BUSHIR NDO BASI TENA MWADUI FC, AONDOKA NA UJUMBE MZITO

Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush”
amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania bara.

Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa.

“Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kua kocha Mkuu wa timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka nlokua nkiihudumikia. Ukweli hakuna Mtz hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua ni kwa vp nliisaidia timu hio ktk kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu hiyo na naam niliifanya na lkn c kwa ujanja wng tuu bali na Mungu alinisaidia ktk kuifanikisha kazi hio.. Kuna v2 v3 ambavyo viliniponza hadi kufikia kuipoteza kazi yng hio.. La kwanza ni haki zangu {financially} la pili ni kuusu usajili na la tatu ni kuusiana na chuki na choyo kutoka kwa asst nliyekua nae vl yy ndo nlomkuta pale.. So Paaalllsss kwa maelezo yng zaidi bc fwatilieni magazeti ya kesho vl kuna gazeti la michezo mtaikuta story hio.. Lkn all above all mii c mwalimu mkuu tena wa Mwadui fc”. Aliandika katika ukurasa wa Facebook.

“Any way! Who knows? Jst wait n c ni wapi ntakoelekea hukohuko ktk ligi kuu ya Vodacom na Inshllh ntawajulisha tuu Paaallllssss wngu, vl taari nshapata mialiko kadhaa ila tuu bado cjaamua ni wapi nielekee.. Paaalllss nimeamua kuwaambia ukweli wng ktk hili ili tuu mcsikilize ya wa2 mitaani vl ukweli ni huo.. Gd9t Paaaalllss...!!!!”.

Katikati ya msimu uliopita Bushir alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu kutoka chini na kufanya kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja.



Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS