Posts

Showing posts from November, 2017

WACHEZAJI 24 WA ZANZIBAR HEROES WATAKAOKWENDA KENYA KESHO CHALENJ CUP HAWA HAPA

Image
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)  itaondoka nchini kesho Alhamis kuelekea Nairobi, Kenya kwa basi tayari kushiriki mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017. Jumla ya msafara wa watu 34 wakiwemo viongozi pamoja na wachezaji 24 wataondoka saa 6 za mchana kwa Boti kisha wakifika Dar es salam watapanda Basi kwenda mpaka Mkoani Tanga watalazimika kulala hapo, kisha asubuhi yake kuanza safari nyengine mpaka Mombasa na wakifika Mombasa watapanda Treni mpaka Nairobi. Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :- WALINDA MLANGO Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU). WALINZI Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Khei...

KAMARA AWAPONGEZA WAAMUZI WA ZANZIBAR WALOPATA BEJI YA FIFA

Image
Katibu wa Waamuzi wa Soka Zanzibar Muhsin Ali “Kamara” amewapongeza waamuzi wanne wa Zanzibar waliyopata beji ya FIFA. Kamara amesema ni faraja kwa Zanzibar kutoa waamuzi wa nne wenye beji hiyo ya FIFA. Jana Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 wa Tanzania kati yao wanne kutoka Zanzibar katika msimu wa mshindano mwaka 2018. Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kutoka Zanzibar ni Mfaume Ali akiwa ni Muamuzi wa kati huku Wasaidizi walipewa beji hizo Mgaza Kunduli, Mbaraka Haule na mwanamama Dalila Jaffari.

ZANZIBAR HEROES YAAGWA, WAAHIDI KUBEBA KOMBE LA CHALENJ

Image
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeagwa rasmi leo na kukubidhiwa bendera ya Taifa, wimbo wa Taifa pamoja na jezi za Taifa na tayari kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya. Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 24 imekabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma. Akizungumza na Waandishi wa habari Waziri Rashid amesema Wizara yake iko bega kwa bega na wadau wa michezo katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inapiga hatua. Kwa upande wake Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Moroco) amesema yeye ni mzowefu katika Mashindano hayo huku akiwatoa wasi wasi Wazanzibar kwa kusema kuwa vijana wake watafanya vyema katika Mashindano hayo. Mara baada ya kupokea bendera ya Taifa Nahodha wa timu hiyo Suleiman Kassim “Seleembe” amesema kuwa wao wamejiandaa kikamilivu na wanajua wanabeba dhamana kubwa kwa Wazanzibar wote,...

ZANZIBAR HEROES KUAGWA KESHO NA WAZIRI WA MICHEZO

Image
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) , inatarajia kuagwa kesho kwa ajili ya safari yao ya kwenda mjini Kenya, kwenye Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza Disemba 3-17, 2017. Heroes itaagwa saa 9:00 alaasiri na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na michezo Rashid Ali Juma katika ukumbi wa V.I.P Uwanja wa Amaan. Katika Mashindano hayo Heroes imepangwa Kundi  A ambalo lina timu za Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

AMOUR PWINA AIBEBA ZANZIBAR HEROES

Image
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeendelea kucheza michezo ya kirafiki ambapo leo imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 baada ya kuifunga timu ya Kombain iliochaguliwa na Makocha wa Zanzibar, mchezo wa kirafiki uliopigwa saa10 jioni katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Heroes yote yamefungwa na Amour Suleiman (Pwina) dakika ya 35 na 80 ya mchezo. Huu ni mchezo wa tano wa kirafiki kwa Heroes kufuatia awali kutoka sare ya bao 1-1 na Kombain ya Unguja, kisha wakatoka tena sare ya 1-1 na Taifa ya Jang'ombe, wakaifunga Villa United 5-2, jana wakaichapa Dulla Boys 2-1 na leo kushinda 2-0. Kwasasa Heroes watacheza mchezo mmoja tu wa kirafiki kabla ya kuelekea Kenya katika Mashindano ya CECAFA ambapo mchezo wao wa mwisho wa kujipima nguvu utapigwa siku ya Jumanne saa 11:00 za jioni katika uwanja wa Amaan dhidi ya Kombain ya Wachezaji wanaocheza ligi kuu soka Tanzania Bara ambao hawakuitwa Heroes.

KOCHA MOROCCO AMUONGEZA EMANUEL MARTIN ZANZIBAR HEROES

Image
  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi kiungo Mshambuliaji wa timu ya Yanga Emanuel Martin ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza Disemba 3-17, 2017. Katika uteuzi wa awali Martin hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kwenye kikosi cha Heroes kabla ya kubla ya kuchujwa na kubakia 24 ambao wanatarajia kuondoka Zanzibar Jumatano ya Novemba 29. Martin ambae ni mchezaji wa zamani wa JKU ya Zanzibar ataungana na wenzake Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame "Lu...

