Posts

Showing posts from December, 2017

JKU YAFUFUA MATUMAINI KWENYE KOMBE LA MAPIUNDUZI, MABINGWA WATETEZI AZAM NAO KUANZA KIBARUA KESHO

Image
Klabu ya JKU leo imepata alama tatu muhimu kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Zimamoto bao 1-0 katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan. Bao pekee la JKU limefungwa na Salum Mussa Bajaka dakika ya 1 ya mchezo huo. Badae saa 2:15 usiku kuna mchezo mwengine kati ya Mlandege dhidi ya Taifa ya Jang’ombe kwenye uwanja wa Amaan. Mashindano hayo yataendelea tena kesho Jumapili kwa kupigwa michezo miwili ya kundi A katika uwanja wa Amaan. Saa 10:00 Mabingwa watetezi Azam Fc watacheza na Mwenge na saa 2:15 Jamhuri  watakipiga  na URA ya Uganda.

YAJUWE MATUKIO 10 MAKUBWA YA MICHEZO ZANZIBAR YALIOTOKEA 2017, YALOANDALIWA NA MWANA MICHEZO ABUBAKAR KHATIB KISANDU

Image
1.YANGA KUCHAPWA 4-0 NA AZAM,  AZAM KUTWAA MAPINDUZI CUP MBELE YA SIMBA (a) January 7,2017 katika uwanja wa  Amaan Zanzibar , Yanga walipata kipigo ambacho hawatokisahau mbele ya Azam Fc kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa 4-0 na kupelekea kuwa kipigo cha pili kikubwa kwa  Yanga  kufungwa toka May 6 2012 alipofungwa goli 5-0 na  Simba  katika uwanja wa  Taifa Dar es Salaam . Magoli ya  Azam FC  siku hiyo yalifungwa na nahodha wao  wakati huo John Bocco  , Yahaya Mohamed    Joseph Mahundi   na  Enock Atta . (b) January 13, 2017 timu ya Soka ya Azam Fc ilitwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2017 baada ya kuifunga Simba bao 1-0 kwa bao lililofungwa na kiungo mkabaji Himid Mao Mkami dakika ya 13 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan. 2.ZIMAMOTO NA KVZ KUCHEZA CAF NA KUTOLEWA HATUA YA AWALI Februari 19, 2017 wawakilishi wa Zanzibar na kwenye kombe la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika timu ya Zimamoto na KVZ zilitolewa katika hatua ya awali kweny

ZANZIBAR HEROES YABANWA NA KOMBAIN YA PEMBA, SASA WAPO KWENYE TAARABU KULA BATA

Image
NA JUMA MUSSA – ZBC PEMBA Washindi wa pili wa michuano ya CECAFA CHALLENGE CUP 2017 timu ya Zanzibar Heroes imewasili kisiwani Pemba kwa ajili ya kukamilisha sherehe yao na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pemba Kombaini ikiwa ni miongoni mwa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi mh dokta Ali Moh’d Shein ya kukipeleka kikosi hicho kisiwani Pemba kutoa burudani kwa wakaazi wa huko. Kwenye mapokezi hayo yaliyoongozwa na Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo mh Choum Khamis Kombo na wapenda michezo ,  Waziri huyo amewataka wananchi kuwapa hamasa wachezaji hao ili kuweza kufanya vyema katika michezo mingine itakayoshiriki. Ikicheza mbele ya mashabiki walijitokeza kuisapoti timu hiyo katika uwanja wa Gombani Zanzibar Heroes ilishuhudiwa wakishidwa kuwaumiza mashabiki wa Pemba Kombaini baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana. Hata hivyo the Heroes itabidi kujilaumu wenyewe baada ya kukosa mabao mengi kwa kushindwa kuzitumia vyema nafasi w

MWENGE NA MLANDEGE ZAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, BADAE TAIFA NA ZIMAMOTO

Image
Timu ya Mwenge na Mlandege zimeanza vyema Mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwenye michezo iliopigwa leo kwenye uwanja wa Amaan. Mlandege waliwachapa JKU mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa saa 8 za mchana ambapo mabao ya Mlandege yamefungwa na Khamis Abuu dakika ya 18 na Abubakar Ame (Luiz) dakika ya 60 huku bao pekee la JKU limefungwa na Khamis Abdallah katika dakika ya 34. Nao Mwenge wamefanikiwa kuwachapa bao 1-0 timu ya Jamhuri kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo huku bao pekee la Mwenge likifungwa na Ali Salim Bajaka dakika ya 31 ya mchezo. Badae saa 2:15 usiku utapigwa mchezo mwengine kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Zimamoto kwenye uwanja wa Amaan. Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan. Saa 10:00 za jioni Zimamoto  watakuwa na kazi ngumu kucheza JKU na Saa 2:15 Taifa ya Jan’gombe watakipiga na Mlandege.

