RAIS MPYA WA TFF AONEKANA UWANJANI SIMBA IKIBANWA NA MLANDEGE
Rais mpya wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Walace
Karia alikuwa mmoja kati ya watu waliohudhuria mchezo wa kirafiki kati ya Simba
dhidi ya Mlandege ambao ulipigwa jana saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan
timu hizo zikitoka sare ya 0-0.
Jumamosi iliyopita ya Agost 12, 2017 Karia alishinda Urais wa
TFF baada ya kupata kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye
uchaguzi huo uliofanyika Mjini Dodoma.
Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay,
Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais
wa TFF.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu
wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya
Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha
miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Comments
Post a Comment