KUNA SIRI GANI ZANZIBAR? SIMBA YAWASILI UNGUJA, YANGA YAFIKA PEMBA


Kikosi cha wachezaji 23 cha Simba kimewasili Visiwani Zanzibar jioni ya leo wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao leo asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia.


Simba wataweka kambi visiwani hapa mpaka Agost 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao utakaopigwa Agost 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam.


Simba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan ambapo wakitarajiwa kucheza michezo 2 ya kirafiki visiwani hapa.


Kambi ya Simba ipo kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS