CAPTAIN WA TAIFA JANG’OMBE SALULA AZUNGUMZIA SABABU YA KUFANYA VIBAYA TIMU YAKE

Ahmed Ali Suleiman “Salula” 

Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Jang’ombe ambae pia ni nahodha wa timu hiyo Ahmed Ali Suleiman “Salula” amesema wao wachezaji hawana tatizo lolote mpaka sasa licha ya kucheza michezo 8 bila ya kupata ushindi hata mchezo mmoja.

Salula amesema wanapigana kadri ya uwezo wao lakini anashangaa wanapata matokeo mabaya hivyo amewaomba Mashabiki wao waendelee kuwaunga mkono katika kipindi hichi kigumu kwani wao wanajitahidi kwa nguvu zote kupeleka furaha Taifa.

“Sisi tunajishangaa sana, makocha wetu wanatufundisha vizuri kila siku na tukifika uwanjani tunapata nafasi nyingi sisi kuliko mpinzani wetu lakini utashangaa mwisho wa mchezo tunafungwa sisi au tunatoka sare, sisi wachezaji tushakaa pamoja na kujiuliza tuna tatizo gani lakini tunakosa jibu, hivyo nawaomba mashabiki wetu waendelee kuwa na sisi katika shida na raha na zaidi tutajipanga kwa msimu ujao mpya”. Alisema Salula.


Katika hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Taifa ya Jang’ombe ndio timu pekee ambayo haijawahi kushinda hata mchezo mmoja katika michezo 8 iliyocheza baada ya kufungwa michezo 5 na kutoka sare michezo 3 wakiwa na alama 3 pekee ambapo mchezo unaofuata Taifa ya Jang’ombe watacheza na ndugu zao Jang’ombe Boys mchezo ambao utapigwa Jumapili ya July 30, 2017 saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS