HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

Jina lake ni Khamis Mussa “Rais” ambae hadi leo bado rekodi yake haijavunjwa na mchezaji yoyote kwenye mechi ya Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.
Ni Striker hatari wa Jang’ombe Boys, huyu jamaa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zilipokutana timu hizo.
Ameshafunga mabao mawili mpaka sasa na hakuna mwengine yeyote alifika mabao hayo.
Rais amefunga mabao hayo katika mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016.
Mabao hayo alifunga katika dakika ya 45 na 53 huku akimuweka katika wakati mgumu mlinda mlango hatari wa Taifa ya Jang’ombe Ahmed Ali “Salula”.
Wachezaji wengine ambao wanaweza kuivunja rikodi hiyo kwa upande wa timu ya Taifa ni Mkongo Baraka Ushindi, Mkenya Mohd Said “Mess”, Omar Yussuf Chande na Hassan Seif “Banda”  ambao wote wamefunga bao moja tu.
RIKODI USO KWA USO BOYS V/S TAIFA
WAMEKUTANA MARA 5 MPAKA SASA
Msimu wa mwaka 2012-2013
Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Taifa 1-2 Boys
Ligi ya Waamuzi dakika 90 Taifa 0-0 Boys, Penalti Taifa 4-5 Boys
Novemba 19, 2016
Bonanza la Coconut FM Taifa 2-0 Boys
Mabao yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess.
Disemba 10, 2016
Ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa kwanza Taifa 2-2 Boys
Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53.
Disemba 30, 2016
Kombe la Mapinduzi 2017 Taifa 1-0 Boys
Bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda”.
Khamis Mussa "Rais"

Comments