Posts

Showing posts from April, 2017

MLANDEGE HOI KWA AMAN FRESH, KESHO KWEREKWE CITY NA GULIONI

Image
Mchezo wa kwanza hatua ya 4 bora ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini kati ya Mlandege dhidi ya Aman Fresh wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1 mchezo uliopigwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Aman Fresh ndio wa mwanzo kupata bao katika dakika ya 51 kupitia Rashid Suleiman Said. Bao la Mlandege limefungwa kwa penalti na Saleh Salum "Neymar" dakika ya 86. Lakini munamo dakika ya 63 Mohd Abdallah "Edi Mundo" wa Mlandege alikosa penalti. Mchezo mwengine utapigwa kesho Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mchezo huo ni wa kulipana kisasi kwani msimu huu timu hizo zilikutana Jumapili ya Disemba 4, 2016 katika hatua ya Makundi ambapo Gulioni alipigwa mabao 5-0 dhidi ya City, sasa sijui kesho itakuaje Gulioni atalipa kisasi au City ataendeleza ubabe. Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo

RAZA ATOLEWA MASHINDANO YA MAJIMBO NA WAUZA LA TONGE TONGE

Timu ya Jimbo la Uzini imetolewa katika hatua ya robo fainali kwenye Mashindano ya Majimbo baada ya kufungwa na Jimbo la Malindi kwa penalti 4-3 kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare ya 2-2, mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Polisi Ziwani. Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja wa robo fainali katika uwanja wa Polisi Ziwani kati ya Timu ya Afisi kuu ya CCM dhidi ya Kaskazini B. Bingwa wa Mashindano hayo atazawadiwa Gari aina ya Carry.

MIEMBENI WATIA AIBU LIGI KUU ZENJ, WAFIKA UWANJANI NA WACHEZAJI 9 TU

Image
Timu ya Miembeni wazee wa kwala leo imeonesha kituko katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kufika kiwanjani hapo wakiwa wachezaji 8 pekee. Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan ambapo Kwala walikuwa wanacheza na Mafunzo. Mchezo umeanza huku Miembeni wakiwa pungufu (9) na baadae wakatimia 11, wakaenda mapumziko Mafunzo 3-0 Miembeni . Waliporudi kipindi cha pili wakaingia 8 wakacheza mchezo huo mpaka dakika ya 54 Miembeni wakabakia wachezaji 6 uwanjani kufuatia wachezaji wake wengine wawili kushindwa kuendelea na mchezo, ndipo hapo Muamuzi Mfaume Ali Nassor kulazimika kuuvunja mchezo huo huku Mafunzo akiwa mbele kwa mabao 4-0. Mchezo mwengine umepigwa saa 10 za jioni ambapo JKU akaifunga Mundu mabao 4-0. Ligi hiyo itaendelea tena Jumanne. J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku. Jumatano 3/5 KMKM vs Malindi saa 8:00 Am

KAMATI YA KATIBA YA ZFA YAWATOWA HOFU WAZANZIBAR KUHUSU KATIBA WATAKAYOIREKEBISHA KUENDANA NA MATAKWA YA CAF

Image
Kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba ZFA ili kuendana na matakwa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” inatarajia kuiwasilisha rasimu ya awali ya katiba kwa takribani wiki mbili kwa Chama cha Soka Zanzibar “ZFA”. Akizungumza na kisanduzenj.blogspot.com katibu wa kamati hiyo Saleh Ali Said ambae pia ni Mwanasheria wa ZFA amesema wameanza kazi za kuandaa katiba hiyo ambapo jana Jumamosi wameanza kazi ya awali na zoezi hilo litachukua muda mfupi tu kukamilika. “Tushaanza kazi hiyo mana tumekutana wajumbe na zoezi hili si kubwa sana, tutachukua wiki moja na nusu au mbili tu kukamilisha rasimu ya awali ya katiba kisha tutaiwasilisha kwa ZFA, Wazanzibar wasiwe na hofu katiba hiyo itakuwa inaendana na matakwa ya Shirikisho la Soka Afrika pamoja na kwa maslahi ya Mazingira ya Visiwa vya Zanzibar”. Alisema Saleh. Awali Kamati hiyo ilihitaji fedha kwaajili ya bajeti yao ili kufanikisha zoezi hilo ambapo ilihitaji jumla ni shs Milioni thalasini na tisa ,

HAPATOSHI LEO USIKU MLANDEGE V/S AMAN FRESH, KESHO WATOTO WA MOO KWEREKWE CITY V/S GULIONI 4 BORA WILAYA YA MJINI

Image
Hatua ya nne bora ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini ambapo wanatafutwa Bingwa na Makamo Bingwa wa Wilaya hiyo watakaowakilisha katika Mabingwa wa Wilaya kupigania nafasi za kupanda daraja la 2 Taifa kwa msimu ujao, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo April 30, 2017 kati ya timu ya Mlandege dhidi ya Amani Fresh mchezo ambao utapigwa saa 1 ya usiku. Mchezo mwengine utapigwa kesho Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mchezo huo ni wa kulipana kisasi kwani msimu huu timu hizo zilikutana Jumapili ya Disemba 4, 2016 katika hatua ya Makundi ambapo Gulioni alipigwa mabao 5-0 dhidi ya City, sasa sijui kesho itakuaje Gulioni atalipa kisasi au City ataendeleza ubabe. Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”, Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa kuch

WAUZAJI KARAFUU ZSTC WAWATIA ADABU WAZIMA UMEME ZECO MASHINDANO YA MEI MOSI

Image
TIMU YA SHIRIKA la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mwaka huu 2017 wa Mashindano ya Mei Mosi baada ya kuwafunga mabingwa Watetezi timu ya Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) mabao 2-0 fainali ambayo imepigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Amaan. Mabao yote ya ZSTC yamefungwa na Majid Omar Majid ambae alionesha makali yake katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na mvua kiwanjani hapo. Katika Mashindano ya mwaka huu 2017 Mfungaji bora Bora amefanikiwa kuwa Habibu Juma Ali aliyefunga mabao 5 katika Mashindano hayo,  huku kipa bora akiwa Mbarouk Juma Ali wa Shirika la Bandari na Muamuzi bora ni Juma Makame. Mashindano hufanyika kila mwaka na kuwapa fursa wafanyakazi wa Mashirika mbali mbali kuonesha viwango vyao. Mh Ayoub Mohammed Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akimkabidhi zawadi Juma Makame Muamuzi Bora

DK SHEIN AHIMIZA WAZANZIBAR KUWA NA UZALENDO KWA KUIPENDA ZANZIBAR HEROES, HATA WAKIPENDA KINA ARSENAL LAKINI UZALENDO MUHIMU

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amewataka Wanaanchi wa Jimbo la Uzini kuwa na uzalendo wa kupenda chao na kukithamini kwani mtu chake ambapo amewasisitiza kuipenda timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”. Dkt. Shein ameyasema hayo asubuhi ya leo huko Dunga Wilaya ya Kati kwenye Ukumbi wa Walimu alipokuwa akiwakabidhi Vifaa vya Michezo timu 46 za soka za Jimbo la Uzini ambao wamepewa vifaa hivyo na Muwakilishi wao Mh Mohd Raza. Amesema katika uzalendo lazima uanze kukipenda chako huku akiwanasihi Vijana hao kuipenda timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”. “Katika Uzalendo mtu hukipenda chake kwanza, hebu ipendeni kwanza Zanzibar Heroes timu yenu ya Taifa ya Zanzibar, ipendeni Timu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania “Taifa Stars”, muzipende timu zenu huo ndio uzalendo”. Alisema Dkt Shein. Hata hivyo Dkt Shein amesisitiza kuwa hajamzuia mtu kupenda klabu za Ulaya lakini mtu asipende sana cha nje akakisahau za kwao.

TAIFA YA JANGOMBE LEO YAJIFARIJI, BADRU ASHUSHA PRESHA ZA MASHABIKI

Image
Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja umeanza jioni ya leo katika uwanja wa Amaan kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Chuoni. Katika pambano hilo Taifa amepata ushindi wa mabao 2-1. Chuoni ndio wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 kupitia Ali Rajab, na bao hilo likadumu hadi kipindi cha kwanza kimemalizika. Kipindi cha pili kuanza tu sekunde 35 Adam Ibrahim akarejesha bao hilo na dakika 59 Ali Badru akafunga bao la pili. Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja majira ya saa1 usiku kati ya Polisi dhidi ya Kijichi.

SINA TAARIFA ZOZOTE ZA KUFUNGIWA MAISHA NISIJIHUSISHE NA SOKA, KAMA WAMEFANYA HIVYO ZFA, HUO NI UHUNI-HUSSEIN

Image
InakaribiaWiki moja sasa tangu kufungiwa kwa wajumbe wawili wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Mjini Hussein Ali Ahmada na Masoud Attai kutoka Wilaya ya Kazkazini “A” ambao wote kwa pamoja wametimuliwa ndani ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” na kusimamishwa maisha kutojihusisha na shughuli za soka, leo yameibuka mapya kutoka kwa Hussein ambae amesema hana taarifa rasmi za kufukuzwa kwake na yeye anajua bado ni Mjumbe wa ZFA Taifa kutoka ZFA Wilaya ya Mjini. Amesema amesikia kwenye vyombo vya habari tu kama amefungiwa lakini hajapewa uthibitisho wowote na ZFA na kama wamefanya hivyo ZFA kitendo hicho ni uhuni tu. “Mimi nimesikia tu kwenu Waandishi, lakini sijapewa taarifa rasmi mpaka leo, hivyo mimi taarifa hizo sijazielewa, kwasababu ukifungiwa upewe barua maalum na ujuwe sababu gani zilizopelekea mimi kufungiwa, kama mimi nimesimamishwa si tatizo lakini nipewee taarifa rasmi na wafate taratibu, mana sielewi hata katiba gani ambayo wametumia kunisimamisha kama munavyosema,

4 BORA DARAJA LA PILI WILAYA YA MJINI KUANZA APRIL 30, MLANDEGE, KWEREKWE CITY, GULIONI NA AMAN FRESH KUPIGANA

Image
Hatua ya nne bora ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini ambapo wanatafutwa Bingwa na Makamo Bingwa wa Wilaya hiyo watakaowakilisha katika Mabingwa wa Wilaya kupigania nafasi za kupanda daraja la 2 Taifa kwa msimu ujao, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake April 30, 2017 kati ya timu ya Mlandege dhidi ya Amani Fresh mchezo ambao utapigwa saa 1 ya usiku. Mchezo mwengine utapigwa Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali amesema ligi yao itakuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote 4 zilizofanikiwa ni ngumu. “Hii 4 bora ya mwaka huu si mchezo kwa vile timu zote zinaushindani wa hali ya juu”. Alisema Yahya. Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”, Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa kucheza li

HOMA INAZIDI KUWA KALI LIGI KUU ZENJ YAKARIBIA KUMALIZIKA KUTAFUTA TIMU 8 BORA NA 12 ZAKUSHUKA DARAJA

Image
Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja unatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan. Ratiba ya mzunguko wa 33 ligi kuu ya soka Zanzibar kanda ya Unguja hiyo. Ijumaa 28/4 Taifa vs Chuoni saa 10:00 Amaan. J/mosi 29/4 Polisi vs Kijichi saa 10:00 Fuoni J/pili 30/4 Mafunzo vs Miembeni saa 8:00 Amaan J/pili 30/4 JKU vs Mundu saa 10:00 Amaan J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku. Jumatano 3/5 KMKM vs Malindi saa 8:00 Amaan. Jumatano 3/5 Kipanga vs KVZ saa 10:00  Amaan. Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66 huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi ya nne zote bado hazijajihakikishia kutinga hatua hiyo wakiwa na alama sawa 58 huku Polisi ambayo inakamata nafasi

TAIFA YA JANG’OMBE YAPIGWA FAINI KWA FUJO LA MASHABIKI WAKE KWENYE MCHEZO WA JANA

Image
Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ng’ambo) imepigwa faini ya Shilingi laki mbili kwa utovu wa nidhamu ambao umefanywa na Mashabiki wake ambao wamerusha chupa za maji na kusababisha mpira kusimama kwa dakika 10 kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa katika Uwanja wa Amaan ambapo Taifa alifungwa bao 1-0. Faini hiyo inatakiwa kulipwa si zaidi ya tarehe  4/5/2017 ambapo Maamuzi hayo yameamuliwa na kamati Tendaji ya ZFA Unguja iliyokutana asubuhi ya leo. Akizungumza na Mtandao huu Afisa Habari wa ZFA Ali Bakar “Cheupe” amesema kamati Tendaji imeipitia ripoti ya mchezo huo kati ya Boys na Taifa na kugunduwa kuwa Mashabiki wa Taifa wamefanya Utovu wa nidhamu. “Kamati Tendaji ya ZFA imepitia ripoti ya mchezo huo na katika ripoti hiyo imeripotiwa baadhi ya Mashabiki na Wapenzi wa timu ya Taifa bila ya uhalali wowote wamefanya utovu wa nidhamu kwa kurusha chupa za maji na kusababisha mpira kusimama, hivyo wamepigwa faini ya S

MECHI ZA MWISHO ZA LIGI KUU ZENJ ZAPELEKEA KUBADILIKA KWA RATIBA ILI KUEPUSHA KUPANGA MATOKEO

Image
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imebakisha mizunguko miwili ili kumalizika lakini homa kali zaidi ni kila mmoja anataka kujua ni timu gani ambazo zitafanikiwa kucheza 8 bora na timu zipi 6 ambazo zitateremka daraja katika hatua ya awali. Leo Kamati Tendaji ya ZFA Unguja  imeamua kufanya mabadiliko madogo ya ratiba baada ya kupokea agizo kutoka kwa uongozi wa uwanja wa Amaan sambamba na kuepusha upangaji wa matokeo. Mabadiliko ambayo yamefanywa yamepelekea siku ya Ijumaa ya April 28, 2017 kuchezwa michezo mitatu ambapo KMKM watasukumana na Malindi saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan ambapo muda huo huo katika Uwanja wa Fuoni watacheza kati ya Kipanga dhidi ya KVZ , na mchezo wa Chuoni dhidi ya Taifa ya Jang’ombe utapigwa saa 1:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan. Siku ya Jumamosi ya April 29, 2017 utapigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Fuoni saa 10:00 za jioni kati ya Kijichi dhidi ya Polisi. Mei 4, 2017 kutapigwa michezo miwili saa 10:00 za jioni katika

MIEMBENI CITY YAITAKA LIGI KUU KWA HAMU KUBWA

Image
Timu ya Miembeni city imefanikiwa kupata alama tatu muhimu jioni ya leo baada ya kuifunga timu ya Sebleni United katika mchezo wa 4 bora ligi daraja la kwanza Taifa uliopigwa katika Uwanja wa Amaan. Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa mabao ya Miembeni City yamefungwa na Ahmed Keis dakika ya 79 na Issa Chitwanga dakika ya 84. Mchezo mwengine umepigwa saa 1 za usiku katika uwanja huo wa Amaan ambapo timu ya Charawe ikafanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2. Kwa matokeo hayo Miembeni City imezidi kujipa matumaini ya kupanda ligi kuu msimu ujao ambapo wakifanikiwa kupita hapo watakutana na timu nyengine ambazo zitabakia kwenye ligi kuu msimu huu pamoja na wao wanne wawili kutoka Pemba na wawili Unguja ili kupanga mfumo gani watumie kupatikana timu 12 za ligi kuu msimu ujao. City mchezo wa awali waliichapa Charawe mabao 2-0 ambapo mpaka sasa wanaongoza wakiwa na alama 6 kwa michezo miwili huku Charawe ikishika nafasi ya pili kwa alama 3 na Ngome ikishika nafa

ALI MOHAMMED AZIPA TANO TIMU ZA PEMBA ZILIZOTINGA 8 BORA

Image
MAKAMO wa Rais wa ZFA Taifa, Ali Mohamed amezipongeza timu za Pemba ambazo zimeingia katika hatua ya 4 bora na kuzitaka kujiandaa katika michuano ya Super 8, ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. Akizungumza na viongozi wa timu hizo, huko katika ofisi za ZFA Gombani Chake Chake, Makamo alisema licha ya timu hizo kufanya vizuri katika michezo yao, lakini wana kazi kubwa ambayo imewaelekea. Alifahamisha kuwa kutokana na kiwango ambacho walikionyesha wakati wakisaka nafasi hiyo, timu hizo zilionekana kiwango chao kiko chini sana, hivyo inatia wasiwasi kwa timu za Pemba hazitoweza kuleta ushindani kwa timu za Unguja. “Tumemaliza michezo yetu kwa upande wetu na sasa kilichobakia ni kujiandaa, kushiriki katika hatua ya nane bora ila nilichokiona mimi hakuna timu hata moja, ambayo itaweza kutoa upinzani na timu za Unguja kwani kiwango chetu kiko chini sana”. Alifahamisha Makamo. Alifahamisha kuwa kiwango kinachoonyeshwa na timu za Pemba ni dhahiri kuwa kwa mfumo

TAIFA YA JANG'OMBE NA ZIMAMOTO MMOJA ATASHUSHWA NA POLISI 4 BORA WA UNGUJA?

Image
Msimamo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja

BAO PEKEE LA RAIS WA BOYS LASAHAULISHA BENDERA YA MASHABIKI WA TAIFA AMAN

Image
Baada ya jana timu ya Taifa ya Jang'ombe kufungwa bao 1-0 na Jang'ombe Boys kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa Amaan,  baadhi ya Mashabiki wa timu hiyo wasahau bendera yao kiwanjani hapo. Bao la dakika ya 86 lililofungwa na Khamis Mussa (Rais) ndilo lililopeleka kilio kwa Taifa na ndilo lililosababisha Bendera hiyo kusahauliwa.  Wachezaji wa JKU ambao hufanya mazoezi katika uwanja wa Aman asubuhi ya leo wameishuhudia bendera hiyo iliyosahauliwa na mashabiki hao katika uwanja huo. "Ni kweli tumeiona Bendera ya Mashabiki wa Taifa asubuhi ya leo iliyosahauliwa jana usiku".Kilieleza chanzo. Taifa ya Jang'ombe na Jang'ombe boys ni mahasimu sana,  jambo ambalo linapelekea kwa timu itakayofungwa baadhi ya mashabiki wao kushindwa hata kula na kufanya mambo mengine.

BOYS KIDUME MBELE YA TAIFA, KWENYE HISTORIA WAONGOZA KUWAFUNGA WENZAO MARA NYINGI

Image
Timu ya Jang’ombe Boys jana imeweka rikodi njema baada ya kuifunga Taifa ya Jang’ombe bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ulisukumwa saa 2 za usiku kwenye uwanja wa Amaan. Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Khamis Mussa (Rais) katika dakika ya 86. Huu ni mchezo wa 6 kukutana katika historia za timu hizi ambapo katika michezo hiyo waliyokutana Taifa alishinda miwili, na Boys kushinda mitatu na mmoja kutoka sare, hivyo mpaka sasa Boys anarikodi nzuri kuliko Taifa. RIKODI USO KWA USO BOYS V/S TAIFA WAMEKUTANA MARA 6 MPAKA SASA Msimu wa mwaka 2012-2013 Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Taifa 1-2 Boys Ligi ya Waamuzi dakika 90 Taifa 0-0 Boys, Penalti Taifa 4-5 Boys. Novemba 19, 2016 Bonanza la Coconut FM Taifa 2-0 Boys Mabao yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess. Disemba 10, 2016 Ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa kwanza Taifa 2-2 Boys Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chand

RAIS WA BOYS AVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE, NA NDIE MCHEZAJI ALIYEMFUNGA MABAO MENGI KIPA SALULA WA TAIFA

Image
Mshambuliaji hatari wa timu ya Soka ya Jang’ombe Boys Khamis Mussa (Rais) amevunja rekodi nyingine akiwa Boys katika Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe. Goli alilofunga jana katika dakika ya 86 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe limemfanya kufikisha mabao matatu katika mchezo wa Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe akicheza katika dimba Amaan, ambapo Boys kwa mara ya kwanza msimu huu wakiifunga Taifa baada ya kushinda 1-0. Rais ameanza safari yake ya kufunga katika Dabi hiyo alipofunga mabao mawili kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016. Rikodi nyengine aloiweka Rais jana amekuwa mchezaji wa kwanza kumfunga mabao mengi zaidi mlinda mlango hatari wa Taifa ya Jang’ombe Ahmed Ali “Salula” baada ya kumfunga mabao matatu kwenye msimu huu. Baada

FULL TIME KUTOKA AMAN JANGOMBE DABI

Image
Full time kutoka Aman, Taifa ya Jang'ombe 0-1Jang'ombe Boys.  Bao limefungwa na Khamis Mussa "Rais" dakika ya 86.

HAYA HAPA MATOKEO YA LIGI KUU ZENJ LEO

Image
Saa 8 mchana,  Kilimani City 2-0 Miembeni,  saa 10 jioni KVZ 4-0 Black Sailors

MASHABIKI WAANZA KUJITOKEZA KWA WINGI KUANGALIA BOYS DHIDI YA TAIFA

Image
Zoezi la kuuza tiketi mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzobar kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Jang'Ombeboys Fc tayari limeshaanza kuanzia saa12:00 jioni. Mechi itaanza saa 2:30 usiku uwanja wa Amaan. Viingilio katika mchezo huo ni: majukwaa ya urusi, orbit na saa itakua 2000, majukwaa ya wings 3000, V.I.P B,C na D itakua 5000 na V.I.P A 10,000.

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

Image
Jina lake ni Khamis Mussa “Rais” ambae hadi leo bado rekodi yake haijavunjwa na mchezaji yoyote kwenye mechi ya Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe. Ni Striker hatari wa Jang’ombe Boys, huyu jamaa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zilipokutana timu hizo. Ameshafunga mabao mawili mpaka sasa na hakuna mwengine yeyote alifika mabao hayo. Rais amefunga mabao hayo katika mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016. Mabao hayo alifunga katika dakika ya 45 na 53 huku akimuweka katika wakati mgumu mlinda mlango hatari wa Taifa ya Jang’ombe Ahmed Ali “Salula”. Wachezaji wengine ambao wanaweza kuivunja rikodi hiyo kwa upande wa timu ya Taifa ni Mkongo Baraka Ushindi, Mkenya Mohd Said “Mess”, Omar Yussuf Chande na Hassan Seif “Banda”  ambao wote wamefunga bao moja tu. RIKODI USO KWA

VIINGILIO VYA MECHI YA TAIFA NA BOYS HIVI HAPA

Image
Chama cha Soka Visiwani Zanzibar "ZFA" kimetangaza viwango vya viingilio vya mchezo wa kesho Jumanne 25/4/2017 Dabi ya Jang'ombe katika mwendelezo wa ligi kuu ya soka Zanzibar kanda ya Unguja kati ya Jang'ombe Boys vs Taifa ya Jang'ombe saa 2:30 usiku uwanja wa Amaan. Viingilio katika mchezo huo ni: Jukwaa ya urusi, orbit na saa itakua 2000, jukwaa la wings 3000, V.I.P "B", "C" na "D" itakua 5000 na V.I.P "A" 10,000.

LIVE KUTOKA UWANJA WA AMAN, ZIMAMOTO V/S POLISI

Image
Kikosi cha Zimamoto Full time kutoka uwanja wa Amaan,  Zimamoto 0-3 Polisi,  mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja. Mabao ya Polisi yamefungwa Suleiman Ali Nuhu dakika 32 na Abdallah Omar Ali dakika ya 45 na Mohd Hassan dakika ya 59.

MUNDU YAKUMBUKA SHUKA WAKATI TAYARI KUMEKUCHA, KESHO HOMA YA JIJI KATI YA TAIFA NA BOYS

Image
Timu ya Mundu kutoka Nungwi Kaskazini ya Unguja leo imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2 walipoichapa Chwaka Stars  kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya kanda ya Unguja mchezo uliopigwa atika uwanja wa Amaan saa 10 za jioni. Mabao ya Mundu yamefungwa na Abas Pele (Hat trik) dakika ya 55, 60,82 na Yahya Shaaban dakika ya 63. Mabao ya Chwaka Stars yamefungwa na Hisan Abdallah dakika ya 11 na Ibrahim Sultan dakika ya 51. Leo saa 1 za usiku Zimamoto dhidi ya Polisi katika Uwanja wa Amaan. Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo mitatu katika uwanja wa Aman. Saa 8 za mchana Miembeni dhidi ya Kilimani City,  saa 10 KVZ dhidi ya Black Sailors,  na usiku homa ya jiji kati ya Taifa ya Jang'ombe na ndugu zao Jang'ombe Boys.

AFRICAN MAGIC YAWATESA KVZ, KOMBE LA MUUNGANO

Image
Kikosi cha African Magic Mashindano ya Kombe la Muungano 2017 kwa mpira wa Kikapu (Basketball)  yameendelea tena saa 2 asubuhi ya leo Jumatatu katika Uwanja wa Gmkhana ambapo timu ya African Magic ya Wanawake ikafanikiwa kuwafunga Maafande wa KVZ kwa vikapu 72-31. Mchezo mwengine umepigwa majira ya saa 4 za asubuhi katika Uwanja huo ambapo walicheza Wanaume timu ya Stone Town dhidi ya Nyuki ambapo Wana Jeshi wa Nyuki wakafanikiwa kushinda kwa vikapu 79-59. Mechi nyengine za leo zote ni kwa upande wa Wanaume ambapo mchezo unaoendelea sasaivi saa 6 za mchana ni kati ya Polisi dhidi ya JKT, na saa 8 za mchana watakipiga timu ya Mbuyuni dhidi ya Tanado, saa 10 za jioni African Magic dhidi ya Stone Town. Kombe hilo litaendelea tena kesho Jumanne ya April 24, kwa kupigwa mchezo mmoja tu saa 2 za asubuhi kwa Wanaume wa Tonado kutokea Tanzania bara dhidi ya Chake ya Pemba ambapo watasukumana katika Uwanja wa Gmkhana.

TAIFA V/S BOYS ZIJUWE RIKODI ZAO WALIVYOKUTANA

Image
Mchezo wa Dabi ya Jang’ombe wa ligi kuu soka ya Zanzibar kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys utasukumwa kesho Jumanne saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan. Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe Lakini Taifa katika Msimu huu wa mwaka 2016-2017 ameweka rikodi nzuri kwani mpaka sasa kwenye msimu huu wamekutana mara tatu na mbili Taifa kushinda na moja sare. Huu ni mchezo wa 6 kukutana katika historia za timu hizi ambapo katika michezo mitano waliyokutana Taifa alishinda miwili, na Boys kushinda miwili na mmoja kutoka sare, hivyo mpaka sasa hakuna mbabe wapo sawa na mchezo wa kesho ndio utatoa mwanya mzuri kwa timu itakayoshinda itakuwa imeweka rikodi nzuri zaidi ya mwenziwe. Kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016. Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya Boys yo

AZAM SPORTS FEDERATION CUP – NUSU FAINALI: AZAM-SIMBA, MBAO-YANGA

DROO ya Mechi za Nusu Fainali za Azam Sports Federation Cup imefanyika Leo na Mabingwa Watetezi Yanga kupangwa kucheza na Mbao FC huko CCM Kirumba, Mwanza. Nusu Fainali nyingi ni kati ya Azam FC na Simba na Mechi hii itachezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam hapo 29. Mbao FC na Yanga zitachezwa Aprili 30.

HAJI MANARA JELA MWAKA 1, FAINI SH MIL 9

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amehukumiwa Kifungo cha Mwaka Mmoja kutojihusisha na masuala ya Soka na pia kutakiwa kulipa Faini ya Shilingi Milioni 9. Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya Manara kupatikana na Makosa Matatu yaliyoainishwa kwamba ni kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia utendaji wa Shirikisho hilo.

POINTI ZA SIMBA DHIDI YA KAGERA WAREJESHEWA WENYEWE KAGERA

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuip okonya Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar. Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera katika Ligi Kuu ya Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 72. Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na n d ipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo. Akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zimechangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo ali z itaja kuwa ni: “Malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa

LIGI KUU ZENJ BADO INAWAKA MOTO MKALI, KMKM HOI KWA MAOSTADHI WA CHUONI

Image
Wachezaji wa KMKM Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili tofauti ambapo saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa Amaan  mabaharia wa KMKM wakakubali kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Maostadhi wa Chuoni. Mchezo mwengine umepigwa saa 10 za jioni kiwanjani hapo baada ya Mafunzo kuichapa Kijichi 2-0. Lakini kwa upande wa kanda ya Pemba leo Chipukizi ilitoka na ushindi mabao 5-1 dhidi ya Aljazeera huku Shaba wakiichapa New Star bao 1-0. Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika Uwanja wa Amaan. Saa 10:00 za jioni Mundu FC v/s Chwaka Stars, na saa 1:00 usiku ni zamu ya Polisi v/s Zimamoto. Mzunguko wa 32 utamalizika Jumanne 25-04-17        Miembeni SC v/s Kilimani City FC      Amani saa 8:00 mchana, na saa 10:00 za jioni KVZ v/s Black Sailors na saa 1:00 Usiku Derby ya Jangombe kati ya Jang’ombe Boys FC v/s Taifa ya Jang’ombe.

IKRAM OMAR MJUMBE MPYA ZFA KWA MARA YA KWANZA KUINGIA KATIKA MKUTANO MKUU

Image
Ikram Omar Mjumbe mpya wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Kati Mjumbe mpya wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Kati Ikram Omar ambae pia ni Mtangazaji wa Michezo kupitia kipindi cha Coco Sports ya Coconut FM leo kwa mara ya kwanza ametinga katika Mkutano Mkuu wa ZFA uliofanyika Gombani Kisiwani Pemba. Hivi karibuni Ikram amefanikiwa kushinda katika Uchaguzi mdogo wa ZFA Wilaya ya Kati kwa nafasi ya Mjumbe kwenda Taifa baada ya kumuangusha mpinzani wake Salum Hassan. Kwasasa ndani ya ZFA kuna Waandishi wa Habari wawili akiwemo Ikram na Ali Bakar “Cheupe” ambae ni Afisa Habari wa chama hicho.