Posts

Showing posts from February, 2018

DIAMOND AANZA KUSAKA WATANGAZAJI WA WASAFI RADIO NA TV, WAZIRI WA MICHEZO ZANZIBAR AWAOMBA WAZANZIBAR WAJITOKEZE KWA WINGI NGOME KONGWE KESHO

Image
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amewataka watangazaji pamoja na watu wenye vipaji hivyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi maalum la kutafuta vipaji hivyo zoezi ambalo litafanyika kesho Jumanne kuanzia saa 3 asubuhi hadi jioni katika ukumbi wa Ngome Kongwe. Waziri Rashid ameyasema hayo Afisini kwake Kikwajuni wakati akimkabidhi msanii Nasib Abdul maarufu Diamond hati ya leseni ya kufungua vituo vya wasafi Radio na TV. Kwa upande wake Diamond amesema ameamua kufika Zanzibar kutafuta vipaji hivyo kwani anajua Zanzibar kuna vipaji vingi huku akiwataka Wazanzibar wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo ili wapate fursa ya ajira.

ZANZIBAR HEROES MAPEMA KUTANGAZWA NA KUANZA MAANDALIZI

Image
Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo imesema itahakikisha Chama cha soka Zanzibar (ZFA) inasimamia kufanya maandalizi ya timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) mapema mwaka huu ili izidi kutoa upinzani mkali katika mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup. Akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Konde Omar Seif Abeid aliyetaka kujua wizara ina mpango gani kabambe uliondaliwa kuhakikisha Zanzibar Heroes inaendelea kutoa upinzani katika mashindano hayo, naibu waziri wa wizara hiyo Chum Kombo Khamis amesema wizara kwa kushirikiana na idara ya michezo itahakikisha kuwa ZFA inasimamia kufanyika maandalizi ya timu hiyo mapema ili kuleta ushindani katika mashindano hayo. Zanzibar Heroes ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup mwaka jana baada ya kufungwa kwa penalty 3-2 na wenyeji Kenya kufuatia kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.

BALOZI SEIF AHIMIZA MAZOEZI

Image
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Jamii inapaswa kuzingatia ulazima wa kufanya mazoezi ya Viungo kila mara ili iweze kujenga afya njema na hatimae kupunguza gharama za matibabu kwa magonjwa yanayoweza kutibika. Alisema kulingana na mabadiliko ya mifumo ya Afya na Ulaji wa vyakula vya kutengeneza visivyozingatia utaratibu wa Kitaalamu Duniani kote mazoezi yanalazimika kupewa kipaumbele kikubwa katika kuimarisha Afya za Wanaadamu. Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo mapema asubuhi wakati wa Bonaza la Vikundi vya Mazoezi   Nchini lililoandaliwa na kikundi cha New Life Exercise Club na kile cha Kiembe Samaki Fitness Club na kufanyika katika Uwanja wa Amaan Mjini zanzibar. Alisema mazoezi ni sehemu pia   inayowafanya Watu kuondokana na mihemko na kuachana na mawazo ya kufanya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia. Hivyo ametoa wito kwa wanamichezo hao kuwa Mabalozi wa Kampeni ya kuwahimiza watu wafanye mazoezi, kupinga udhalilishaji, kuch

ZANZIBAR HEROES WAKABIDHIWA VIWANJA VYA PLAN HUKO TUNGUU

Image
Wachezaji na Viongozi 33 wa Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) wamekabidhiwa hati zao za viwanja walivyoahidiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein aliyoitoa Disemba 23, 2017. Wakikabidhiwa Viwanja hivyo eneo la Tunguu Plan na Waziri wa ardhi, maji, nishati na mazingira Salama Aboud Talib amewataka kuvienzi na kuvitunza kama walivyoagizwa na Dkt Shein kuwa wasiviuze bali wavitumie katika kujenga maisha yao. Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini Michezo ndio maana ikawazawadia viwanja pamoja na zawadi mbali mbali. Nae waziri wa habari utalii utamaduni na michezo Rashid Ali Juma amesema leo ni siku ya historia kwa mashujaa hao baada ya kukabidhiwa rasmi viwanja vyao walivyoahidiwa na rais wa zanzibar na kuwahimiza kuendelea kujituma kwani michezo ni ajira. Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman (Morocco) amemshukuru Dkt Shein kwa ahadi yake kutimizwa leo huku wakiwa nafura kubwa sana kwa

JKU APIGWA 7-0 KOMBE LA KLABU BINGWA HUKU ZIMAMOTO AKIFA KIUME KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika JKU na Zimamoto zote zimetolewa rasmi leo katika Mashindano hayo baada ya kufungwa ugenini katika michezo yake ya marejeano. Katika kombe la Klabu Bingwa JKU wamefungwa na Wenyeji Zesco ya Zambia mabao 7-0 na kufanya kutelewa kwa jumla ya mabao 7-0 kufuatia mchezo wa awali uliochezwa Amaan Zanzibar kumalizika kwa sare ya 0-0. Mabao ya Zesco manne yamefungwa   na Zikiru Adams dakika 4, 42, 57, 60 huku mengine yakifungwa na Lazarus Kambole dakika 36, Winston Kalengo dakika 77 na Lameck Banda dakika ya 87. Kwa upande wa Zimamoto ambao walikuwa wanawakilisha Zanzibar katika Kombe la Shirikisho nao wametolewa kwa kufungwa 1-0 na wenyeji wao Wallaita Dicha ya Ethiopia na kufanya watolewe kwa jumla ya mabao 2-1. Bao pekee la Wallaita Dicha limefungwa na Arafat Djako dakika ya 29. Huu ni mfululizo wa kufanya vibaya kwa vilabu vya Zanzibar katika Mashindano hayo kufuatia msimu u

MSIMAMO WA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Image

JKU WABANWA MBAVU NYUMBANI KWAO NA ZESCO YA ZAMBIA

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya JKU imelazimishwa sare ya 0-0 nyumbani kwao kwenye uwanja wa Amaan dhidi ya Zesco United kutoka Zambia. Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na mashambulizi yakushutukizia dakika tisini za muamuzi JeanClaude Ishimwe kutoka Rwanda hakuna timu iliyoona lango la mweziwe zaidi ya kosa kosa nyingi kwa kila timu. Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya JKU Ali Suleiman Mtuli amesema mchezo ulikuwa nzuri na wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao utakaochezwa huko Zambia. Nae Haji Juma (Chafu) mlinda mlango wa JKU amefanikiwa kuwa nyota wa mchezo huo na amesema wataendelea kupigana ili waiwakilishe vyema Zanzibar katika Mashindano hayo. Nae kocha wa timu ya ZESCO United Tenant Chembo amesema ameyapokea matokeo hayo huku wakijipanga kwa mchezo wao wa marejeano nyumbani kwao. Wawakilishi wengine wa Zanzibar timu ya Zimamoto watarajiwa kujitupa dimbani kesho mnamo majira ya saa

ZESCO WAFANYA MAZOEZI KWA SIRI, WATU WOTE WAMEZUILIWA KUINGIA UWANJA WA AMAAN

Image
Timu ya Zesco United kutoka Zambia imezuia mashabiki kuingia uwanja wa Amaan, kuangalia mazoezi ya klabu hiyo baada ya kuamua kufanya mazoezi siri kuelekea mchezo wao kesho kutwa (Jumamosi) dhidi ya wenyeji wao JKU katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika. Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar walijitokeza kwa wingi nje ya uwanja wa Amaan wakisubiri timu ya ZESCO ifike uwanjani ili waangalie mazoezi yao, lakini hali ilikuwa tofauti baada ya wachezaji kuingia ndani ya uwanja huo na Mageti yote yakafungwa na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia. Kabla ya dakika 15 kumaliza mazoezi wakawaruhusu waandishi wa Habari tu pekee yao kwaajili ya kufanya mahojiano na kupiga picha. Hii ni kawaida hasa katika Mashindano kama haya kwa timu kuzuia mashabiki kwani huwa na wasi wasi kuibiwa baadhi ya mbinu zao pamoja na kujulikanwa kwa haraka wachezaji wao nyota ambao wanaimani waje kuwafunga wenyeji wao. “ Haturuhusu kuingia uwanjani nyinyi muje Jumamosi kuangalia mechi tu

WA ETHIOPIA WATAKAOCHEZA NA ZIMAMOTO WAWASILI ZENJ

Image
Wapinzani wa Zimamoto kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika  Walaitta Dicha ya Ethiopia imewasili Zanzibar mchana wa leo ikijiandaa na mchezo wao siku ya Jumapili majira ya saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

ZESCO UNITED YAWASILI ZANZIBAR, TAYARI KUWAVAA JKU JUMAMOSI

Image
Wapinzani wa JKU katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya Zesco United kutoka Zambia wamewasili leo Zanzibar tayari kabisa kwa mchezo wa Jumamosi kwenye uwanja wa Amaan. Timu hiyo imewasili leo saa nne asubuhi kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ambapo wachezaji wa timu hiyo wameongozana na viongozi wao na wamepokelewa na wenyeji wao ambao ni viongozi wa timu ya JKU. Afisa habari wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) Ali Bakar (Cheupe) amesema kwa upande wao Chama maandalizi yote wamekamilisha huku akiwataka Mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kwenda kuzishangiria timu za Zanzibar. Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano hayo ya Kimataifa ni JKU ambao wataivaa Zesco United siku ya Jumamosi katika mchezo wa kombe la Klabu bingwa huku Zimamoto ambao watawakilisha kwenye kombe la Shirikisho wataivaa Walaitta Dicha ya Ethiopia siku ya Jumapili michezo yote itapigwa majira ya saa 10:00 za jioni katika uwanja wa

MSIMAMO WA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Image

MASHINDANO YA HALF MARATHON YAFANA ZANZIBAR

Image
Mashindano ya Zanzibar Half Marathon yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijana, kuviendeleza na kuwandaa vijana hao katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yamefanyika hii leo Foradhan Mjini Unguja huku washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi mbali mbali walishiriki Mashindano hayo kwa kilomita 5, 10 na 21. Akizungumzia Mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdul Hakim Cosmas Chasama amesema Mashindano hayo yamewapa mazoezi mazuri wanaridha ambao watashiriki Mashindano mbali mbali makubwa yakiwemo ya ndani na nje ya Tanzania. Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Wanaume amefanikiwa kuwa Dickson Marwa kutoka Tanzania Bara huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mohammed Ramadhan Mgeni kutoka Zanzibar huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Remigius John kutoka Tanzania bara. Kwa upande wa Wanawake Kilomita 21 Mshindi ni Angel John Juma kutoka Tanzania bara huku nafasi ya pili ikikamatwa na Asma Rajab kutoka Zanzibar wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mia Vej

ZTTA CHAKUTANA NA WADAU WAKE

Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar (ZTTA), leo kimekutana na viongozi wa vilabu vya Unguja kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ya maendeleo ya mchezo huo Visiwani Zanzibar, kikao ambacho kimefanyika saa 3 asubuhi katika ukumbi wa skuli ya Hailesalas

NAGE (REDE) ZANZIBAR WAENDA DAR ES SALAM KUWAFUNDISHA WENZAO MCHEZO HUO

Wachezaji wa mchezo wa Nage Zanzibar wametakiwa kuukuza mchezo huo Tanzania bara ili kuiletea sifa Zanzibar katika Michezo. Akizungumza wakati wa kuziaga timu nne za mchezo wa Nage Zanzibar Talib Ali Talib ambae ni mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa mjini, amesema lengo la kwenda Tanzania bara ni kuukuza mchezo huo pia kuzidisha uhusiano wao na Tanzania bara katika kusheherekea miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM. Timu nne za Nage zilizokwenda Jijini Dar es salam ni Miembeni Magic kutoka jimbo la Kikwajuni, karakana kutoka jimbo la Chumbuni, Six center kutoka Jimbo la Mwera na  yataka moyo kutoka jimbo la Welezo. Kwa matokeo ya leo huko Dar es salam timu za Zanzibar zote zimeanza vyema ambapo Miembeni chupa 63-3 Magomeni ya Dar, Karakana City 45-15 Kinondoni ya Dar, Yataka moyo ya Welezo Zanzibar 17-8 Kijitonyama ya Dar.