Posts

Showing posts from August, 2017

KOMBE LA MTOANO KWENDA MAPUMZIKO MPAKA JUMANNE, TIMU 4 TAYARI ROBO FAINALI ZIMETINGA

Image
Mashindano ya Kombe la Mtoano yaloandaliwa na chama cha Soka Wilaya ya Mjini yamekwenda mapumziko mpaka Jumanne ya Septemba 5, 2017 huku timu 4 zikiwa tayari zimeshatinga hatua ya robo fainali. Jumanne kutapigwa michezo miwili   kati ya Mwembe makumbi dhidi ya Raska zone city saa 8 za mchana , na saa 10 jioni Kundemba itacheza na El Hilal, michezo yote katika uwanja wa Amaan.  Siku ya Jumatano kutakuwa na shughuli pevu kati ya Polisi na Black Sailors timu zote hizo zinacheza ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo ambao utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan. Mpaka sasa timu 4 tayari zimeshatinga hatua ya robo fainali kufuatia kushinda michezo yao ya awali ambazo ni Polisi Bridge, Negro United, Hawai na Shaba. Mashindano hayo yameshirikisha vilabu vya madaraja tofauti vikiwemo vya ligi kuu soka ya Zanzibar, Daraja la Kwanza Taifa, Daraja la Pili Taifa, Daraja la Pili Wilaya na Daraja la Tatu. Attachments area

BUSHIRI KWENDA KUWASAIDIA MUEMBELADU

Image
Kocha wa zamani wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushiri Mahmoud (Bush) amejitolea kwenda kuisadia timu ya Muembeladu inayoshiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini. Bushiri ambae kwasasa amerejea kwa muda Visiwani Zanzibar kufuatia mwanzoni mwa msimu huu kutoendelea tena kuifundisha Mwadui, sasa ataenda kuisaidia Muembeladu ambao wamemuomba kwenda kuisadia timu hiyo. Akithibitisha kwenda kuwasaidia Muembeladu Bushiri amesema Muembeladu wamemfata kuwasaidia na yeye hakufanya hiyana kakubali kwenda kuwasaidia huku pia akisubiria mipango yake mengine ya kurejea Tanzania bara. "Wamenifuata Uongozi wa Muembeladu nikawasaidie, sasa na mimi nimeona nkawasaidie ila nimeshawaambia kuwa sitokaa kwa muda mrefu wa kuishi Zanzibar kwa vile nina mipango yangu ya kurudi tena Tanzania bara hivyo kama miezi mitatu tu ntakuwepo hapa". Alisema Bushiri. Katikati ya msimu uliopita Bushiri   alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo

TAIFA YA JANGOMBE YAIPIGA NEGRO KWENYE MCHEZO WA KUTEST MITAMBO

Image
Timu ya Taifa ya Jangombe (Wakombozi wa Ngambo) wamefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Negro FC katika tamasha la Negro day mchezo uliopigwa jana usiku katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Taifa yamefungwa na Said Kipara pamoja na Abdallah Mudhihir “Mido”. Aidha katika mchezo huo timu zote zilipata fursa ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ambapo Taifa watashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar wakati Negro watacheza ligi daraja la pili taifa.

MZIRAI APANIA KUPANDA TENA DARAJA TIMU YAKE YA KWEREKWE CITY

Image
Baada ya kufanikiwa kupanda daraja la Pili Taifa msimu ulopita timu ya Kwerekwe City yenye Maskani yake Mwanakwerekwe Ijitimai imepania na msimu huu mpya kuondoka daraja hilo na kupanda daraja jengine. Akizungumza na Mtandao huu katibu wa timu hiyo Mussa Habibu “Mzirai” amesema wamepania kupanda tena daraja kutoka la Pili Taifa hadi la kwanza na kutimiza malengo yao ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2019-2020. Amesema falsafa yao ni umoja upendo na uwajibikaji hivyo haoni sababu ya kutopanda tena daraja kwani timu yake ina uongozi kamili na wachezaji wana ari kubwa sana. “Baada ya kupanda daraja la pili taifa sasa akili yetu tumepania kucheza ligi daraja la kwanza taifa, tuna uongozi imara kama munavyowajua kina Mani Gamera au boss Moo, Bakari Rais, Ochu Gerrard na wengine wote hivyo hatuna sababu ya kupanda tena daraja na kutimiza ndoto zetu za kucheza ligi kuu msimu wa mwaka 2019-2020”. Alisema Mzirai. Timu ya Kwerekwe City ilianzishwa mwaka 2014 ambapo

KOMBE LA MTOANO LIMEENDELEA TENA LEO, JUMATANO IJAYO ZAMU YA KUNDEMBA

Image
Kombe la Mtoano limeendelea tena leo kwa kupigwa michezo 2 katika uwanja wa Amaan saa 8 za mchana na saa 10 za jioni ambapo timu ya Negro United na Polisi Bridge zimesonga mbele kwa kushinda michezo yao. Polisi Bridge ilicheza na New King saa 10 za jioni na kushinda kwa penalti5-4 wakati Negro United ikaifunga Gereji kwa Penaliti 5-3 katika mchezo wao uliochezwa saa 8 mchana. ligi hiyo itaendelea tena Septemba 5, 2017 kati ya Mwembe makumbi dhidi ya Raska zone city saa 8 za mchana , na saa 10 jioni Kundemba itacheza na El Hilal, michezo yote katika uwanja wa Amaan. 

KOMBE LA MTOANO KUANZA RASMI LEO, TIMU 16 ZITASHIRIKI MADARAJA TOFAUTI

Image
MICHUANO ya ligi ya Mtoano inatarajiwa kuanza rasmi leo Jumatatu kwa kupigwa michezo miwili itakayochezwa saa 8:00 za mchana na saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan. Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na ZFA wilaya ya mjini inashirikisha timu 16 za madaraja tofauti. Afisa Habari wa chama hicho Mwajuma Juma amesema timu 16 zitashiriki ligi hiyo na mchezo wa kwanza utachezwa saa 8:00 mchana kati ya Hawai na Urafiki. Aidha alisema kuwa mchezo mwengine utachezwa saa 10:00 ambao utawakutanisha timu ya Shaba kutoka kisiwani Pemba dhidi ya African Coast. Alisema kuwa chama chao kimekuwa na kawaida ya kuandaa mashindano hayo kila mwaka kwa madhumuni ya kuzipa mazoezi timu ya kujiandaa na ligi ambapo msimu uliopita Bingwa wa Mashindano hayo timu ya Taifa ya Jang’ombe ambae msimu huu hakushiriki. Aidha alizitaja timu nyengine zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Negro United, Gereji, New King, Polisi Bridge, Mwembemakumbi, Raska Zone City, Kundemba, Elhilal, Black Sailors

MPIRA WA KIKAPU WILAYA YA MJINI WAANDAA MASHINDANO MAKUBWA YALODHAMINIWA NA KAMPUNI KUTOKA MAREKANI

Image
Chama cha Basketball Wilaya ya Mjini (UBA) kinatarajia kuanzisha mashindano ya Mpira wa Kikapu kwa Wanaume yananayotarajia kuanza rasmi Septemba 9, 2017 katika viwanja vya Gymkhana Mjini Unguja na katika ufunguzi huo siku hiyo kutapigwa mchezo kati ya timu ya POLISI dhidi ya MBUYUNI. Katibu wa Basketball wilaya ya mjini Saidi Ali Mansabu amesema mashindano hayo wamepata wadhamini kutoka kiwanda cha kutengeneza Jezi cha UTA ambacho kipo Marekani. “Mashindano yetu tunatarajia kuanza Septemba 9, 2017 ambapo tumepata wadhamini kampuni moja ya kutengeneza Jezi inaitwa UTA ipo Marekani, wametudhamini Jezi na mahitaji mengine katika Mashindano haya, nawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kwasababu haya ni mashindano makubwa sana kwa vile wadhamini ni wenye mpira huu”. Alisema Mansabu. Jumla ya timu 14 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo ambayo yataanzia kwa hatua ya makundi kwa kupangwa makundi mawili, kundi A na kundi B ambapo timu nne za juu kwa kila kundi zitatinga hatua ya

NEGRO DAY KESHO, WATAKIPIGA NA TAIFA YA JANG’OMBE AMAN USIKU

Image
Tamasha la Negro Day litafanyika kesho Jumanne Agost 29, 2017 ambapo timu ya Negro FC itacheza mchezo maalum wa kirafiki na Timu ya Taifa ya Jang’ombe mchezo ambao utasukumwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan. Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa Negro FC Hussein Ahmada amesema katika Tamasha hilo wao Negro watalitumia pia kwaaajili ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya ambao wamesajiliwa kwaajili ya msimu mpya wa mwaka 2017-2018. Amesema pia watatangaza Benchi jipya la ufundi wakiwemo kocha mkuu na msaidizi wake pamoja na kumtangaza mfadhili wao mpya ambae ni mkorea. Aidha Ahmada amesema watazitambulisha jezi zao mpya na pia kutakuwa na burudani mbali mbali katika Tamasha hilo ambalo litaadhimishwa kila mwaka siku ya Agost 29. “Negro day ni siku maalum kwetu kwa kila mwaka ikifika Agost 29 tutafanya tamasha maalum, tutawatangaza wachezaji wetu wapya, benchi la ufundi pamoja na mfadhili wetu tutamtangaza na mambo mengine mengi tu”. Alisema Ahmada. Negro FC in

MZEE MARUNGU AFARIKI DUNIA, NI PIGO JENGINE KWA ZFA NA WAPENZI WA SOKA

Image
Muamuzi mstaafu wa Kimataifa Ahmed Mohd Awadh (Mzee Marungu) amefariki dunia leo Jumanne Agost 22, 2017 ambapo Maziko yatafanyika nyumbani kwake Shangani na kuzikwa leo saa 10 jioni Mwanakwerekwe. Mbali ya kuwahi kuwa muamuzi wa kimataifa pia marehemu alikuwa Kamisaa wa ligi za Zanzibar. Juzi wapenzi wa soka Visiwani Zanzibar walipata pigo jengine kufutia kuondokewa na Dokta wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes” Dokta Abdallah Said Mohammed “ Dokta Kuku” aliyefariki dunia Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar na kuzikwa jana Agost 21, 2017 kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema Peponi Amiin. Kwa taarifa Zaidi endelea kusoma Blog hii.   Marehemu Marungu wa kwanza kushoto waliosimama

BABAAKE MWINYI: UJIO WA GADIEL HAUNIPI HOMA YA KUKOSA NAMBA MWANANGU KIKOSI CHA KWANZA YANGA, BALI NDIO UTAKAMFANYA MWINYI APIGE KAZI ZAIDI

Image
Baba mzazi na meneja wa Mwinyi Haji Ngwali mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga Mzee Haji Ngwali amesema hana mashaka na mtoto wake ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza kwa timu ya Yanga licha ya kusajiliwa mlinzi mwengine wa kushoto Gadiel Michael aliyejiunga akitokea Azam FC. Mwinyi ambae ni msimu wake wa tatu tangu ajiunge na Yanga amekuwa na wakati mzuri tangu asajiliwe na timu hiyo ambapo amecheza michezo mingi kuliko mpinzani wake wakati huo Oscar Joshua ambapo kwasasa anampinzani mwengine Gadiel Michael aliyetoka Azam FC baada ya Joshua kuachwa.   Mzee Haji Ngwali Mzee Haji amesema anaamini mazoezi ndio kila kitu na mpira ni mchezo wa hadharani si mchezo wa kusifiwa katika Magazeti hivyo muhimu kocha wao ndie anaejua nani atamrizisha na kupelekea kumpanga. Amesema anajua Mwinyi ametoka Zanzibar kwaajili ya soka tu hivyo anaamini mwanawe atafanya vizuri kama ataendelea kujituma mazoezini na kuendeleza kuwa na nidhamu ya hali ya juu. “Mimi ndie baba mzaz

PRISONS YAMALIZA KAMBI VISIWANI ZANZIBAR KWA KUSHINDA MICHEZO 4 NA SARE 1 DHIDI YA BLACK SAILORS

Image
Timu ya Tanzania Prisons ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar imemaliza michezo yake ya kutest mitambo baada ya kuifumua Mlandege kwa mabao 4-1 kwenye mchezo uliopigwa jana saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Prisons yamefungwa na Lambati Sabiyanka dakika ya 8 na 40, Leunsi Mutalema dakika ya 62 na Eliuti Mpepo dakika ya 84 huku bao pekee la Mlandege likifungwa na Abubakar Ame “Luiz” dakika ya 54. Prisons iliweka Kambi Visiwani hapa tangu Jumamosi ya Agost 12, 2017 ambapo ilicheza michezo ya kirafiki 5 na kushinda michezo 4 huku mchezo 1 wakitoka sare na Black Sailors ambapo walizifunga timu ya Mlandege, Ngome, KMKM na Dula Boys. Leo watasafiri na majira ya saa 3 asubuhi kwa kurudi Dar es salaam huku wakiwashukuru wapenz wote wa mpira hapa zanzibar na kushukuru uongozi wa ZFA kwa kuwatafutia timu ambazo zimewapa mazoezi makubwa. Prisons ambayo inafundishwa na kocha Mzanzibar Abdallah Mohd “Bares” iliweka kambi visiwani hapa kwa kujiandaa na ligi kuu sok

HILIKA AIBUKA MFUNGAJI BORA LIGI YA ZANZIBAR

Image
Mshambuliaji wa Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2016/2017 baada ya kufunga jumla ya mabao 14 katika hatua ya 8 bora. Hilika alianza dalili za kuwania ufungaji bora baada ya kushinda yeye pia kwenye ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo alishinda jumla ya mabao 19 katika kanda hiyo, hivyo ukipiga hesabu 19 na 14 utapata 33 ambayo ndio idadi ya mabao aliyofunga msimu huu wote tangu ligi ilipoanza kanda mpaka kufikia hatua ya 8 bora. Nafasi pili imekamatwa na Mwalim Mohd wa Jamhuri aliyefunga mabao 10 katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora. Mtandao huu umepiga stori na mshambuliaji huyo na kutaka kujua amejisikiaje kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo ambapo amefurahishwa mno na kusema kuwa ni lengo lake kuwa mfungaji bora na katimiza. “Nimefurahi sana kwani niliweka lengo hilo lakini nawashukuru viongozi wangu wote pamoja na wachezaji wangu kwani bila ya ushirikiano wao siwezi kufaniki

ZIMAMOTO YAUNGANA NA JKU KUWAKILISHA ZANZIBAR CAF

Image
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Zimamoto imefanikiwa kumaliza ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora kwa kushika nafasi ya pili baada ya kuichapa Kizimbani mabao 8-1 mchezo uliopigwa jana katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. Kwa matokeo hayo Zimamoto imefikisha alama 28 na kushika nafasi ya pili ambapo Bingwa wa ligi hiyo ni JKU alitangazwa karibu ya wiki moja nyuma. Bingwa (JKU) na Makamo Bingwa wa ligi hiyo (Zimamoto) watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo msimu uliopita waliwakilisha Zimamoto na KVZ ambao wote walitolewa mzunguko wa kwanza.

RAIS MPYA WA TFF AONEKANA UWANJANI SIMBA IKIBANWA NA MLANDEGE

Image
Rais mpya wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Walace Karia alikuwa mmoja kati ya watu waliohudhuria mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Mlandege ambao ulipigwa jana saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan timu hizo zikitoka sare ya 0-0. Jumamosi iliyopita ya Agost 12, 2017 Karia alishinda Urais wa TFF baada ya kupata kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo uliofanyika Mjini Dodoma. Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi. Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.

SIMBA YABANWA NA MLANDEGE, KESHO WATAKIPIGA TENA NA GULION

Image
Kikosi cha Simba Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba jana imebanwa mbavu na watoto wa Abdul Satar timu ya Mlandege baada ya kutoka sare tasa 0-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Amaan saa 2 za usiku. Simba iliwachezesha nyota wake kadhaa wapya akiwemo Mlinda Mlango Aishi Manula, mlinzi Salim Mbonde pamoja na kiungo Haruna Niyonzima huku washambuliaji wake wapya hatari Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco hawakucheza. Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia ni mchezo wake wa tano wa kirafiki katika kipindi hichi cha kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2017-2018. Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam kisha kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0 na jana kutoka sare ya 0-0 na Mlandege.

SIMBA NA MLANDEGE HAPATOSHI LEO USIKU

Image
Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, leo Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan. Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne. Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam na mwisho kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0. Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita ya Agost 13 walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan ambapo leo watakipiga tena na Simba.

DIRISHA LA USAJILI ZANZIBAR KUFUNGWA LEO ALHAMIS

Image
Dirisha la uhamisho na usajili rasmi litafungwa leo Alhamis Agost 17 majira ya saa 6:00 za usiku ambapo Makocha na Viongozi wengine wa Vilabu wamezidi kuwa bize kutafuta wachezaji wanaowahitaji ili kuziboresha timu zao katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018. Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kilitangaza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 kufunguliwa July 17, 2017 na kumaliza leo Alhamis Agost 17, 2017. Zoezi hilo ni kwaajili ya Madaraja yote kuanzia ligi kuu soka ya Zanzibar, ligi daraja la kwanza Taifa, la Pili Taifa hadi ligi za Madara ya Wilaya.

ZIMAMOTO NA JAMHURI, BOYS ZAGOMBEA NAFASI YA KUSHIRIKI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, WAPISHANA KWA POINT 1 NA UMEBAKI MCHEZO 1

Image
Kikosi cha Zimamoto  Bingwa mpya wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2016-2017 tayari ameshapatikana ambae ni JKU huku akiwa amebakiwa mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mwenge utakaopigwa Jumamosi ya Agost 19, 2017 katika uwanja wa Amaan. Lakini homa kali katika ligi hiyo ni nani atamaliza nafasi ya pili kati ya Zimamoto yenye alama 25 au Jamhuri yenye points 24 au Jangombe Boys yenye alama 24 pia ambapo wote wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi. Kwa mujibu wa ratiba Zimamoto atamalizana na Kizimbani wakati Jamhuri watakipiga na Jang’ombe Boys ambapo michezo hiyo ilikuwa imepangwa siku tofauti katika uwanja wa Gombani yani Jumamosi na Jumapili lakini kutokana na umuhimu wa michezo hiyo ZFA huenda ikalazimika michezo hiyo kuipanga siku moja na wakati mmoja ili kuepusha upangaji wa matokeo. Bingwa na Makamo Bingwa wa ligi hiyo watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo msimu uliopita waliwaki

KWEREKWE CITY WALIANZA NA WENGINE WAMEFUATIA, TIMU 4 ZIMEJULIKANA ZILIZOPANDA LIGI DARAJA LA PILI TAI

Image
Bechi la Ufundi wa Kwerekwe City Timu 4 zilizofanikiwa kupanda daraja la Pili Taifa kutoka la Pili Wilaya zimeshapatikana ambazo ni Kwerekwe city, New King, Mlandege na Mfenesini. Timu hizo msimu mpya wa mwaka 2017-2018 zitashiriki ligi daraja la Pili Taifa ambapo ligi hiyo itakuwa na timu 36 na itachezwa kwa mfumo wa makundi ambapo zitapangwa kwenye makundi matatu na kila kundi kushuka timu 3. Timu mbili za juu za daraja hilo zitapanda daraja la kwanza Taifa kwa msimu wa mwaka 2018-2019.   Kikosi cha Mlandege

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA KESHO ALHAMIS, HAKUNA KUONGEZA SIKU-KATIBU ZFA

Image
Dirisha la uhamisho na usajili rasmi linafungwa kesho Alhamis Agost 17 majira ya saa 6:00 za usiku ambapo Makocha na Viongozi wengine wa Vilabu wamezidi kuwa bize kutafuta wachezaji wanaowahitaji ili kuziboresha timu zao katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018. Akizungumza na Mtandao huu katibu mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema usajili unafungwa kesho Agost 17 na wao ZFA hawatoongeza siku wala muda ukifika wakati uliopangwa zoezi hilo litapigwa kufuli. “Ni kweli zoezi la uhamisho na usajili linafungwa kesho Alhamis saa 6:00 za usiku na wala hatutarajii kuongeza siku wala saa, muda ukifika zoezi hilo litafungiwa”. Alisema Tedy. Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kilitangaza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 kufunguliwa July 17, 2017 na kumaliza kesho Agost 17, 2017. Zoezi hilo ni kwaajili ya Maraja yote kuanzia ligi kuu soka ya Zanzibar, ligi daraja la kwanza Taifa, la Pili Taifa hadi ligi za Madara ya Wilaya.

KESHO NI ZAMU YA SIMBA NA MLANDEGE

Image
Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, kesho Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan. Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne. Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam na mwisho kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0. Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita ya Agost 13 walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan ambapo kesho watakipiga tena na Simba.   Kikosi cha Mlandege

JUUKO MURSHID KUTUA ZENJ KUUNGANA NA WENZAKE KAMBI YA SIMBA, NYONI NAE KUTINGA ZENJ KESHO AKITOKEA BURUNDI MSIBANI

Image
Mlinzi wa kati wa Simba Mganda Juuko Murshid wakati wowote kuanzia leo anatarajiwa kujiunga na wenzake kambini Visiwani Zanziabar kwaajili ya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga utakaupigwa Agost 23, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam. Akizungumza na Mtandao huu Mratibu wa Simba Abbas Suleiman amesema Juuko yupo Dar es salam akitokea Afrika ya Kusini na leo Jumanne muda wowote ataungana na wenzake kambi hapa Zanzibar. “Juuko yupo Dar es salam na muda wowote kuanzia Jumanne ataungana na wenzake hapa Zanzibar”. Wakati huo huo mlinzi mpya wa Simba Erasto Edward Nyoni nae akitarajiwa kuungana na wenzake kuanzia kesho Jumatano ambapo anatokea Burundi msibani. “Nyoni ataungana na wenzake kesho Jumatano mana alikuwepo Burundi kwenye msiba wa bamkwe wake na leo Jumanne atafika Dar es salam kisha kuja huku Zenj, alikwenda msibani baada ya kufiwa na bamkwe wake hivyo sisi tulimpa nafasi hiyo na karibu ataungana na wenzake”. Alisema Abba

SIMBA WAANZA KUJIFUA KWENYE UWANJA WA AMAAN

Image
Kikosi cha Simba leo Jumanne Agost 15 kimeanza mazoezi yake katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar mazoezi ambayo yamefanyika kuanzia saa 3 za asubuhi katika uwanja huo. Simba waliwasili Zanzibar jana Jumatatu wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao jana asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia. Kambi ya Simba visiwani hapa watakaa mpaka Agost 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Agost 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam. Abbas Suleiman ambae ni mratibu wa timu ya Simba amezungumzia sababu kubwa inayowavutia kuweka kambi Zanzibar ambapo amesema Zanzibar ni nyumbani kwao. “Zanzibar ni nyumbani ndio mana tunapenda kuja kuweka kambi mara nyingi, na tunapenda kuja kuweka kambi hapa si tukikutana na Yanga tu hata baadhi ya mechi nyengine, hapana siri nyengine yoyote isipokuwa hapa ni nyumbani tu, kuna utulivu wa h

KUNA SIRI GANI ZANZIBAR? SIMBA YAWASILI UNGUJA, YANGA YAFIKA PEMBA

Image
Kikosi cha wachezaji 23 cha Simba kimewasili Visiwani Zanzibar jioni ya leo wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao leo asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia. Simba wataweka kambi visiwani hapa mpaka Agost 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao utakaopigwa Agost 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam. Simba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan ambapo wakitarajiwa kucheza michezo 2 ya kirafiki visiwani hapa. Kambi ya Simba ipo kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

TIMU NYENGINE YA BARA KUCHEZA NA YA ZANZIBAR KESHO FUONI

Image
Timu ya Tanzania Prisons ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar kesho Jumanne Agost 15, 2017 itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Fuoni kuanzia saa 10:00 za jioni. Kiingilio katika mchezo huo ni Shilingi Elfu moja tu. Prisons ambayo inafundishwa na kocha Mzanzibar Abdallah Mohd “Bares” ipo kambi visiwani hapa kwa kujiandaa na ligi kuu soka ya Tanzania bara msimu mpya ambapo mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo watacheza Jumamosi Agost 26, 2017 dhidi ya timu mpya iliyopanda daraja ya Njombe Mji. Kikosi cha zamani chaTanzania Prisons

LAKIDATU MABINGWA WAPYA KIPWIDA CUP, NABIL JAJA NA ALI BAUSI WAENDELEA KUNGARA

Image
Michuano ya kipwida CUP imefikia tamati jana kwa msimu wa 2017 kwa kupigwa mchezo wa fainal kati ya Njaa kali na Lakidatu ambapo lakidatu imetwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa kutoka na ushindi wa mabao 3-1. Mchezo huo ambao umehudhuriwa na mashabiki wengi katika dimba hilo la lion kids huko Maungani Wilaya ya Magharibi B Unguja. Mabao ya Lakidatu yamefungwa na Nabil Amour “Jaja” dakika ya 3, 31 na Ali Bausi dakika ya 63 na lile la Njaa kali likafungwa na Abrahman Othman dakika ya 7. Bingwa ambao ni Lakidatu wamekabidhiwa Ng'ombe, Kombe kubwa,  Medali na seti ya jezi huku mshindi wa pili timu ya Njaa kali ikapewa medali, seti ya jezi na mbuzi Mnyama na timu zote shiriki ambazo 16 zimepewa mpira mmoja mmoja.

