MKURUGENZI WA UFUNDI WA ZFA AOMBA KUJIUZULU HUKU KATIBU WA WIZARA YA MICHEZO AKITHIBITISHA ZFA WALIPOKEA BARUA KUTOKA CECAFA KWA LILE SWALA LA KARUME BOYS


Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Abdulghan Msoma ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake baada ya kukosa ushirikiano wa kutosha ndani ya chama hicho.

Msoma ameandika barua hiyo kwenda kwa Rais wa ZFA ambapo amesema ZFA hakuna utendaji ndio mana kaamua kukaa pembeni huku akisema wakati mwengine yanatoka maamuzi ambayo hayajajadiliwa katika vikao kwenye chama hicho.

Nae katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Omar Hassan ‘King’ amesekiri kuwa ZFA wamethibitisha kupokea Barua kutoka CECAFA kuhusu ufafanuzi wa umri wa Mashindano ya Vijana yaliyomalizika hivi karibuni Burundi ambapo Zanzibar kupitia timu yao ya Karume Boys iliondoshwa kutokana na kupeleka wachezaji waliozidi umri ambapo kwasasa mambo yanaanza kufichukwa kwa kuwa kuna taarifa ya kuwa Makamo wa Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali amesimamishwa kuhusu sakata hilo.

Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 huku Zanzibar ikuwapeleka wachezaji 12 waliozaliwa 2001 jambo ambalo ZFA wamesema hawana taarifa kama wachezaji walotakiwa waliozaliwa 2002 ambapo wao walijuwa walokuwa na umri chini ya miaka 17 hivyo hata walozaliwa 2001 ikiwa bado hawajafika miaka 17 walifikiri wanaruhusiwa ndio mana wakaenda nao ambapo katibu Mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye alisema kuwa ZFA walitumiwa ufafanuzi wa umri kwenye Barua Pepe labda hawazisomi tu.

Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS