ZU YAPAA KWENDA ETHIOPIA KATIKA MASHINDANO YA AFRIKA
Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar University (ZU) imeondoka Visiwani Zanzibar leo kwenda Makelle nchini Ethiopia kwenye Mashindano ya tisa ya Vyuo Vikuu vya Afrika (FASU) yanayotarajiwa kuanza rasmi July 1-9, 2018. Jumla ya msafara wa watu 23, wakiwemo wachezaji 19 na Viongozi 4 wameondoka saa 3 asubuhi kwa Boti mpaka Dar es salam kisha 12:00 jioni wakaondoka Dar es salam kwa shirika la Ndege la Ethiopia moja kwa moja mpaka Addis Ababa Mjini Ethiopia. Akizungumza na Mtandao huu Bandarini Mjini Unguja wakati kikosi hicho kinaondoka mkuu wa Taaluma wa Chuo hicho Ahmad Majid amesema Chuo chao wamepata nafasi ya kushiriki Mashindano hayo baada ya kufanya vyema katika Mashindano ya Vyuo vya Afrika Mashariki na Kati. Nae Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Mwinyi Ahmad amesema Jumla ya Vyuo 64 kutoka Nchi mbali mbali za Afrika vitashiriki Mashindano hayo ambapo kwa Tanzania nzima ZU ndio pekee watashiriki. Kwa upande wake Kocha Mkuu wa ZU Juma Yussuf Sumbu amewatoa hofu ...