AJIBU AANZA MAKALI YAKE ZENJ, AFANYA VITU SI MCHEZO YEYE NA KAMUSOKO

Image
Kikosi cha Yanga kilichoanza mchezo wa jana Mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Ajib jana ameonesha kiwango cha hali ya juu kabisa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege uliopigwa saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mbali ya kuonesha uhodari wake wa kuuchezea mpira Ajibu pia alifungua akaunti yake ya mabao baada ya kufunga bao lake la kwanza dakika ya 50 katika historia ya klabu yake hiyo mpya tangu ajiunge nayo akitokea Simba. Bao hilo la Ajib ni msaada mkubwa wa Kiungo wa wakimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko ambae alipiga shuti kali na Ajib akamalizia. Bao jengine la Yanga lilifungwa na Emanuel Martin dakika ya 73 ambapo ni bao lake la pili katika msimu huu kuanza kufuatia kushinda bao la ushindi Yanga walipoifunga Singida United 3-2. Kikosi cha Yanga kimeondoka  kisiwani Unguja asubuhi ya leo Jumatatu kwa Ndege na kwenda Kisiwani Pemba kuweka kambi kujiandaa na pambano na mtani wake, Simba katika mchezo

MASHINDANO YA VYUO VYA MAFUNZO YA AMALI KUFANYIKA ZANZIBAR

Mamlaka ya Mafunzo ya Amali imeandaa mashindano ya mpira wa miguu ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya kesho Jumaatatu Agost 14, 2017 ambapo yatazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Amani nje kwa kushirikisha vyuo 12 vilivyopo chini ya mamlaka hiyo. Akizugumza na Mtandao huu mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo mwalimu Mkubwa Ibrahim Khamisi amesema kwa kuamini michezo ni ajira ndio maana wakafanya hivyo na lengo nikupata washiriki kwenye mashindano ya elimu bila malipo. “Michezo ni ajira ndo mana tumeanzisha mashindano haya, tunajua vipaji vipo vingi sana Zanzibar, hivyo tunawaomba wadao wa soka kujitokeza kuangalia vipaji”. Alisema Mkubwa. Katika Mashindano hayo ambayo yamejumuisha jumla ya Vyuo 12 ambapo vimepangwa katika Makundi 2 tofauti yani kundi A na B. Kundi A kuna chuo cha Institute of Business and Social Study, Zanzibar Commercial Institute, Zanzibar Mosquito Net, Chuo cha Wazazi cha Forodhani na Chuo cha Mwanakwerekwe wakati kundi B kuna chuo cha Meli

YANGA SC YAFIKA UNGUJA LEO USIKU KUCHEZA NA MLANDEGE, KESHO ASUBUHI PEMBA KWAJILI YA MPAMBANO WAO DHIDI YA SIMBA

Image
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga wamewasili kisiwani Unguja leo saa 5 za asubuhi wakitokea Jijini Dar es salam ambapo leo saa 2:00 za usiku watacheza mchezo wa kirafiki na Mlandege SC mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Amaan. Yanga wamefikia katika Hoteli ya Lail-Noor ambayo ipo Maisara Mjini Unguja. Kesho asubuhi Yanga wataondoka kisiwani Unguja na kwenda Kisiwani Pemba kuweka kambi kujiandaa na pambano na mtani wake, Simba katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa Agost 23, 2017 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam.   Kushoto ni Haji Mwinyi Ngwali "Bagawai" kati ni Abubakar Khatib Haji "Kisandu" na kulia ni Abdallah Haji Shaibu "Ninja"

KAPINGA ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA MAJESHI, AZIDI KUWAPA HAMASA YA KUTWAA UBINGWA

Image
Wanamichezo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wametakiwa kuzidisha nidhamu, upendo, umoja na mshikamano katika kuhakikisha wanapata mafanikio katika Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati ya mwaka huu ambayo yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia Agost 26, 2017. Wito huo umetolewa na mkuu wa operesheni, mafunzo na michezo ndani ya jeshi la wananchi wa Tanzania Brigidia Jeneral Alfred Kapinga alipotembelea kambi ya timu hiyo ambayo ipo Migombani Jeshini Mjini Unguja. Alisema nidhamu na upendo ndio silaha kubwa ya mafanikio, hivyo anaamini wakiendelea kutunza watafanikiwa kubeba ubingwa katika mashindano hayo. “Mulichaguliwa wengi sana lakini mumechujwa na sasa mumebakia nyinyi, naamini nidhamu, upendo, umoja na mshikamano ndio silaha kubwa ya mafanikio yenu, endelezeni naamini mutabeba ubingwa mimi sina wasi wasi na nyinyi”. Alisema Kapinga. Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Bur

