MASHINDANO YA HALF MARATHON YAFANA ZANZIBAR


Mashindano ya Zanzibar Half Marathon yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijana, kuviendeleza na kuwandaa vijana hao katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yamefanyika hii leo Foradhan Mjini Unguja huku washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi mbali mbali walishiriki Mashindano hayo kwa kilomita 5, 10 na 21.

Akizungumzia Mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdul Hakim Cosmas Chasama amesema Mashindano hayo yamewapa mazoezi mazuri wanaridha ambao watashiriki Mashindano mbali mbali makubwa yakiwemo ya ndani na nje ya Tanzania.
Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Wanaume amefanikiwa kuwa Dickson Marwa kutoka Tanzania Bara huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mohammed Ramadhan Mgeni kutoka Zanzibar huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Remigius John kutoka Tanzania bara.
Kwa upande wa Wanawake Kilomita 21 Mshindi ni Angel John Juma kutoka Tanzania bara huku nafasi ya pili ikikamatwa na Asma Rajab kutoka Zanzibar wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mia Vejlgaard Just kutoka Denmark.
Na katika kilomita 10 Wanaume mshindi ni Abdallah Jecha Abdallah kutoka Zanzibar, mshindi wa pili ni Filipo Jacob Mambo kutoka Tanzania bara huku Said Khamis Ali kutoka Zanzibar akishinda nafasi ya tatu.
Kwa upande wa Wanawake kilomita 10 washindi ni Rosemery Gustaph Malki kutoka Zanzibar huku nafsi ya pili ikikamatwa na Warda Shaaban Mbura kutoka Zanzibar na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Maria Michael Benedictor kutoka Tanzania bara.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS