Posts

Showing posts from June, 2018

ZU YAPAA KWENDA ETHIOPIA KATIKA MASHINDANO YA AFRIKA

Image
Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar University (ZU) imeondoka Visiwani Zanzibar leo kwenda Makelle nchini Ethiopia kwenye Mashindano ya tisa ya Vyuo Vikuu vya Afrika (FASU) yanayotarajiwa kuanza rasmi July 1-9, 2018. Jumla ya msafara wa watu 23, wakiwemo wachezaji 19 na Viongozi 4 wameondoka saa 3 asubuhi kwa Boti mpaka Dar es salam kisha 12:00 jioni wakaondoka Dar es salam kwa shirika la Ndege la Ethiopia  moja kwa moja mpaka Addis Ababa Mjini Ethiopia. Akizungumza na Mtandao huu Bandarini Mjini Unguja wakati kikosi hicho kinaondoka mkuu wa Taaluma wa Chuo hicho Ahmad Majid amesema Chuo chao wamepata nafasi ya kushiriki Mashindano hayo baada ya kufanya vyema katika Mashindano ya Vyuo vya Afrika Mashariki na Kati. Nae Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Mwinyi Ahmad amesema Jumla ya Vyuo 64 kutoka Nchi mbali mbali za Afrika vitashiriki Mashindano hayo ambapo kwa Tanzania nzima ZU ndio pekee watashiriki. Kwa upande wake Kocha Mkuu wa ZU Juma Yussuf Sumbu amewatoa hofu Waza

KOCHA MUU NAE AUTAKA URAIS WA ZFA, IDADI INAZIDI KUONGEZEKA

Image
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Wanawake (Zanzibar Queens), Mtende Renger na Chuoni Mustafa Hassan (Kocha Muu) nae ametangaza nia ya kugombea Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA). Amesema kwa vile analijua vyema soka la Zanzibar na uzoefu wa kuongoza anao ameona ipo haja kuongoza Chama hicho. Kocha Muu atafanya idadi ya Wadau wa soka kuongezeka walotangaza nia ya kugombea nafasi hiyo baada ya hivi karibuni Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanal, Abdul Hamid Mshangama na kocha wa Zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Bausi wote kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo unaokuja. ZFA watalazimika kufanya uchaguzi kufuatia viongozi wake wakuu kuamua kujiuzulu akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Urais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali hivyo nafasi hizo mpaka sasa zipo tupu huku ikisubiriwa kamati ya Uchaguzi kutangaza tarehe za kuanza harakati za k

TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAAGWA, YAAHIDI KURUDI NA MEDALI ZA DHAHABU

Image
Timu ya taifa ya Riadha ya Zanzibar chini ya miaka 18 itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika June 29 na 30, 2018 jijini Dar es salam imeagwa na kukabidhiwa rasmi bendera ya Taifa ikiwa ni ishara ya kuwakilisha Zanzibar katika mashindano hayo. Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 20, viongozi 5 na Waamuzi 10 imeagwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Amaan V.I.P na kuhudhuriwa na Viongozi wa Wizara hiyo na wadau mbalimbali akiwemo Rais wa chama cha Riadha Zanzibar Abdul hakim Cosmas Chasama na Katibu Mkuu wa chama hicho Suleiman Ame. Akizungumza wakati wa hafla hiyo Naibu Lulu amesema Wizara yake iko bega kwa bega na wadau wa michezo huku akiwataka kupambana ili kuchukua ubingwa ambapo amewasisitiza kudumisha nidhamu kwani ndio silaha muhimu kwao. Nae Rais wa chama cha riadha Zanzibar Abdul hakim Cosmas Chasama, amesema

RAZA AUTAKA URAIS WA ZFA, ATANGAZA RASMI NIA

Image
M wakilishi wa jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanal ametangaza nia ya kugombea Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kwa ajili ya kuliteka maendeleo ya mchezo huo.   Raza ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari za michezo katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja. Mwanamichezo huyo ambae aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya michezo kwa Rais wa awamu ya tano Dk Salmin Amour, amesema nia hiyo imekuja baada ya kuona soka la Zanzibar kuanguka, hivyo ameona ipo haja kutangaza nia ili kuja kulikomboa. Amesema atahakikisha anaukuza mchezo huo kwani atashirikiana ipasavyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inaonekana ipo mstari wa mbele kwenye michezo. ZFA watalazimika kufanya uchaguzi kufuatia viongozi wake wakuu kuamua kujiuzulu akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Urais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali hivyo nafasi hizo mpaka sasa zipo tupu

MRAJIS AWAJIA JUU ZFA, KUHUSU KUTAKA VIONGOZI WALIOJIUZULU WAREJESHWE

Image
  Afisi ya Mrajis wa vyama vya Michezo Zanzibar imepinga maamuzi ya Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Taifa) yakuzikataa Barua za kujiuzulu kwa viongozi wakuu wa Chama hicho. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza amesema Ofisi yake inatambua uhalali wa kujizulu viongozi hao ambao waliandika barua wenyewe. Juzi wajumbe 13 wa ZFA walikutana Gombani Pemba na kuzikataa barua za viongozi hao wa juu waliojuzulu huku wajumbe hao wakimtaka Katibu mkuu wa ZFA kuwaandikia Barua aliyekuwa Rais na Makamo wa Urais ZFA Pemba Ravia Idarous Faina na Ali Mohammed Ali kurejeshwa kwenye nafasi zao. Viongozi watatu wakubwa wa ZFA akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Rais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali waliandika barua kujiuzulu nafasi zao kuongoza Chama hicho. Suleiman Pandu Kweleza-Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar

KIONGOZI MWENGINE MKUBWA WA ZFA AJIUZULU

Image
Makamo wa Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA PEMBA) Ali Mohammed nae amejiuzulu rasmi nafasi yake kuongoza chama hicho. Taarifa kama hiyo ni muendelezo ndani ya chama hicho kufutia viongozi wengine wajuu akiwemo akiwemo alokuwa Rais Ravia Idarous Faina pamoja na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali nao kujiuzulu siku chache zilizopita. Inaonekana wazi chanzo cha viongozi wote hao kujiweka pembeni ni kuhusu uzembe uliofanywa kati yao na kupelekea timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana U-17 (Karume Boys) kuondolewa katika Mashindano ya CECAFA na kupigwa faini ya Dola elfu kumi na tano pamoja na kuzuiliwa kutoshiriki Mashindano yote yatakayoendeshwa na Baraza hilo mpaka kulipa kwa faini hiyo kwa kosa la kupeleka wachezaji wakubwa waliozaliwa chini ya tarehe 01/01/2002. ZFA ilizungumza na Vyombo vya Habari kupitia Makamo wake huyo (Ali Mohammed) na kukataa kuwa CECAFA hawajatuma ufafanuzi wa umri kwa wachezaji walotakiwa kushiriki mashindano ya CECAFA ya Vijana (U-17

RIADHA NOMA ZANZIBAR, WATINGA FAINALI,SOKA KIKAPU, MIKONO, MEZA KAMA KAWAIDA WATESA

Image
Kikosi cha Mpira wa Kikapu kanda ya Unguja MASHINDANO ya Umisseta yanazidi kushika kasi hapa Mwanza, huku timu ya kanda ya Pemba na Unguja zikiendelea kufanya vyema kwa baadhi ya michezo. Katika michezo iliyochezwa leo nyakati za asubuhi, mchana na jioni, timu ya riadha Kanda ya Unguja imeweza kutinga hatua ya fainali baada ya kutamba kwenye mbio za mita 100 wanaume na wanawake, ambapo walioshinda ni wanaume ni Mohamed Rashid na Omar Rashid, wanawake ni Naima Ali na Nasra Abdalla Abdalla. Lakini kanda ya Pemba kwa upande wa riadha haikufanya vyema baada ya wakimbiaji wake kushindwa kuingia hatua ya fainali kwenye mbio za mita 100 , wakati mbio za mita 400 iliweza kushika nafasi ya nne na sita katika makundi yao. Wakati   huo huo kanda ya Unguja imeweza kutoka na ushindi katika mchezo wa mpira wa kikapu ambapo ilicheza michezo miwili tofauti. Mchezo wa kwanza iliweza kutoka na ushindi wa   vikapu 62-13 dhidi ya mkoa wa Njombe, wakati mchezo wa pili Unguja iliishinda

ZANZIBAR YAENDELEA KUTESA UMISSETA KWENYE SOKA, MIKONO NA RIADHA

Image
Kikosi cha Mpira wa Mikono Unguja TIMU ya kanda ya Unguja mpira wa miguu imeendelea kufanya vyema katika mashindano ya Umisseta, baada ya leo kuwafunga mkoa wa Njombe mabao 2-0. Mchezo huo ulikuwa mzuri na kupenda kwa muda wote, Unguja ilianza kupanga mashambulizi ili kutafuta bao la mapema, juhudi ambazo zilifanikia katika dakika ya 15 kwa bao lililofungwa Ali Hassan. Baada ya bao hilo kila timu iliendelea kucheza kwa umakini mkubwa ili kutafuta bao, na juhudi hizo zilizaa matunda kwa upande wa Unguja, baada ya kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Talib Ali dakika ya 30. Kwa upande wa mpira wa Wavu bado mambo hayajawa mazuri baada ya kuendelea kupoteza michezo yake kwa kanda zote Unguja na Pemba. Katika michezo hiyo kanda ya Pemba   ilipoteza mchezo baada ya kufungwa seti 3-0 na Singida, na kanda ya Unguja ilipoteza mchezo dhidi ya Manyara kwa kufungwa seti 3-2. Kwa upande wa mchezo wa mpira wa Kikapu kanda ya Unguja ilitoka na ushindi   baada ya kuwafu