MASHINDANO YA BASEBALL TANZANIA KUFANYIKA KESHO ZANZIBAR

Image
Chama cha Baseball na Softball Zanzibar (ZABSA) kimeandaa Mashindano maalum ya Mabingwa ya mchezo huo Mashindano ambayo itashirikisha timu za Zanzibar na Tanzania Bara ambapo kesho Jumamosi yakitarajiwa kuanza na kumalizika kesho kutwa Jumapili katika viwanja vya Amaan Nje. Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Chama hicho Othman Ali Msabaha amesema lengo la kuandaa Mashindano hayo ni kuzidi kuuhamasisha mchezo huo ambao kwa Zanzibar una miaka 3 wakati kwa bara una miaka 8 tangu kuanzishwa kwake. “Lengo la Mashindano haya ni kuzidi kuusambaza huu mchezo mana tunataka uzidi kukuwa kwa kasi sana, na pia tunataka uwe mpaka kwenye vikosi vya ulinzi na mitaani isiwe kwenye Mashule tu”. Alisema Msabaha. Jumla ya timu 4 zitashiriki Mashindano hayo zikiwemo mbili kutoka Tanzania Bara timu ya Skuli ya Azania pamoja na Kibasila ambapo kwa Zanzibar zitashiriki timu za Skuli ya Mwanakwerekwe pamoja na Kombain ya Unguja.

KIPANGA INAKUJA KIVYENGINE MSIMU HUU, YAACHA WACHEZAJI 8 NA KUSAINI 8

Image
Baada ya msimu ulopita chupuchupu kunusurika kushuka daraja timu ya Kipanga imejipanga upya kuhakikisha msimu huu inafanya vizuri katika ligi kuu soka ya Zanzibar ambayo inatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 1,2017. Akizungumza kwa kujiamini mwenyekiti wa timu ya Kipanga Said Ali Juma Shamhuna amesema timu yake imesajili wachezaji wapya 8 na kuwaacha 8 ambapo kwasasa ameshafunga usajili baada ya kusajili makinda hao huku akiamini msimu huu watafanya vizuri. “Tumesajili wachezaji 8 wapya na tumewaacha 8, hawa tulosajili wote ni vijana wakitokea Central na daraja la pili, kati ya hao 8 wapya wanne ni askari na wanne ni raia naamini msimu huu tutafanya vizuri sana, wachezaji niliowasajili ni Yahya anatokea Muembeladu, Ibrahim maarufu Deco anatokea Bububu, Benzema anatokea Medson na Cheda pia anatokea Medson hao ni wachezaji raia lakini wachezaji Majeshi nilioongeza ni Moko, Ahmada, Ali Mohd na Ali Bashir”. Alisema Shamhuna. Msimu uliopita Kipanga bado kidogo ishuke daraja baada ya

UJAMAA NA UKONGWE WAO WAFUNDISHWA SOKA NA VIJANA WA GULIONI

Image
Kikosi cha Ujamaa Sports Club Timu kongwe Visiwani Zanzibar Ujamaa Sports Club wamekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa vijana wa Gulion FC kwenye mchezo maalum wa Sherehe za kutimiza miaka 60 kwa Ujamaa mchezo ambao umesukumwa jana saa 2 za usiku kwenye uwanja wa Amaan. Mabao ya Gulioni katika mchezo huo yamefungwa na Abdul Hamid Ramadhan dakika ya 45, Ali Juma dakika ya 71 na Shaabani Hassan dakika ya 88 huku bao pekee la Ujamaa likifungwa na Mwinyi Ame dakika ya 79. Ujamaa ndio timu aliyewahi kucheza kwa kiwango cha hali ya juu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambapo Katika mchezo huo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh Rashid Ali Juma akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia alikuwa mlinda mlango hatari wa timu hiyo miaka iliyopita. Msimu huu mpya wa mwaka 2017-2018 Ujamaa itashiriki ligi daraja la Pili Taifa Unguja wakati Gulioni FC itacheza