ZANZIBAR SAND HEROES YAREJEA NYUMBANI NA KOMBE

Mabingwa wa Mashindano ya Copa Dar es salam ya soka la ufukweni , timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Sand Heroes) wamerejea nyumbani Zanzibar na kupokelewa kwa shangwe na Wazanzibar.


Sand Heroes wamerejea wakitokea Dar es salam baada ya  jana kubeba ubingwa huo kwa kuwafunga Malawi 3-2 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Fukwe za Coco.

Katika mapokezi hayo, yaliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa michezo,akiwemo katibu mkuu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee, viongozi wa ZFA akiwemo Rais Ravia Idarous Faina na wadau wengine wa michezo.

Mabingwa hao punde tu walipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja moja kwa moja wakapelekwa katika ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan ambapo huko katibu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee
amewapongeza mashujaa hao kwa kuyatekeleza vyema majukumu waliyopewa na kuiwakilisha vyema Zanzibar katika Mashindano hayo.

Nae kocha mkuu wa timu hiyo Ali Sharifu (Adolf) amekiri kuwa mashindano yalikuwa magumu licha ya wao Zanzibar kutwaa Ubingwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Haji Issa (Kidali) amesema vijana wake walipambana mpaka wakachukua ubingwa kwani walijua kuwa majukumu walopewa na waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma siku waliyokabidhiwa Bendera, ndio ilikuwa silaha yao ilofanya mpaka wakabeba kombe.

Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Sand Heroes) ilifanikiwa kubeba ubingwa huo mbele ya Malawi walioshika nafasi ya pili pamoja na wenyeji Tanzania bara waliyokamata nafasi ya tatu na Uganda waliomalizia wanne.









Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS