SIMBA YABANWA NA MLANDEGE, KESHO WATAKIPIGA TENA NA GULION

Kikosi cha Simba
Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba jana imebanwa mbavu na watoto wa Abdul Satar timu ya Mlandege baada ya kutoka sare tasa 0-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Amaan saa 2 za usiku.

Simba iliwachezesha nyota wake kadhaa wapya akiwemo Mlinda Mlango Aishi Manula, mlinzi Salim Mbonde pamoja na kiungo Haruna Niyonzima huku washambuliaji wake wapya hatari Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco hawakucheza.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia ni mchezo wake wa tano wa kirafiki katika kipindi hichi cha kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2017-2018.

Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam kisha kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0 na jana kutoka sare ya 0-0 na Mlandege.

Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita ya Agost 13 walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan ambapo jana wakatoka sare ya 0-0 na Simba.

Simba watashuka tena dimbani kesho Jumamosi Agost 19, 2017 saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan ambapo watacheza na timu ya Gulioni FC “Chama la Wana na Upendo”.

 
Kikosi cha Mlandege

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS