JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE
Timu za JKU Academy zinaondoka usiku wa leo kwa boti ya usiku
kwenda Jijini Dar es salam kisha saa 12 za asubuhi kesho Jumatatu kuanza safari
ya Arusha ambapo wanakwenda katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na
Kati (Rolling Stone) mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi July 9-19,
2017.
JKU mwaka huu wanatarajia kushiriki timu tatu tofauti katika
Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu
60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar usiku wa leo.
Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU
Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano.
Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza
rasmi July 9 na kumalizika July 19, 2017 ambapo msimu huu kumepangwa vituo
tofauti makundi mengine yamepangiwa Arusha, mengine Manyara.
Comments
Post a Comment