KVZ YAIWEKA WAKATI MGUMU KIPANGA, MALINDI HOI KWA KMKM ANASUBIRI MECHI YA MWISHO, KILIMANI CITY MENO NJE YANUSURIKA KUSHUKA DARAJA


Ligi kuu soka ya Zanzibar imeendelea tena leo michezo 3 katika viwanja 2 tofauti.

Saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan KMKM wakaitandika Malindi bila ya huruma mabao 3-1.

Mabao ya KMKM yamefungwa na Vent John dakika 12, Mudrik Muhibu dakika ya 40 na Faki Mwalim dakika ya 87.

Bao pekee la Malindi limefungwa na Salmin Vuai dakika ya 78.

Kwa matokeo hayo Malindi bado ina wakati mgumu ili ibakie katika daraja huku ikisubiri mchezo wa mwisho washinde dhidi Taifa na wakati huo huo waiombee dua Kipanga ifungwe dhidi ya KMKM ndipo watanusurika kushuka daraja.

Malindi imebakisha mchezo 1 baada ya kucheza michezo 33 hadi sasa na mchezo iliosalia upande wao watamalizana na Taifa ya Jang’ombe ambapo kwa ratiba watacheza Jumamosi 06-05-2017 saa10:00 Amaan.

Malindi ipo nafasi ya 13 wana alama 39 katika michezo 33 waliyocheza wameshinda 11 sare 6 na kupoteza 16.


Kikosi cha KVZ

Mchezo mwengine leo umepigwa Saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan KVZ wakaiwekea ngumu Kibanga baada ya kuifunga mabao 2-1.

Mabao ya KVZ yamefungwa yote na Salum Songoro dakika ya 28 na 71, wakati bao pekee la Kipanga limefungwa na Hassan Ali dakika ya 79.

Mchezaji wa Kipanga Yussuf Mwinyi alioneshwa kadi nyekundu na Muamuzi Rashid Farahan "Webb" baada ya kuoneshwa kadi za njano 2.

Bado Kipanga yupo hati hati kubakia ligi kuu na analazimika ashinde mchezo wake wa mwisho dhidi ya KMKM ili abakie salama.

Timu hiyo ambayo inamilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamebakiwa na mchezo mmmoja wa mwisho watamalizana na KMKM.

Katika Msimamo wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 41 kati ya michezo 33 waliyocheza wameshinda 12, sare 5 na wamefungwa 16.

Saa 10 za jioni katika uwanja wa Fuoni Kilimani City ikajiweka mikono salama baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Jang'ombe Boys.

Mabao ya City yamefungwa na Suleiman Kibadeni na Abdillah Seif Bausi huku bao pekee la Boys limefungwa na Ramadhan Khamis.

City kwasasa haimo tena katika vita vya kushuka daraja na vita hivyo imewaachia Kipanga na Malindi.

City wenyewe wanajita watoto wa Mjini wamebakiwa na mchezo mmoja watamalizana na Chuoni na hata wakipoteza hawawezi kushuka tena daraja kwani wamejiweka mikono salama.

Katika msimamo wapo nafasi ya 11 katika michezo 33 waliyocheza wameshinda 14, sare 4 na kupoteza 15 na kwasasa wana alama 46 ambaazo haziwezi kufikiwa na timu za chini yake.

Kati ya Malindi na Kipanga nani ataungana na Kimbunga, Chaka Stars, Miembeni, Kijichi na Mundu kushuka Daraja?, jawabu lake tutalipata kwenye mzunguko wa mwisho ambao utaanza kesho.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa kuanza mzunguko wa mwisho wa 34 ambapo Black Sailors watasukumana na Mundu katika uwanja wa Fuoni.
Kikosi cha Kipanga

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS