HILIKA NA AHMED WAFUKAZANA KWA KUPACHIKA MABAO LIGI KUU YA SOKA ZANZIBAR

Ibrahim Hamad Hilika
Mshambuliaji Ahmed Ali Omar wa Jamhuri pamoja na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto wao ndio vinara wa kupachika mabao kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora.

Washambuliaji hao mpaka sasa wameshafunga jumla ya mabao 5 kila mmoja katika michezo 8 waliyocheza.

Wanaochuwana na washambuliaji hao ni Mshambuliaji wa Jang’ombe Boys Khamis Mussa “Rais”, Mwalimu Mohd wa Jamhuri pamoja na Abdull Yussuf wa Mwenge ambao wote wameshafunga mabao 4 kila mmoja.

Wengine wanaofuatia ni Seif Saleh wa Okapi, Mussa Ali Mbarouk wa Jamhuri na Hassan Haji wa Zimamoto wote hao wana mabao 3.


Hakim Khamis “Men” ndie Mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ulopita alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa msimu huo ambapo mpaka sasa hajapewa zawadi yoyote kwa kufanikiwa kuwa mfungaji bora.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS