Posts

Showing posts from October, 2017

BOYS HOI KWA KILIMANI CITY, SAILORS YAIMALIZA CHARAWE

Image
Timu ya Jang’ombe Boys imeendelea kufanya vibaya katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Kilimani city mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan. Bao pekee la City limefungwa na Baraka Mashango dakika ya 19. Mapema saa 8 za mchana Kiwanjani hapo Black Sailors wakaendelea na ari yao ya ushindi baada ya kuifunga Charawe mabao 2-1. Mabao ya Sailors yamefungwa na Mustafa Hamad “Mboma” dakika ya 43 na Maulid Dhamiri wa Charawe alijifunga mwenyewe dakika ya 59 huku bao pekee la Charawe limefungwa na Boniface Afred dakika ya 45. Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja itaendelea tena Alhamis ya Novemba 2, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan   ambapo Saa 8:00 za mchana Mafunzo watakuwa na kazi kwa Kipanga na saa 10:00 za jioni JKU watakipiga na KVZ. Jang'ombe Boys

TAIFA YA JANG’OMBE MAMBO BADO MECHI NNE HAWAJAONJA LADHA YA USHINDI, KVZ NA MAFUNZO WALA SAHANI MOJA, KESHO KMKM NA ZIMAMOTO

Image
Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ngambo) imeendelea kucheza pasipo kupata ushindi katika michezo yake ya ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo saa 8 za mchana kutoka sare ya 0-0 dhidi ya JKU katika uwanja wa Amaan . Kwa matokeo hayo Taifa imefikisha alama 3 kufuatia kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitatu wakati JKU amejikusanyia alama 10 baada ya kushinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja. Saa 10 za jioni ulipigwa mchezo mwengine katika uwanja wa Amaan kati ya KVZ na Mafunzo mchezo ambao umemalizika kwa sare ya 0-0. KVZ anaongoza ligi hiyo akifuatiwa na JKU baada ya timu zote hizo kuwa na alama 10 katika michezo yao 4 waliyocheza huku Mafunzo baada ya mechi ya leo amefikisha alama 5 kufutia kushinda mmoja, sare 2 na kufungwa mmoja. Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan. Saa 8:00 za mchana wataanza Wana Jeshi timu ya Kipanga kukupiga na Maafa

MIEMBENI CITY MECHI NNE SAWA NA DAKIKA 360 BILA YA GOLI, KESHO TAIFA NA JKU HAPATOSHI

Image
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10 za jioni ambapo Miembeni City wakatoka sare ya 0-0 na Chuoni. Kwa matokeo hayo Chuoni inajikusanyia alama 5 baada ya kushinda mmoja, sare miwili na kufungwa mmoja wakati Miembeni city wana alama moja kufutia kufungwa mitatu na sare mmoja wa leo. City walianza kufungwa na Polisi 1-0, wakachapwa 1-0 na Mafunzo, kisha kupigwa 1-0 na JKU na leo kutoka sare ya 0-0 na Chuoni, hivyo wamecheza dakika 360 pasipo kutingisha nyavu za wapinzani hata mara moja. Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8:00 za mchana Taifa ya Jang’ombe dhidi ya JKU na Saa 10:00 za jioni KVZ na Mafunzo.

SIMBA WAMALIZA KAMBI ZANZIBAR NA KUREJEA NYUMBANI DAR KWA NDEGE LEO ASUBUHI

Image
Kikosi cha Simba kimeondoka Visiwani Zanzibar leo saa 3 za asubuhi kwa Ndege na kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Uhuru. Akizungumza na Mtandao huu wakati waondoka hapa Zanzibar kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema akili yao yote ni kuifunga Yanga kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwataka Mashabiki wa Simba waendelee kuishangiria timu yao. “Kambi ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana naamini tumefikia malengo yetu, hapa tunaondoka na leo jioni Dar tutafanya mazoezi ya mwisho, nawaomba Mashabiki wa Simba wazidi kuishangiria timu yao”. Alisema Manara. Simba walikuwa kambini mjini hapa tangu Jumatatu ya Oktoba 23 na leo Ijumaa Oktoba 27 wamerejea nyumbani Dar es salam kuwavaa Yanga.

LIGI KUU ZENJ KUINGIA MZIGONI TENA KESHO MIEMBENI CITY KUKIPIGA NA CHUON

Image
Chuoni Mzunguko wa nne wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja utaanza kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan kati ya Chuoni dhidi ya Miembeni City majira ya saa 10:00 za jioni. Chuoni inakwenda katika mchezo huo wakiwa na alama 4 wakishika nafasi ya 6 huku Miembeni City wenyewe wakijitupa katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya yakupoteza michezo mitatu mfululizo ya awali na wakikamata nafasi ya 13 katika timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo. Miembeni City IJUMAA 27/10/017 22 MIEMBENI CITY VS CHUONI SAA 10:00 ALS AMAAN J’MOSI 28/10/017 23 TAIFA YA J/MBE VS JKU SAA 8:00 MCH AMAAN J’MOSI 28/10/017 24 KVZ VS MAFUNZO SAA 10:00 ALS AMAAN J’PILI 29/10/017 25 KIPANGA VS POLISI SAA 8:00 MCH AMAAN J’PILI

MAKOCHA WA SOKA MAGHARIBI B WAANZA KUPIGWA MSASA

Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) leo kimefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya awali ( Priminary) kozi ambayo imefanyika katika Ukumbi wa ZFA Wilaya ya Magharibi B Mwanakwerekwe Ijitimai. Akifungua kozi hiyo Makamo wa Urais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali amewapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hiyo na amewataka washiriki kuendelea kujifunza zaidi ili Zanzibar watowe makocha bora. “Nawapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hii nawapongeza sana, tena mukimaliza hii muendeleze tena kusoma mkufunzi bi Nassra ni hodari sana tunampongeza, nimefurahi washiriki wanatoa Wilaya tofauti na wengine mpaka Pemba nimefurahi sana nategemea tutatoa makocha bora”. Alisema Zam. Nae mkufunzi wa kozi hiyo Nassra Juma ambae anatambulika Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) amesema kupitia kozi hiyo yatatokea mabadiliko makubwa na kuibuka makocha wazuri ambao watalisaidia soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. “Kama watakuwa wasikivu katika masomo

HAWA NDIO WANAONGOZA KWA MAGOLI LIGI KUU ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Image
Mzunguko wa nne wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja utaanza Ijumaa Oktoba 27 katika uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni Miembeni City dhidi ya Chuoni . Mpaka sasa jumla ya mabao 41 yamefungwa katika ligi hiyo huku washambuliaji Salum Songoro wa KVZ na Nassor Ali wa Kipanga ndio wanaongoza katika safu ya ufungaji ambapo wameshafunga jumla ya mabao 4 kila mmoja. MABAO 4 Salum Songoro (KVZ) mabao 4 Nassor Ali (Kipanga) mabao 4 MABAO 3 Mudrik Muhibu  (KMKM) mabao 3 Salum Akida (KMKM) mabao 3 MABAO 2 Ali Haji Said “Zege” (JKU) mabao 2 Salum Songoro

BOYS KAMA TAIFA, YABANWA NA CHUONI LEO

Image
Mzunguko wa tatu wa ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja umehitimishwa jioni ya leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan kati ya Jang’ombe Boys na Chuoni ambao wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0. Kwa matokeo hayo Boys amefikisha alama 2 baada ya kucheza michezo mitatu kwa kwenda sare miwili na kufungwa mmoja wakati Chuoni amejikusanyia alama 4 baada ya kushinda mmoja, sare mmoja na kufungwa mmoja. Mzunguko wa nne wa ligi hiyo utaanza Ijumaa Oktoba 27 katika uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni  Miembeni City dhidi ya Chuoni . Jang'ombe Boys

AZIZ SHAWEJI ASIMAMISHWA MECHI 4 KUCHEZA LIGI KUU ZENJ NA KOCHA ABRAHMAN MUSSA NAE APIGWA STOP KUKAA KATIKA BENCHI

Image
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimempa adhabu ya kumsimamisha kucheza mechi nne beki wa Kilimani City, Aziz Shaweji baada kupatikana na hatia ya kukiuka nidhamu ya michezo katika mechi kati ya Kilimani City na Black Sailors iliyopigwa juzi Jumapili saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan. Akizungumzia kadhia hiyo katibu mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema Shaweji alipatikana na kosa wakati timu yake ya Kilimani City ilipofungwa 2-0 na Black Sailors ambapo alimzonga Muamuzi wa kati wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor. Hivyo Shaweji atazikosa mechi kati ya Kilimani City dhidi ya Jang’ombe Boys itakayopigwa Oktoba 30, Kilimani city na Chuoni ya Novemba 6, Kilimani city dhidi ya Charawe ya Novemba 12 na ya mwisho Kilimani city dhidi ya Zimamoto itakayopigwa Novemba 19. Wakati huo huo kocha wa Kilimani City Abrahman Mussa nae amesimamishwa kukaa katika benchi hadi pale atakapopeleka vyeti vyake vya ukocha ZFA. Katibu Tedy amesema wamemsimamisha mpaka wathibitishe chet