TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR YA MPIRA WA MEZA YASHINDANA NA KAKA ZAO WA BARA KUTAFUTA TIMU YA TANZANIA ITAKAYOKWENDA AUSTRALIA
Mashindano maalum ya mchujo wa kutafuta timu ya Taifa ya Mpira wa Meza Tanzania yameanza leo na kumalizika kesho Jumapili kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Kisutu Jijini Dar es salam. Katika mchujo huo timu ya Taifa ya Zanzibar inachuana na wenzao wa Tanzania bara kwaajili ya kupata wachezaji wawili watakaowakilisha Tanzania katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yatafanyika Gold Coast Australia kuanzia April 4-15, 2018. Jumla ya Wachezaji 10 wanagombania nafasi hizo 2 za kwenda Australia ambapo Wachezaji kutoka Zanzibar wapo wawili ambao ni Mohammed Shaabani na Khalid Ahmed. Wachezaji hao 10 watacheza kwa mizunguko 9 ambapo kila mmoja atacheza na mwenzake na wawili wa mwanzo ndio watakaofanikiwa kwenda huko Australia. Zaidi endelea kufatilia Blog hii kupata taarifa kwa kina kwenye kinyanganyiro hicho.