DIAMOND AANZA KUSAKA WATANGAZAJI WA WASAFI RADIO NA TV, WAZIRI WA MICHEZO ZANZIBAR AWAOMBA WAZANZIBAR WAJITOKEZE KWA WINGI NGOME KONGWE KESHO
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amewataka watangazaji pamoja na watu wenye vipaji hivyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi maalum la kutafuta vipaji hivyo zoezi ambalo litafanyika kesho Jumanne kuanzia saa 3 asubuhi hadi jioni katika ukumbi wa Ngome Kongwe. Waziri Rashid ameyasema hayo Afisini kwake Kikwajuni wakati akimkabidhi msanii Nasib Abdul maarufu Diamond hati ya leseni ya kufungua vituo vya wasafi Radio na TV. Kwa upande wake Diamond amesema ameamua kufika Zanzibar kutafuta vipaji hivyo kwani anajua Zanzibar kuna vipaji vingi huku akiwataka Wazanzibar wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo ili wapate fursa ya ajira.