LAKIDATU MABINGWA WAPYA KIPWIDA CUP, NABIL JAJA NA ALI BAUSI WAENDELEA KUNGARA

Michuano ya kipwida CUP imefikia tamati jana kwa msimu wa 2017 kwa kupigwa mchezo wa fainal kati ya Njaa kali na Lakidatu ambapo lakidatu imetwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa kutoka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huo ambao umehudhuriwa na mashabiki wengi katika dimba hilo la lion kids huko Maungani Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Mabao ya Lakidatu yamefungwa na Nabil Amour “Jaja” dakika ya 3, 31 na Ali Bausi dakika ya 63 na lile la Njaa kali likafungwa na Abrahman Othman dakika ya 7.


Bingwa ambao ni Lakidatu wamekabidhiwa Ng'ombe, Kombe kubwa,  Medali na seti ya jezi huku mshindi wa pili timu ya Njaa kali ikapewa medali, seti ya jezi na mbuzi Mnyama na timu zote shiriki ambazo 16 zimepewa mpira mmoja mmoja.

Comments

  1. Safi sana mwanangu NABIL AMOUR JUMA wanakuita JAJA ila kwangu nitaendelea na jina langu la kukuita SHEARER

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS