Posts

Showing posts from July, 2017

BUSHIR NDO BASI TENA MWADUI FC, AONDOKA NA UJUMBE MZITO

Image
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush” amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania bara. Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa. “Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kua kocha Mkuu wa timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka nlokua nkiihudumikia. Ukweli hakuna Mtz hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua ni kwa vp nliisaidia timu hio ktk kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu hiyo na naam niliifanya na lkn c kwa ujanja wng tuu bali na Mungu alinisaidia ktk kuifanikisha kazi hio.. Kuna v2 v3 ambavyo viliniponza hadi kufikia kuipoteza kazi yng hio.. La kwanza ni haki zangu {financially} la pili ni kuusu usajili na la tatu ni kuusiana na chuki na choyo kutoka kwa asst nliyekua nae vl yy nd

ALICHOKISEMA CAPTAIN SANGULA BAADA YA KUSAJILIWA NDANDA

Image
Mlinzi wa kati Ibrahim Mohammed “Sangula” aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Jang’ombe Boys, amejiunga rasmi na klabu ya Ndanda FC kwa mkataba wa miaka 2 ambapo kesho Jumanne Agost 1, 2017 akitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar kuelekea Mtwara ilipo klabu yake hiyo mpya. Sangula ambae ndie Captain wa Jang’ombe boys amewashukuru wadau wote wa soka Visiwani Zanzibar kwa ushirikiano wao huku akisisitiza hawezi kumsahau kocha wake Issa Amasha na ataendelea kuipenda Boys licha ya kuhama. “Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa na Ndanda FC, lakini nampongeza sana kocha wangu Amasha kwa kunilea vizuri kipindi chote mpaka sasa nimesajiliwa kucheza ligi ya bara, naipenda sana Jang’ombe boys lakini ndio maisha ya soka hutodumu timu moja naenda kutafuta maisha kwengine, nawaomba waniombee dua ili mimi na Wazanzibar wengine tunacheza soka tufanikiwe kutimiza ndoto zetu”. Alisema Sangula. Sangula alionekana sana katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na Mashindano ya Spo

TAIFA YAENDELEZA UTEJA KWA BOYS, YAPIGWA MARA 3 MFULULIZO

Image
Taifa ya Jang'ombe Timu ya Jang'ombe boys imeendeleza wimbi lake la ushindi mbele ya kaka zao Taifa ya Jang'ombe baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa jana jioni katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Boys yamefungwa na Hafidh Barik (Fii) dakika ya 6 na Juma Ali (Mess) dakika ya 66. Kwa matokeo hayo rikodi bado inawapendelea Boys ambapo timu hizo zimeshakutana mara 8 katika historia huku mara 5 Boys akishinda, mara 2 kafungwa na mara 1 sare ambapo Dabi hiyo ya Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe Boys ndio dabi inayoongoza kukutana mara nyingi msimu mmoja kuliko dabi zote Dunia nzima ambapo dabi hiyo imekutana mara 6 hii haijawahi kutokea Dabi yoyote Duniani kukutana mara 6 ndani ya msimu mmoja. Ndani ya msimu huu wa mwaka 2016-2017 ambao kwa Zanzibar bado unaendelea dabi hiyo walikutana Novemba 19, 2016 katika Bonanza la Coconut FM ambapo matokeo Taifa 2-0 Boys huku mabao ya Taifa yalifungwa na Mkongo Barak

BUSHIR NDO BASI TENA MWADUI FC, AONDOKA NA UJUMBE MZITO

Image
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush” amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania bara. Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa. “Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kua kocha Mkuu wa timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka nlokua nkiihudumikia. Ukweli hakuna Mtz hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua ni kwa vp nliisaidia timu hio ktk kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu hiyo na naam niliifanya na lkn c kwa ujanja wng tuu bali na Mungu alinisaidia ktk kuifanikisha kazi hio.. Kuna v2 v3 ambavyo viliniponza hadi kufikia kuipoteza kazi yng hio.. La kwanza ni haki zangu {financially} la pili ni kuusu usajili na la tatu ni kuusiana na chuki na choyo kutoka kwa asst nliyekua nae vl yy nd

TAIFA YAENDELEZA UTEJA KWA BOYS, YAPIGWA MARA 3 MFULULIZO

Image
Timu ya Jang'ombe boys imeendeleza wimbi lake la ushindi mbele ya kaka zao Taifa ya Jang'ombe baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan. Mabao ya Boys yamefungwa na Hafidh Barik (Fii) dakika ya 6 na Juma Ali (Mess)  dakika ya 66. Nako huko katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba timu ya Kizimbani wakaichapa Okapi mabao 2-1. Mabao ya Kizimbani yamefungwa na Khamis Suleiman dakika ya 49 na Haji Rashid dakika 62 wakati bao pekee Okapi limefungwa na Seif Saleh dakika ya 90.

HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA

Image
Abdull Yussuf wa Mwenge Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri Mwalimu Mohammed leo amefanikiwa kufunga mabao 3 (Hat trick) katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora na timu yake Jamhuri iliposhinda mabao 5-3 dhidi ya Mwenge kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Gombani Pemba. Mabao hayo amefunga katika dakika ya 11, 15, 27 ambapo katika mchezo huo huo mshambuliaji wa timu ya Mwenge Abdull Yussuf nae amelipa hat trick baada ya kufunga mabao yote 3 ya Mwenge katika mchezo huo waliopoteza mabao ambayo alifunga dakika ya 33, 37 na 79. Washambuliaji hao wote wawili kwasasa ndio vinara wa kuzifumania nyavu katika ligi hiyo ambapo wote wakiwa na jumla ya mabao 7 kila mmoja wakifuatiwa na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto mwenye mabao 6 baada ya leo kufunga bao moja timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya JKU kwenye uwanja wa Amaan. Jumla ya Hat trick tatu mpaka sasa zimeshafungwa katika ligi hiyo zikiwemo mbili za leo pamoja nay a wiki iliyopita il

JKU NA ZIMAMOTO HAKUNA MBABE, JAMHURI YAPATA USHINDI MNENE, KESHO TAIFA NA BOYS

Image
Mzunguko wa 9 wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora umeanza jioni ya leo kwa kupigwa michezo 2 katika viwanja 2 tofauti. Katika uwanja wa Amaan kisiwani Unguja timu ya JKU na Zimamoto wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1. Bao la Zimamoto limefungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 15 wakati bao la JKU limefungwa na Is haka Othman “Bopa” dakika ya 81. Nako huko katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, timu ya Jamhuri imeondoka na alama 3 muhimu baada ya kushinda mabao 5-3 dhidi ya Mwenge. Mabao ya Jamhuri yamefungwa na Mwalimu Mohammed (Hat trick) dakika ya 11, 15, 27, Khamis Abrahman “Mburu” dakika ya 60, na Mussa Ali Mbarouk dakika ya 88 ambapo mabao ya Mwenge yote matatu (Hat trick) yamefungwa na Abdull Yussuf dakika ya 33, 37 na 79. Ligi hiyo itaendelea tena kesho saa 10:00 za jioni kwa kupigwa mchezo kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys kwenye uwanja wa Amaan na katika uwanja wa Gombani watasukumana kati ya Okapi dhidi

DABI YA JANGOMBE KESHO KATI YA TAIFA NA BOYS, RATIBA KAMILI HII HAPA

Image
9 TH   ROUND J’MOSI 29/7/017 33 ZIMAMOTO VS JKU SAA 10  JIONI AMAAN J’MOSI 29/7/017 34 JAMHURI VS MWENGE SAA 10  JIONI GOMBANI J’PILI 30/7/017 35 OKAPI VS KIZIMBANI SAA 10  JIONI GOMBANI J’PILI 30/7/017 36 JANG’OMBE BOYS VS TAIFA SAA 10:00 JIONI AMAAN

LIGI KUU SOKA ZENJ KESHO ZIMAMOTO V/S JKU, JUMAPILI DABI YA JANGOMBE TAIFA V/S BOY, RATIBA KAMILI HII HAPA

Image
Kikosi cha Zimamoto Kikosi cha JKU 9 TH   ROUND J’MOSI 29/7/017 33 ZIMAMOTO VS JKU SAA 10  JIONI AMAAN J’MOSI 29/7/017 34 JAMHURI VS MWENGE SAA 10  JIONI GOMBANI J’PILI 30/7/017 35 OKAPI VS KIZIMBANI SAA 10  JIONI GOMBANI J’PILI 30/7/017 36 JANG’OMBE BOYS VS TAIFA SAA 10:00 JIONI AMAN

DABI ILOKUTANA MARA NYINGI DUNIANI NDANI YA MSIMU MMOJA NI DABI YA JANG’OMBE KATI YA TAIFA NA BOY

Image
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe Dabi ya Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe Boys ndio dabi inayoongoza kukutana mara nyingi msimu mmoja kuliko dabi zote Dunia nzima. Msimu huu dabi hii mpaka sasa ishakutana mara 5 na kesho kutwa Jumapili ya July 30, 2017 watakutana tena kwa mara ya 6, hii haijawahi kutokea Dabi yoyote Duniani kukutana mara 6 ndani ya msimu mmoja. Kila mji kuna kuwa na dabi mfano pale Jijini Dar es salam Kariakoo kuna dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, au kule London Uengereza kuna dabi ya London kati ya Arsenal na Totenham Spurs, au kule Jijini Manchester Uengereza kuna dabi ya Manchester kati ya Manchester City na Machester United, au kule Spain kuna dabi ya Madrid kati ya Atletico Madrid na Real Madrid, lakini dabi zote hizo kwa msimu mmoja zinakutana mara 2, 3 au 4, ila kwa dabi ya Jang’ombe itakuwa imevunja rikodi dabi ya kwanza kukutana mara nyingi msimu mmoja. Ndani ya msimu huu wa mwaka 2016-2017 ambao kwa Zanzibar bado

