SINA TAARIFA ZOZOTE ZA KUFUNGIWA MAISHA NISIJIHUSISHE NA SOKA, KAMA WAMEFANYA HIVYO ZFA, HUO NI UHUNI-HUSSEIN

InakaribiaWiki moja sasa tangu kufungiwa kwa wajumbe wawili wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Mjini Hussein Ali Ahmada na Masoud Attai kutoka Wilaya ya Kazkazini “A” ambao wote kwa pamoja wametimuliwa ndani ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” na kusimamishwa maisha kutojihusisha na shughuli za soka, leo yameibuka mapya kutoka kwa Hussein ambae amesema hana taarifa rasmi za kufukuzwa kwake na yeye anajua bado ni Mjumbe wa ZFA Taifa kutoka ZFA Wilaya ya Mjini.

Amesema amesikia kwenye vyombo vya habari tu kama amefungiwa lakini hajapewa uthibitisho wowote na ZFA na kama wamefanya hivyo ZFA kitendo hicho ni uhuni tu.

“Mimi nimesikia tu kwenu Waandishi, lakini sijapewa taarifa rasmi mpaka leo, hivyo mimi taarifa hizo sijazielewa, kwasababu ukifungiwa upewe barua maalum na ujuwe sababu gani zilizopelekea mimi kufungiwa, kama mimi nimesimamishwa si tatizo lakini nipewee taarifa rasmi na wafate taratibu, mana sielewi hata katiba gani ambayo wametumia kunisimamisha kama munavyosema, lakini mimi niseme ZFA wanafanya maamuzi kipuuzi”. Alimalizia Hussein.

Jumamosi iliyopita ya April 22, 2017 Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA uliofanyika Gombani Kisiwani Pemba uliwafukuza wajumbe wake wawili Hussen Ali Ahmada na Massoud Attai na kuwafungia maisha kutojihusisha na Soka kutokana na sababu tofauti moja wapo ikiileza kuwa viongozi hao walifanya vitendo vya ubadhirifu wa mali wakati walipoongoza ZFA kwa muda baada ya chama hicho kupelekwa Mahakamani.
Hussein Ali Ahmada

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS