MIEMBENI CITY MECHI NNE SAWA NA DAKIKA 360 BILA YA GOLI, KESHO TAIFA NA JKU HAPATOSHI

Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10 za jioni ambapo Miembeni City wakatoka sare ya 0-0 na Chuoni.

Kwa matokeo hayo Chuoni inajikusanyia alama 5 baada ya kushinda mmoja, sare miwili na kufungwa mmoja wakati Miembeni city wana alama moja kufutia kufungwa mitatu na sare mmoja wa leo.

City walianza kufungwa na Polisi 1-0, wakachapwa 1-0 na Mafunzo, kisha kupigwa 1-0 na JKU na leo kutoka sare ya 0-0 na Chuoni, hivyo wamecheza dakika 360 pasipo kutingisha nyavu za wapinzani hata mara moja.


Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8:00 za mchana Taifa ya Jang’ombe dhidi ya JKU na Saa 10:00 za jioni KVZ na Mafunzo.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS