MRAJIS AWAJIA JUU ZFA, KUHUSU KUTAKA VIONGOZI WALIOJIUZULU WAREJESHWE


 Afisi ya Mrajis wa vyama vya Michezo Zanzibar imepinga maamuzi ya Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Taifa) yakuzikataa Barua za kujiuzulu kwa viongozi wakuu wa Chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza amesema Ofisi yake inatambua uhalali wa kujizulu viongozi hao ambao waliandika barua wenyewe.

Juzi wajumbe 13 wa ZFA walikutana Gombani Pemba na kuzikataa barua za viongozi hao wa juu waliojuzulu huku wajumbe hao wakimtaka Katibu mkuu wa ZFA kuwaandikia Barua aliyekuwa Rais na Makamo wa Urais ZFA Pemba Ravia Idarous Faina na Ali Mohammed Ali kurejeshwa kwenye nafasi zao.

Viongozi watatu wakubwa wa ZFA akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Rais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali waliandika barua kujiuzulu nafasi zao kuongoza Chama hicho.
Suleiman Pandu Kweleza-Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS