JKU YAFUFUA MATUMAINI KWENYE KOMBE LA MAPIUNDUZI, MABINGWA WATETEZI AZAM NAO KUANZA KIBARUA KESHO
Klabu ya JKU leo imepata alama tatu muhimu kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Zimamoto bao 1-0 katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan. Bao pekee la JKU limefungwa na Salum Mussa Bajaka dakika ya 1 ya mchezo huo. Badae saa 2:15 usiku kuna mchezo mwengine kati ya Mlandege dhidi ya Taifa ya Jang’ombe kwenye uwanja wa Amaan. Mashindano hayo yataendelea tena kesho Jumapili kwa kupigwa michezo miwili ya kundi A katika uwanja wa Amaan. Saa 10:00 Mabingwa watetezi Azam Fc watacheza na Mwenge na saa 2:15 Jamhuri watakipiga na URA ya Uganda.