ZANZIBAR HEROES HAO KISIWANI PEMBA KUFUNGA MWAKA 2017 KWA FURAHA

Image
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kesho saa 1 asubuhi watasafiri kwa Boti kwenda Kisiwani Pemba na huko watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Pemba. Mechi hiyo itachezwa kesho kutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba. Safari hiyo ya kwenda Pemba ilipendekezwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwenye tafrija maalum iliyoendana na Taarab ya kikundi cha Taifa cha Zanzibar ambapo siku hiyo pia Rais huyo aliwazawadia Wachezaji na Viongozi Milioni 3 na kiwanja kila mmoja. Zanzibar Heroes imefanikiwa kushika nafasi ya pili ya michuano hiyo ya ‘CECAFA’ baada ya kupata matokeo ya kufungwa magoli 3-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penanti baada ya kwenda sare ya goli 2-2 kwa dakika 120 na timu ya Taifa ya Kenya.

KESHO RASMI MAPINDUZI CUP INAANZA KUPIGWA MICHEZO MITATU

Image
Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake rasmi kesho Ijumaa Disemba 29, 2017 katika uwanja wa Amaan kwa kupigwa michezo mitatu tofauti. Saa 8:00 za mchana wataanza kati ya Mlandege dhidi ya JKU, Saa 10:00 za jioni Jamhuri watacheza na ndugu zao Mwenge na  saa 2:15 usiku Zimamoto watakipiga na Taifa ya Jang'ombe. Jumla ya timu 11 zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwemo sita za Zanzibar, nne kutoka Tanzania bara na moja kutoka Uganda ambapo zimepangwa katika makundi mawili A na B. Katika kundi A, kuna Mabingwa watetezi Azam FC, Simba SC, URA, Mwenge na Jamhuri. Katika michuano hiyo Klabu ya Yanga ambayo ipo katika kundi B, ipo pamoja na timu za Zimamoto, Mlandege, JKU, Taifa ya Jang'ombe na Singida United . Ratiba kamRatiba kamili hii hapa. Dec 29, 2017 Ijumaa saa 8:00 mchana Mlandege vs JKU  Group B, saa 10:00 Jamhuri vs  Mwenge Group A, saa 2:15 Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe Group B Dec. 30, 2017 Jumamosi saa 10:00 Zimamoto  vs J

MAPINDUZI CUP KUANZA RASMI IJUMAA, ZIJUWE TIMU 11 ZITAKAZOSHIRIKI ZIMEPANGWA NA NANI

Image
Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kesho kutwa Ijumaa Disemba 29, 2017 katika uwanja wa Amaan. Siku hiyo itapigwa michezo mitatu ambapo saa 8:00 za mchana wataanza kati ya Mlandege dhidi ya JKU, Saa 10:00 za jioni Jamhuri watacheza na ndugu zao Mwenge na  saa 2:15 usiku Zimamoto watakipiga na Taifa ya Jang'ombe. Jumla ya timu 11 zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwemo sita za Zanzibar, nne kutoka Tanzania bara na moja kutoka Uganda ambapo zimepangwa katika makundi mawili A na B. Katika kundi A, kuna Mabingwa watetezi Azam FC, Simba SC, URA, Mwenge na Jamhuri. Katika michuano hiyo Klabu ya Yanga ambayo ipo katika kundi B, ipo pamoja na timu za Zimamoto, Mlandege, JKU, Taifa ya Jang'ombe na Singida United . Ratiba kamRatiba kamili hii hapa. Dec 29, 2017 Ijumaa saa 8:00 mchana Mlandege vs JKU  Group B, saa 10:00 Jamhuri vs  Mwenge Group A, saa 2:15 Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe Group B Dec. 30, 2017 Jumamosi saa 10:

ZANZIBAR SAND HEROES YAREJEA NYUMBANI NA KOMBE

Image
Mabingwa wa Mashindano ya Copa Dar es salam ya soka la ufukweni , timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Sand Heroes) wamerejea nyumbani Zanzibar na kupokelewa kwa shangwe na Wazanzibar. Sand Heroes wamerejea wakitokea Dar es salam baada ya  jana kubeba ubingwa huo kwa kuwafunga Malawi 3-2 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Fukwe za Coco. Katika mapokezi hayo, yaliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa michezo,akiwemo katibu mkuu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee, viongozi wa ZFA akiwemo Rais Ravia Idarous Faina na wadau wengine wa michezo. Mabingwa hao punde tu walipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja moja kwa moja wakapelekwa katika ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan ambapo huko katibu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee amewapongeza mashujaa hao kwa kuyatekeleza vyema majukumu waliyopewa na kuiwakilisha vyema Zanzibar katika Mashindano hayo. Nae kocha mkuu wa timu hiyo Ali Sharifu (Adolf) amekiri kuwa mashindano yali

ZANZIBAR YATINGA FAINALI MASHINDANO YA BEACH SOKA, YAONGOZA KULIKO NCHI ZOTE WATACHEZA TENA NA MALAWI FAINALI

Image
Timu ya taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni (Zanzibar Sand Heroes) imefanikiwa kutinga fainali katika Mashindano ya Copa Dar es salam yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Jijini Dar es salam baada ya asubuhi ya leo kuwachapa Malawi mabao 5-1. Mchezo mwengine leo Uganda wakaichapa Tanzania bara kwa mabao 6-5. Kwa matokeo hayo Zanzibar imeongoza katika Mashindano hayo wakishika nafasi ya kwanza huku Malawi wamekamata nafasi ya Pili ambapo Tanzania bara wakishika nafasi ya tatu na Uganda wakikamata nafasi ya nne. Hivyo fainali itachezwa na timu ilokamata nafasi ya kwanza (Zanzibar) dhidi ya timu iloshika nafasi ya pili (Malawi) huku mshindi wa tatu watachuana kati ya timu iloshika nafasi ya tatu (Tanzania Bara) na Uganda waliomalizia nafasi ya nne. Michezo hiyo itapigwa jioni ya leo Jumanne katika fukwe za Coco ambapo utaanza kuchezwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kisha kumalizwa fainali.

DOKTA SHEIN AENDELEA KUPONGEZWA NA WADAU WA SOKA

Image
Wapenzi wa Soka nchini Tanzania wanaendelea kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwapa zawadi ya viwanja vya kujenga nyumba pamoja na fedha taslim Shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na kiongozi wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes). Kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii ikiwemo Twiter, Facebook, Whatsup mashabiki hao wa soka wamezidi kumimina pongezi wa Rais huyo kwa kuwapatia vitu ambavyo hawatovisahau Mashujaa hao walioshinda nafasi ya pili  kwenye mashindano ya Cecafa Senior Challenge yaliyofanyika nchini Kenya mwezi huu wa Disemba. Jambo hilo limezuwa mijadala mingi mitaani huku kila mmoja akisifu uzalendo huo ulofanywa na Dk Shein ambapo Wanamichezo hao wengine walitokwa na machozi kwa furaha kubwa waliyopatiwa na Rais wao kwani hawakuamini zawadi nzuri na bora waliyopatiwa. Dk Shein alizitowa zawadi hizo katika tafrija maalum iliyofanyika juzi Jumamosi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani

KOCHA MOHAMMED KING AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Image
Kocha wa zamani wa Baghdad, Azam FC, Jang'ombe Boys, JKU na Miembeni City Mohammed Seif Mzee (King) amefiwa na baba yake mzazi, Seif Mzee aliyefariki leo. Marehemu Mzee Seif aliwahi kuwa Daktari katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pia aliwahi kufanya kazi katika Meli ya Mv Mapinduzi. Marehemu Seif atazikwa kesho Jumanne saa 4:00 za asubuhi nyumbani kwao Chaani Kichungwani. Inna lillahi wa inna ilayhi rajiuwn Kocha Mohammed Seif Mzee (King) aliyefiliwa na babayake mzazi leo

MABINGWA ZU WATUA NYUMBANI NA KUPATA BONGE LA MAPOKEZI

Image
Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania maarufu TUSA, Chuo cha Zanzibar University (ZU) wamerejea nyumbani Zanzibar na kupokelewa kwa shangwe na wanafunzi wenzao pamoja na wapenzi wa soka wa Zanzibar. ZU wamerejea wakitokea Mjini Dodoma siku chache baada ya kubeba ubingwa huo kwa kushinda 4-0 dhidi ya wapinzani wao Chuo cha St John cha Dodoma.

ZANZIBAR HEROES WAANZA KUFURAHISHWA NA DK SHEIN, LEO WAITWA IKULU KESHO WANAPEWA SHAVU JENGINE

Image
RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameendelea kutoa pongezi kwa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ kwa kuirudishia Zanzibar heshima yake na sasa imekuwa inasemwa vizuri kutokana na jinsi timu hiyo ilivyoonesha kiwango safi cha kusakata soka. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar katika chakula maalum cha mchana alichowaandalia wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes pamoja na viongozi wake wote baada ya kufanya vyema katika mashindano ya mwaka huu ya Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ yaliofanyika nchini Kenya. Katika hotuba yake fupi kwenye hafla hiyo, iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali,akiwemo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, viongozi wa ZFA na waalikwa wengine, Dk. Shein alieleza kuwa vijana hao wa ‘Zanzibar Heroes’ pamoja na kocha wao mkuu wa timu hiyo wamefanya kazi nzuri na ya kupongeza hatua ambayo itaendelea kuipa heshima kubwa Zanzibar. A

ZANZIBAR YAONYESHA TENA KUWA KIWANDA CHA SOKA, LEO ZU YATWAA UBINGWA WA TUSA

Timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar University (ZU) imefanikiwa kutwaa kombe kwenye mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania (TUSA CUP) baada ya kuichapa Chuo cha St John cha Dodoma 4-0 mchezo iliopigwa huko Dodoma. Mabao ya ZU yamefungwa na Said Bakar Said (Hat trick) na Mohd Maulid (Jaba).

LARSON WA MAFUNZO APIGA BONGE LA BAO WALIPOICHAPA POLISI

Image
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imeendelea tena jioni ya leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan ambapo timu ya Mafunzo Wazee wa Jela jela wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuichapa Polisi bao 1-0. Bao pekee la Mafunzo limefungwa na Ali Juma (Larson) dakika ya 5 ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Polisi Said. Ligi kuu soka ya Zanzibar kesho itasimama na kupisha ligi daraja la kwanza Taifa Unguja ambapo katika uwanja wa Amaan kesho Villa United watakipiga na Mundu, katika uwanja wa Mwanakombo Kijichi watasukumana na Ngome huku katika uwanja Bungi Stronge Fire watacheza na Mlandege michezo yote itapigwa majira ya saa 10:00 za jioni.

KARIHE ANZA , FEI TOTO SUB KIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES LEO DHIDI YA KENYA FAINALI

Image
Kocha wa Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco” ametangaza kikosi chake kitakachocheza leo kwenye mchezo wa fainali Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP kati ya Zanzibar dhidi ya wenyeji Kenya katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 09:00 za Alaasiri. ZANZIBAR HEROES 1.   Mohammed Abrahman Mohd (Wawesha) 18 2.   Ibrahim Mohd Said (Sangula) 15 3.   Mwinyi Haji Ngwali 16 4.   Abdulla Salum Kheri (Sebo) 13 5.   Issa Haidar Dau (Mwalala) 8 6.   Abdul azizi Makame Hassan (Abui) 21 7.   Seif Abdallah Rashid (Karihe) 12 8.   Mudathir Yahya Abass 4 9.   Ibrahim Hamad Ahmada “Hilika” 17 10.                    Mohd Issa Juma (Banka) 10 11.                    Suleiman Kassim   Suleiman “Seleembe” 7 (Captain) AKIBA 1.   Ahmed Ali Suleiman (Salula) 1 2.   Nassor Mrisho Salim 30 3.   Mohd Othman Mmanga 6 4.   Adeyum Ahmed Seif 20 5.   Ibrahim Abdallah Hamad 2

SIRI KUBWA KWETU KUFANYA VIZURI ZANZIBAR HEROES KWENYE CECAFA NI UMOJA :ABDUL AZIZ

Image
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Abdul aziz Makame (Abui) ameweka hadharani siri kubwa iliyowapelekea kufanya vyema katika Mashindano ya Cecafa   Senior Challenge Cup yanayoendelea nchini Kenya. Makame amesema umoja wao ndio silaha kubwa kwao mpaka wakafanikiwa kutinga fainali katika Mashindano hayo. “Sisi tunapendana sana, yani tuna umoja wa hali ya juu sote wachezaji, viongozi mpaka Mashabiki wetu, tunapokosea tunafahamishana kwa lengo la kutengeneza si kubomoa ndio maana sasa tumefika fainali”. Alisema Makame. Makame alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo (Men of the Match) katika mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Zanzibar na Uganda ambapo Zanzibar ilishinda 2-1 na kesho Jumapili saa 9:00 Alaasiri Zanzibar itacheza fainali na wenyeji Kenya mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.