ZIMAMOTO NA JAMHURI, BOYS ZAGOMBEA NAFASI YA KUSHIRIKI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, WAPISHANA KWA POINT 1 NA UMEBAKI MCHEZO 1

Kikosi cha Zimamoto 
Bingwa mpya wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2016-2017 tayari ameshapatikana ambae ni JKU huku akiwa amebakiwa mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mwenge utakaopigwa Jumamosi ya Agost 19, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Lakini homa kali katika ligi hiyo ni nani atamaliza nafasi ya pili kati ya Zimamoto yenye alama 25 au Jamhuri yenye points 24 au Jangombe Boys yenye alama 24 pia ambapo wote wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa mujibu wa ratiba Zimamoto atamalizana na Kizimbani wakati Jamhuri watakipiga na Jang’ombe Boys ambapo michezo hiyo ilikuwa imepangwa siku tofauti katika uwanja wa Gombani yani Jumamosi na Jumapili lakini kutokana na umuhimu wa michezo hiyo ZFA huenda ikalazimika michezo hiyo kuipanga siku moja na wakati mmoja ili kuepusha upangaji wa matokeo.

Bingwa na Makamo Bingwa wa ligi hiyo watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo msimu uliopita waliwakilisha Zimamoto na KVZ ambao wote walitolewa mzunguko wa kwanza.



Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS