NEGRO DAY KESHO, WATAKIPIGA NA TAIFA YA JANG’OMBE AMAN USIKU
Tamasha la Negro Day litafanyika kesho Jumanne Agost 29, 2017
ambapo timu ya Negro FC itacheza mchezo maalum wa kirafiki na Timu ya Taifa ya
Jang’ombe mchezo ambao utasukumwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa Negro FC Hussein Ahmada
amesema katika Tamasha hilo wao Negro watalitumia pia kwaaajili ya
kuwatambulisha wachezaji wao wapya ambao wamesajiliwa kwaajili ya msimu mpya wa
mwaka 2017-2018.
Amesema pia watatangaza Benchi jipya la ufundi wakiwemo kocha
mkuu na msaidizi wake pamoja na kumtangaza mfadhili wao mpya ambae ni mkorea.
Aidha Ahmada amesema watazitambulisha jezi zao mpya na pia kutakuwa
na burudani mbali mbali katika Tamasha hilo ambalo litaadhimishwa kila mwaka
siku ya Agost 29.
“Negro day ni siku maalum kwetu kwa kila mwaka ikifika Agost
29 tutafanya tamasha maalum, tutawatangaza wachezaji wetu wapya, benchi la
ufundi pamoja na mfadhili wetu tutamtangaza na mambo mengine mengi tu”. Alisema
Ahmada.
Comments
Post a Comment