Posts

Showing posts from May, 2018

KIONGOZI MKUBWA WA ZFA AJIUZULU KUHUSU SAKATA LA KARUME BOYS, KUMBE WALIPOKEA UJUMBE KUTOKA CECAFA

Image
Katibu Mkuu wa chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea Barua ya kujiuzulu kwa Makamo wa Rais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali kufuatia sakata la timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana (Karume Boys) kuodoshwa katika Mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Burundi Mwaka huu. Tedy amesema Mzee Zam ameiwasilisha barua hiyo mapema leo huku akikiri kupokea taarifa kutoka kwa CECAFA inayofafanua kuhusu umri wa Mashindano ambapo amewaomba msamaha kwa kusema alipitikiwa. Amesema kweli walipokea ufafanuzi wa umri kutoka CECAFA kupitia email ya Mzee Zam na mwenyewe alikiri huku akisema alisahau, hivyo kutokana na kadhia hiyo ameamua kuomba kujiuzulu. Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo walikwenda kinyume na kanuni ya Mashindano. Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini d

MKURUGENZI WA UFUNDI WA ZFA AOMBA KUJIUZULU HUKU KATIBU WA WIZARA YA MICHEZO AKITHIBITISHA ZFA WALIPOKEA BARUA KUTOKA CECAFA KWA LILE SWALA LA KARUME BOYS

Image
Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Abdulghan Msoma ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake baada ya kukosa ushirikiano wa kutosha ndani ya chama hicho. Msoma ameandika barua hiyo kwenda kwa Rais wa ZFA ambapo amesema ZFA hakuna utendaji ndio mana kaamua kukaa pembeni huku akisema wakati mwengine yanatoka maamuzi ambayo hayajajadiliwa katika vikao kwenye chama hicho. Nae katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Omar Hassan ‘King’ amesekiri kuwa ZFA wamethibitisha kupokea Barua kutoka CECAFA kuhusu ufafanuzi wa umri wa Mashindano ya Vijana yaliyomalizika hivi karibuni Burundi ambapo Zanzibar kupitia timu yao ya Karume Boys iliondoshwa kutokana na kupeleka wachezaji waliozidi umri ambapo kwasasa mambo yanaanza kufichukwa kwa kuwa kuna taarifa ya kuwa Makamo wa Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali amesimamishwa kuhusu sakata hilo. Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa

MLANDEGE NA MALINDI ZAREJEA LIGI KUU SOKA ZANZIBAR MSIMU UJAO

Image

BINGWA WA LIGI KUU ZENJ HAJULIKANI ATAPEWA NINI, CENTRAL WILAYA YA MJINI WATATOA MILIONI 1 KWA BINGWA

Image
Wajumbe wa Kamati ya Central W Mjini wakiwa pamoja na Mkanga (Aliyevaa Shati wa kati) Kamati ya central Wilaya ya Mjini imekabidhiwa shilingi Milioni tatu kwaajili ya Zawadi kwa washindi 6 wa Mashindano yao ya Ligi na ya Kombe la Mtoano yanayotarajiwa kumailizika Jumamosi ya Mei 12, 2018 asubuhi katika uwanja wa Amaan. Akiwakabidhi fedha hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Raskazone Trader Ali Khatib Mkanga amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia michezo hasa ngazi za chini kwani ndiko vipaji vinakotokea. Mkanga pia amewapongeza viongozi hao wanaosimamia soka la Vijana ndani ya Wilaya ya Mjini kwa mafanikio yao ya kusimamia vyema Soka hilo la Vijana. Nae katibu msaidizi wa Kamati ya Central Wilaya ya Mjini Alawi Haidar Foum amempongeza Mkanga kwa kusaidia soka la Vijana huku akiwataka watu wengine wasaidie Michezo hasa Vijana kwani ndio msingi imara wa Maendeleo. Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa kamati hiyo Ali Suleiman (Kisheta) amesema kamati yao imepanga ku