WACHEZAJI WA 3 WA YANGA WARIPOTI KAMBI YA ZANZIBAR HEROES

Image
Wachezaji watatu wa Klabu ya Yanga SC akiwemo mlinzi wa kushoto Haji Mwinyi Ngwali, Abdallah Haji Shaibu “Ninja” pamoja na Mshambuliaji Mateo Anton Simon, leo wamejiunga na kambi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na kufanya mazoezi pamoja na wenzao katika uwanja wa Amaan. Wachezaji hao walicherewa kufika kambini hapo kwa takribani wiki moja baada ya kuendelee kuitumikia klabu yao kwenye michezo mbali mbali ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

FAINALI YA MASHINDANO YA MAJIMBO KUPIGWA KESHO, ZAWADI YA GARI IPO KWAAJILI YA BINGWA

Image
Fainali ya Soka ya  Mashindano ya Majimbo ya Unguja inatarajiwa kupigwa kesho Jumamosi ya Novemba 25 kati ya timu ya Jimbo la Kwahani dhidi ya Afisi Kuu ya CCM kwenye uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni. Mapema saa 8:00 za mchana siku hiyo kutaanza kutafutwa mshindi wa tatu ambapo watacheza Jimbo la Malindi dhidi ya Kikwajuni. Uledi Said ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo amesema Bingwa atazawadiwa Gari aina ya Carry, medali za dhahabu pamoja na Kombe huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kassim Majaaliwa .

ZANZIBAR HEROES UTAIPENDA TU, YASHINDA 5-2

Image
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) leo kwa mara ya kwanza mwaka huu imefanikiwa kupata ushindi baada ya kuifunga Villa United (Mpira Pesa) mabao 5-2, kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa saa10 jioni katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Heroes yamefungwa na Salum Songoro dakika ya 26, 66, Hamad Mshamata dakika ya 67, Amour Suleiman "Pwina" dakika ya 68 na Kassim Suleiman dakika ya 69 huku mabao yakufutia machozi ya Villa yamefungwa na Abdul swamad "Brown" dakika ya 26 na Mohd Mussa dakika ya 41. Huu ni mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Heroes kufuatia awali kutoka sare ya bao 1-1 na Kombain ya Unguja, kisha wakatoka tena sare kama hiyo na Taifa ya Jang'ombe. Heroes wataendelea tena kucheza michezo ya kirafiki ambapo watacheza na timu ya Dulla Boys siku ya Jumamosi saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Jambiani kisha watamaliza mchezo wa mwisho siku ya Jumapili na Kombain ya Makocha mchezo utakaopigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

KOCHA KING AKIRI HALI YA MIEMBENI CITY NI NZITO, ASEMA KUSHUKA DARAJA SIO DHAMBI LAKINI ATAHAKIKISHA HAWASHUKI

Image
Kocha Mkuu wa timu ya Miembeni City Mohammed Seif "King" amekiri hali ya klabu yake si nzuri kufuatia kucheza michezo saba mfululizo bila ya kupata ushindi hata mchezo mmoja katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja. King amesema kwa mara ya kwanza anakumbana na matokeo mabaya katika maisha yake ya soka lakini bado hajakata tamaa kwenye ligi hiyo huku akiamini vijana wake watapambana kufa na kupona ili wabakie kwenye ligi Kuu. "Balaa balaa, katika historia yangu kwa mara ya kwanza nakumbana na matokeo mabovu kama haya, nakiri tuna matatizo lakini tutapigana kufa kupona ili tubakie kwenye ligi, na kushuka daraja pia sio dhambi lakini vijana watahakikisha tunabakia". Alisema King. Miembeni City ipo nafasi ya 13 wakiwa na alama 1 tu kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja kufuatia kufungwa michezo 6 na kwenda sare mchezo mmoja ambapo mpaka sasa City wapo kwenye mstari mwekundu kwenye ligi hiyo yenye jumla ya timu 14 ambapo timu 6 za chini zitala...

TAIFA YA JANG'OMBE YAIPUNGUZA KAZI KVZ

Image
Baada ya kucheza michezo 6 mfululizo bila ya kupoteza hata mchezo mmoja hatimae leo timu ya KVZ imekubali kufungwa bao 1-0 na Taifa ya Jang'ombe katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa 7 wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan. Bao pekee la Taifa limefungwa na Mohd Abdallah dakika ya 36 ya mchezo.

