SIMBA WAANZA KUJIFUA KWENYE UWANJA WA AMAAN
Kikosi cha Simba leo Jumanne Agost 15 kimeanza mazoezi yake
katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar mazoezi ambayo yamefanyika kuanzia saa
3 za asubuhi katika uwanja huo.
Simba waliwasili Zanzibar jana Jumatatu wakitokea Jijini Dar
es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa
Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao jana asubuhi waliondoka Unguja na
kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia.
Kambi ya Simba visiwani hapa watakaa mpaka Agost 22, 2017
siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Agost 23 kwenye uwanja
wa Taifa jijini Dar es salam.
Abbas Suleiman ambae ni mratibu wa timu ya Simba amezungumzia
sababu kubwa inayowavutia kuweka kambi Zanzibar ambapo amesema Zanzibar ni
nyumbani kwao.
“Zanzibar ni nyumbani ndio mana tunapenda kuja kuweka kambi
mara nyingi, na tunapenda kuja kuweka kambi hapa si tukikutana na Yanga tu hata
baadhi ya mechi nyengine, hapana siri nyengine yoyote isipokuwa hapa ni
nyumbani tu, kuna utulivu wa hali ya juu ndio mana tunapenda kuja Zanzibar”.
Alisema Abbas.
Kambi ya Simba ipo kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo
Maruhubi Mjini Unguja.
Comments
Post a Comment