BOYS HOI KWA KILIMANI CITY, SAILORS YAIMALIZA CHARAWE
Timu ya Jang’ombe Boys imeendelea kufanya vibaya katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Kilimani city mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan. Bao pekee la City limefungwa na Baraka Mashango dakika ya 19. Mapema saa 8 za mchana Kiwanjani hapo Black Sailors wakaendelea na ari yao ya ushindi baada ya kuifunga Charawe mabao 2-1. Mabao ya Sailors yamefungwa na Mustafa Hamad “Mboma” dakika ya 43 na Maulid Dhamiri wa Charawe alijifunga mwenyewe dakika ya 59 huku bao pekee la Charawe limefungwa na Boniface Afred dakika ya 45. Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja itaendelea tena Alhamis ya Novemba 2, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za mchana Mafunzo watakuwa na kazi kwa Kipanga na saa 10:00 za jioni JKU watakipiga na KVZ. Jang'ombe Boys