananchi mmoja mmoja pamoja na ongeza la ajira kwa vijana. Rais wa vijana wa Afrika Mashariki   Fest Peter George Mzunda amesema lengo la mashindano hayo ni kutangaza utalii pamoja na kuwapa fursa vijana kushiriki michezo ya baskeli na kuamsha hamasa kwa vijana kupata ajira kupitia mchezo huo. Katibu mkuu wa Chama cha baskeli Zanzibar amesema kwa upande wa chama chao wameshukuru kupata nafasi ya kush...

KASSIM KHAMIS WA PRISONS NA ZANZIBAR HEROES KUENDELEA KUUKOSA MSIMU MZIMA BAADA YA KUUMIA KATIKA MCHEZO WA CECAFA WA HEROES NA TZ BARA

Image
Klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara itaendelea kukosa huduma ya kiungo mshambuliaji wake Kassim Suleiman Khamis ambae anaendelea na matibabu ya goti. Khamis aliiumia goti Disemba 7, 2017 akiitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwenye Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup ambapo Heroes waliwafunga ndugu zao Tanzania Bara kwa mabao 2-1, mabao ambayo amefunga yeye mwenyewe Khamis pamoja na Ibrahim Hamad Hilika, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kenyatta Machakos nchini Kenya. Katika mchezo huo uliokuwa mkali Khamis aliumia baada ya kugongana na Daniel Lyanga wa Kilimanjaro Stars na kupelekea kukosa Mashindano yote ya Cecafa msimu uliopita pamoja na kutoitumikia klabu yake ya Prisons ya Mbeya. Akizungumza na Mtandao huu Khamis amesema anaendelea na matibabu na atokosa mechi zote zilizobakia kwa msimu huu huku akitarajia kujifua kwaajili ya kujiandaa na msimu ujao wa mwaka 2018-2019. "Bado goti linanisumb...

KARUME BOYS WAKABIDHIWA BENDERA, TAYARI WAMESHAPANDA PIPA KWENDA BURUNDI KATIKA MASHINDANO YA CECAFA

Image
Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham amekabidhi bendera kwa timu ya taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya miaka 17 (Karume Boys) kwa ajili ya kushiriki michuano ya Cecafa ya Vijana nchini Burundi. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale kikwajuni ambapo viongozi mbali mbali walihudhuria wakiwemo wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo, baraza la Taifa la michezo na chama cha soka ZFA. Akitoa nasaha zake kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo Naibu Lulu amewataka wachezaji hao kujielewa wao ni nani na jukumu kubwa walilopewa na nchi yao huko wanakokwenda huku akiwasisitiza kudumisha nidhamu kwani ndio silaha yao. Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewapa jukumu kubwa la kuiwakilisha nchi, hivyo lazima wafahamu majukumu yao na wanatakiwa kufanya ili kuhakikisha wanailetea sifa nzuri nchi yao pamoja na kuwa na nidhamu kubwa. Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo O...

KOCHA WA KARUME BOYS ATAMBA KUBEBA UBINGWA WA CECAFA KUTOKANA NA KIKOSI CHAKE KILICHOSHEHENI VIPAJI

Image
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka chini ya miaka 17 (Karume Boys) Mzee Ali Abdallah amewatoa hofu Wazanzibar juu ya kikosi chao kinachotarajiwa kwenda Burundi katika Mashindano ya CECAFA ya vijana yanayotarajiwa kuanza rasmi April 14 mwaka huu. Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi mchana wa leo katika uwanja wa Amaan Kocha Mzee amesema wameamua kufanya mazoezi mchana ili kuzowea mazingira ya Burundi katika Mashindano hayo kwani katika ratiba wamepangiwa kucheza michezo mengine mchana huku akiwatoa hofu wa Wazanzibar na kusema kuwa anaamini kikosi chake kitatwaa Ubingwa wa Mashindano hayo. “Tunashukuru Mungu mazoezi yanaendelea vizuri mana Vijana wanapokea vizuri mazoezi, tumeamua kufanya mazoezi mchana kwasababu kule Burundi ratiba ya michezo yetu siku nyengine tunacheza mchana ili tuzowee mazingira, mimi naamini vijana hawa kwa vile wanaari kubwa watabeba ubingwa na Wazanzibar wasiwe na wasi wasi wowote”. Aidha kocha Mzee amesema hana wasi wasi kwa ti...

LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA SI MCHEZO, ANGALIA TIMU 6 ZILIZOPO KATIKA MSTARI MWEKUNDU WA KUSHUKA DARAJA

Image

ZANZIBAR YAPANGWA KUNDI LA KIFO PAMOJA NA NDUGU ZAO TANZANIA BARA CECAFA YA VIJANA NCHINI BURUNDI

Image
Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) imepangwa katika kundi la kifo kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018. Habari zilizopatikana na Mtandao huu kutoka kwa CECAFA zinaeleza kuwa Zanzibar imepangwa kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na baraza hilo inaonesha kuwa Zanzibar itaanza kampeni za kutwaa taji hilo, kwa kucheza na Sudan April 15 katika uwanja wa Gitega majira ya saa 7:30 za mchana. Tayari Zanzibar imechagua wachezaji 20 na ipo katika maandalizi makali chini ya kocha mkuu Mzee Ali Abdallah, ambapo Vijana hao wapo kambi katika Hoteli ya Zanzibar Paradise International iliyopo Uwanja wa Amaan. Katika Mashindano hayo yamepangwa makundi mawili yani A ambalo lenye timu za Kenya, Ethiopia, Somalia na wenyeji Burundi. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza April 14 katika viwanja vitatu tofauti nchin...