ZANZIBAR YAZIDI KUNG’ARA UMISSETA, INAONGOZA MAKUNDI YAO

Image
TIMU za Zanzibar zimeendelea kufanya vyema katika michezo yake mbali mbali iliyocheza leo, baada ya kuibuka na ushindi na kuleta matumaini makubwa ya kuingia hatua ya robo fainali kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa kwa Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yanoyoendelea katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza. Katika michezo iliyopigwa leo, upande wa Soka timu ya Unguja imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Morogoro, mchezo ambao ulikuwa mkali na kuvutia kwa muda wote. Katika pambano hilo, licha ya kufungwa Morogoro walionesha kiwango kizuri na kuwabana Unguja ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika cha hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake. Kipindi cha pili timu zote zilirudi na nguvu mpya kila mmoja akitaka kupata bao la mapema, lakini bahati hiyo iliwaangukia Unguja baada ya kuandika bao hilo pekee lililokwamishwa wavuni dakika ya 72 kupitia kwa Ali Hassan (Ndimbo). Mchezo mwengine uliwakutanisha kanda ya Pemba ambayo ilikuwa

RAIS WA ZFA AJIUZULU RASMI

Image
Rais wa ZFA wa Kati kati Ravia Idarous Faina  Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Ravia Idarous Faina ameandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake na sasa wataungana na Makamo wa Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali na Mkurugenzi wa ufundi Abdulghan Msoma ambao walitangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Mei, 2018. Katibu mkuu wa ZFA Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea barua hiyo ya Ravia. “Ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake, barua ameileta leo Jumatano saa 9 za mchana”. Alisema Tedy. Ravia alipokea kijiti hicho cha Urais kutoka kwa Amani Ibrahim Makungu mwaka 2013. Yote hayo inawezekana ikawa sababu kufuatia Zanzibar kupitia timu yake ya Vijana ya Karume Boys kuondolewa katika Mashindano ya Cecafa ya Vijana yaliyofanyika hivi karibuni nchini Burundi ambapo Karume Boys licha ya kuondoshwa katika Mashindano pia walipigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo walikwenda kinyume na kanuni ya Ma

TIMU ZA ZANZIBAR ZAANZA VYEMA MASHINDANO YA UMISSETA

Image
Wawakilishi wa Zanzibar katika  Mashindano ya Sanaa na Michezo Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa upande wa Soka Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba zimeanza vyema Mashindano hayo baada ya kupata ushindi katika michezo yao ya kwanza. Timu ya Kanda ya Pemba wamefanikiwa kuwafunga 1-0 Mabingwa watetezi timu ya Songwe huku bao pekee la Pemba likifungwa na Mohd Said dakika ya 15. Nao Kanda ya  Unguja wamewafunga Mtwara mabao 2-1 kwa mabao ya Said Saleh (Chidi Carrick ) na Talib Ali Issa huku bao pekee la Mtwara likifungwa na Mohd Juma, michezo yote hiyo imechezwa katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu hapa Butimba, Mwanza. Mashindano hayo yataendelea tena leo Jumanne June 5, 2018 hapa hapa Butimba ambapo timu ya Soka ya Kanda ya Pemba watajitupa uwanjani kucheza na Shinyanga mchezo utakaopigwa majira saa 1:30 za asubuhi. Kwa upande wa Unguja soka watacheza tena kesho Jumatano June 6, 2018 dhidi ya Morogoro. Michezo mengine ya Mpira wa Kikapu (Basketball) na mpira wa Wavu (Voll

UMISSETA ZANZIBAR WAWASILI SALAMA MWANZA, WAPO TAYARI KUBEBA UBINGWA

Image
Msafara wa wanamichezo 170 kutoka Unguja na Pemba wamewasili Mwanza salama, kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Michezo na Sanaa kwa Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) ambayo yanatarajia kuanza kesho kwenye viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba. Akizungumza na Mtandao huu Meneja wa timu ya kanda ya Unguja Abdalla Juma amesema vijana wote kwa ujumla wao Unguja na Pemba wapo katika hali nzuri na hakuna mgonjwa, jambo ambalo ni la kushukuru na wapo tayari kwa ajili ya mashindano hayo. Nae mratibu wa michezo Kanda ya Pemba Ali Hussein amesema wamejiandaa kutoa upinzani mkali mwaka huu huku akisema Unguja na Pemba wapo kitu kimoja kuhakikisha wanaiwakilisha vyema Zanzibar katika Mashindano hayo. Kwa upande wao makocha wa michezo mbali mbali kwa pamoja wameshukuru hali ya hewa ya Mwanza ambayo wamesema haina tofauti kubwa na ile ya Zanzibar, jambo ambalo litawasaidia kushiriki vyema michezo hiyo licha ya jua kali lililokuwepo. Kwa upande wa wachezaji ambao walizungumza na mtanda