MZEE ZAM AULA CECAFA

Image
Makamo wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Unguja) Mzee Zam Ali ameteuliwa kuwa mjumbe katika kamati itakayosimamia Mashindano ya Chalenj CUP yaliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Mashindano ambayo yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya. CECAFA wamemteuwa Mzee Zam kwakuwa ni mzowefu katika Mashindano hayo ambapo ni Mzanzibar pekee kwenye kamati hiyo. Wengine waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Mutasim Gafar (Sudan), Abdigaan Arab Said (Somalia), Jacob Odundo (Kenya), Ashinafi Ejigu (Ethiopia), Aimable Habimana (Burundi), Rogers Byamukama (Uganda), Ajong Domasio Ajong (Sudan ya Kusini) na Ahmed Mgoyi (Tanzania Bara). Wengine ni Sunday Kayuni (Tanzania Bara), Mossi Yussuf (Burundi), Celestine Ntangugira (Rwanda), Yigzaw Ambaw (Ethiopia), Bernard Mfubusa (Burundi), Maxim Itur (Kenya), Rogers Mulindwa (Uganda), Bonny Mugabe (Rwanda), Gishinga Njoroge (Kenya), Amir Hassan (Somalia) na Nicholas Musonye (Kenya). ...

ZANZIBAR HEROES KUCHEZA NA TAIFA YA JANG’OMBE KESHO

Image
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kesho Jumatano inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Taifa ya Jang’ombe pambano litakalopigwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan. Zanzibar Heroes inajiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya ambapo wamepangwa kundi A pamoja na ndugu zao Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

CHINONSO APIGA HAT-TRICK CHARAWE WALIPOPIGWA NA CHUONI, MIEMBENI CITY JAMVI LA WAGENI

Image
Mshambuliaji Charles Chinonso amefunga mabao matatu (Hat-trick) na kuiongoza Chuoni kuichakaza Charawe kwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan. Chinonso amefunga mabao hayo katika dakika ya 9, 11 na 26 huku bao jengine likifungwa na Mustafa Zakaria dakika ya 49. Mapema saa 8 za mchana timu ya Miembeni City ikaendelea rikodi yake mbovu ya kufungwa baada ya leo kufungwa 2-1 na Kipanga. Mabao ya Kipanga yamefungwa na Imran Abdul dakika ya 8 na Said Salum dakika ya 32 na lile la Miembeni City limefungwa na Feisal Riambi dakika ya 18. Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya KVZ.

WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES WAINGIA KAMBINI, WAPANGIWA BONGE LA HOTELI

Image
Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar heroes kinachojiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenji CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya leo kimeingia Kambini kwenye Hoteli ya Zanzibar Paradise International Hotel iliyopo Amaan, huku nyota wengine wanaocheza ligi kuu soka Tanzania bara wakitarajiwa kuwasili kuanzia Jumatatu. Kwenye Mashindano ya CECAFA Zanzibar wapo Kundi A ambalo lina timu ya Taifa ya Zanzibar, Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya huku Kundi B kuna Mataifa ya Sudan ya Kusini, Ethiopia, Zimbabwe, Burundi na Uganda. Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Nassor Mrisho (Okapi), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe). Viungo Abd...

BLACK SAILORS YAKAA KILELENI LIGI KUU ZENJ, YAIGONGA MAFUNZO

Image
Timu ya Black Sailors (Mabaharia Weusi), imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya kuichapa Mafunzo bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan jioni ya leo. Sailors imekaa kileleni baada ya kufikisha jumla ya ponti 15 ilizozipata baada ya kushinda mechi tano na kupoteza miwili,itakuwa sawa na JKU ambayo nayo ina alama 15 baada ya kuichapa KMKM mchana wa leo ambapo Sailors anaongoza akiwa na mabao mengi zaidi ya JKU. Bao pekee la Sailors limefungwa na Malik Haji katika dakika ya 25. Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za mchana Polisi watakuwa na kazi ya kucheza na Jang'ombe Boys na saa 10:00 za jioni Kilimani city watakipiga na Zimamoto.

ZANZIBAR HEROES YABANWA NA WATOTO WA KOMBAIN

Image
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imetoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kombain ya Unguja, katika mchezo wa kirafiki lililopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan. Walianza Kombain ya Unguja kufunga bao katika dakika 10 kupitia Is haka Said na Heroes wakajibu mapigo katika dakika ya 66 mfungaji akiwa Ibrahim Hamad Hilika.

ZANZIBAR HEROES YAPANGWA KUNDI LA KIFO, IPO PAMOJA NA TANZANIA BARA MASHINDANO YA CHALENJI

Image
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imepangwa kundi moja na ndugu zao Tanzania Bara kwenye Mashindano ya CECAFA Chalenji CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya. Kundi hilo ni A ambalo lina Mataifa ya Zanzibar, Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya. Kundi B kuna Mataifa ya Sudan ya Kusini, Ethiopia, Zimbabwe, Burundi na Uganda. Ratiba Kamili hii hapa. CECAFA CHALLENGE CUP FIXTURES 2017 IN KENYA Group A FORMAT Group B Ken, Rwa,Lib,Tan, Zan GROUP STAGE,SEMI FINALS-FINAL Uga,Zim,Bur,Eth,S Sud DATES M.NO FIXTURES VENUES-KAKAMEGA,KISM,NAKURU TIME Sunday 3/12/2017 1 2 (Libya v Tanzania) (Kenya v Rwanda) A 2.00PM 4.00 PM Monday  4/12/2017 ...