BUSHIR NDO BASI TENA MWADUI FC, AONDOKA NA UJUMBE MZITO
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush” amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania bara. Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa. “Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kua kocha Mkuu wa timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka nlokua nkiihudumikia. Ukweli hakuna Mtz hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua ni kwa vp nliisaidia timu hio ktk kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu hiyo na naam niliifanya na lkn c kwa ujanja wng tuu bali na Mungu alinisaidia ktk kuifanikisha kazi hio.. Kuna v2 v3 ambavyo viliniponza hadi kufikia kuipoteza kazi yng hio.. La kwanza ni haki zangu {financially} la pili ni kuusu usajili na la tatu ni kuusiana na chuki na choyo kutoka kwa asst nliyekua nae vl yy nd...