CAPTAIN WA GULIONI AWA MZANZIBAR MWENGINE KUSAJILIWA LIGI KUU BARA

Image
Timu ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga imemsajili beki wa kati ambae ni nahodha wa timu ya Gulioni Ali Hamad Ali “Kinibu” akitokea kwenye ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja. Kinibu amesajiliwa kwenye kikosi hicho cha wapiga debe wa Shinyanga kwaajili ya kuongeza nguvu msimu ujao wa mashindano yakiwemo kombe la FA pamoja na ligi kuu soka Tanzania bara. Mara baada ya kusaini miaka 2 kuitumikia timu hiyo Kinibu amefurahishwa mno na kusema malengo yake ni kucheza nje ya Tanzania hivyo ataendelea kupambana  ili atimize ndoto zake. “Nimefurahi kusaini mkataba wa miaka 2 Stand United, malengo yangu ni kucheza nje ya Tanzania ntaendelea kujituma ili nitimize ndoto zangu”. Alisema Kinibu. Kinibu anavutiwa zaidi na uchezaji wa mlinzi wa kati wa klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa Laurent Koscielny pamoja na mlinzi wa Spain Sergio Ramos.

HILIKA NA AHMED WAFUKAZANA KWA KUPACHIKA MABAO LIGI KUU YA SOKA ZANZIBAR

Image
Ibrahim Hamad Hilika Mshambuliaji Ahmed Ali Omar wa Jamhuri pamoja na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto wao ndio vinara wa kupachika mabao kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora. Washambuliaji hao mpaka sasa wameshafunga jumla ya mabao 5 kila mmoja katika michezo 8 waliyocheza. Wanaochuwana na washambuliaji hao ni Mshambuliaji wa Jang’ombe Boys Khamis Mussa “Rais”, Mwalimu Mohd wa Jamhuri pamoja na Abdull Yussuf wa Mwenge ambao wote wameshafunga mabao 4 kila mmoja. Wengine wanaofuatia ni Seif Saleh wa Okapi, Mussa Ali Mbarouk wa Jamhuri na Hassan Haji wa Zimamoto wote hao wana mabao 3. Hakim Khamis “Men” ndie Mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ulopita alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa msimu huo ambapo mpaka sasa hajapewa zawadi yoyote kwa kufanikiwa kuwa mfungaji

CAPTAIN WA TAIFA JANG’OMBE SALULA AZUNGUMZIA SABABU YA KUFANYA VIBAYA TIMU YAKE

Image
Ahmed Ali Suleiman “Salula”  Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Jang’ombe ambae pia ni nahodha wa timu hiyo Ahmed Ali Suleiman “Salula” amesema wao wachezaji hawana tatizo lolote mpaka sasa licha ya kucheza michezo 8 bila ya kupata ushindi hata mchezo mmoja. Salula amesema wanapigana kadri ya uwezo wao lakini anashangaa wanapata matokeo mabaya hivyo amewaomba Mashabiki wao waendelee kuwaunga mkono katika kipindi hichi kigumu kwani wao wanajitahidi kwa nguvu zote kupeleka furaha Taifa. “Sisi tunajishangaa sana, makocha wetu wanatufundisha vizuri kila siku na tukifika uwanjani tunapata nafasi nyingi sisi kuliko mpinzani wetu lakini utashangaa mwisho wa mchezo tunafungwa sisi au tunatoka sare, sisi wachezaji tushakaa pamoja na kujiuliza tuna tatizo gani lakini tunakosa jibu, hivyo nawaomba mashabiki wetu waendelee kuwa na sisi katika shida na raha na zaidi tutajipanga kwa msimu ujao mpya”. Alisema Salula. Katika hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar timu

JKU INAENDELEA KUONGOZA LIGI KUU ZENJ, ANGALIA MSIMAMO HUU HAPA

Image
Timu ya JKU

TAIFA YA JANG'OMBE BADO IPO ICU, MECHI YA 8 BILA YA USHINDI

Timu ya Taifa ya Jang'ombe imeendelea kuvuruga katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora baada ya jioni ya leo kukubali kuchapwa mabao 2-0 na JKU,  mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan. Mabao ya JKU yamefungwa na Mbarouk Chande dakika ya 58 na Amour Omar "Janja" dakika ya 64. Nako huko katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba timu ya Kizimbani imeichapa Mwenge bao 1-0. Bao la Kizimbani limefungwa na Ali Mkadam dakika ya 68. Ligi hiyo itaendelea Jumamosi. Zimamoto v/s JKU, Amaan. Jamhuri v/s Mwenge,  Gombani. Jumapili Okapi v/s Kizimbani,  Gombani. Jang'ombe boys v/s Taifa ya Jang'ombe Mechi zote hizo saa 10:00 za jioni.

MADUNDO APANIA KUPANDA TENA DARAJA TIMU YAKE YA VILLA UNITED

Image
Baada ya kufanikiwa kupanda daraja la kwanza Taifa msimu ulopita Timu ya Villa United “Mpira Pesa” yenye Maskani yake Mwanakwerekwe imepania na msimu huu mpya kuondoka daraja hilo na kupanda daraja jengine. Akizungumza na Mtandao huu kocha mkuu wa timu hiyo Ramadhan Abdulrahman “Madundo” amesema kwa soka la Zanzibar lilivo hawana sababu timu yao isipande tena daraja msimu huu kama ilivyofanya miaka miwili mfululizo iliyopita. “Sisi kila mwaka tunapanda daraja jengine sasa sioni sababu na mwaka huu tusipande daraja jengine, kwani nina wachezaji wenye uwezo binafsi na pia uongozi wangu upo imara”. Alisema Madundo. Timu ya Villa United ilianzishwa mwaka 2013 ambapo ilianzia kucheza madaraja ya Vijana Wilaya ya Mjini lakini ilipofika msimu wa mwaka 2015-2016 ilishiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini na kufanikiwa kupanda daraja, Msimu ulopita wa mwaka 2016-2017 Villa ilifanikiwa tena kupanda daraja la Kwanza Taifa ambapo msimu ujao mpya wa mwaka 2017-2018 pia wamepania

TIMU 4 ZILIZOPANGA MATOKEO 11-1, 7-1 CENTRAL WILAYA YA MJINI ZAPIGWA FAINI NA KUFUTWA KATIKA MASHINDANO, VIONGOZI WA TIMU HIZO WOTE WAFUNGIWA MWAKA MMOJA

Image
Kikosi cha FC Muembe beni Kamati ya Soka la Vijana Wilaya ya Mjini imezipiga faini ya jumla ya shilingi laki tatu na kuziondosha katika Mashindano timu za FC Muembe beni, Real Kids, Schalke 04 na King Boys baada ya kukutwa na hatia ya upangaji wa matokeo katika mechi zao za mwisho za hatua ya 4 bora zilizopigwa Jumapili iliyopita ya July 23, 2017. Katika michezo hiyo miwili iliyovikutanisha vilabu hivyo vinne, michezo ambayo ilikuwa inatafuta Bingwa wa Daraja hilo la Central ambapo timu ya Schalke 04 ilishinda mabao 11-1 dhidi ya King Boys wakati mchezo mwengine FC Muembe beni iliwafunga Real Kids 7-1 ndipo hapo baada ya kumalizika michezo hiyo viongozi wa Mashindano hayo wakashindwa kutoa zawadi na kupelekea jana kutoa maamuzi hayo baada ya kamati kujiridhisha. Khamis Machano ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema wametoa maamuzi hayo kwakuwa wamejiridhisha kwamba timu hizo zimepanga matokeo na kuamua kuzifuta na pamoja na kuzipiga faini ya shilingi laki tatu. “K

BOYS HOI KWA ZIMAMOTO, JAMHURI BADO KIGUGUMIZI

Image
Timu ya Zimamoto imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe Boys katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora uliosukumwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan. Goli la Zimamoto lilifungwa na Idrissa Simai Pandu dakika ya 84. Mchezo mwengine umepigwa katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba timu ya Jamhuri ikaenda sare ya 1-1 dhidi ya Okapi. Bao la Okapi limefungwa na Bakar Hamad dakika ya 5 wakati bao la Jamhuri limefungwa na Ahmed Ali Omar dakika ya 20. Ligi hiyo itaendelea tena kesho. J’TANO 26/7/017 31 MWENGE VS KIZIMBANI SAA 10  JIONI GOMBANI J’TANO 26/7/017 32 JKU VS TAIFA SAA 10JIONI AMAAN 9 TH   ROUND J’MOSI 29/7/017 33 ZIMAMOTO VS JKU SAA 10  JIONI AMAAN J’MOSI 29/7/017 34 JAMHURI VS MWENGE SAA 10  JIONI GOMBANI J’PILI 30/7/017 35 OKAPI VS