BABAAKE MWINYI: UJIO WA GADIEL HAUNIPI HOMA YA KUKOSA NAMBA MWANANGU KIKOSI CHA KWANZA YANGA, BALI NDIO UTAKAMFANYA MWINYI APIGE KAZI ZAIDI
Baba mzazi na meneja wa Mwinyi Haji
Ngwali mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga Mzee Haji Ngwali amesema hana mashaka
na mtoto wake ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza kwa timu ya Yanga licha
ya kusajiliwa mlinzi mwengine wa kushoto Gadiel Michael aliyejiunga akitokea Azam FC.
Mwinyi ambae ni msimu wake wa tatu
tangu ajiunge na Yanga amekuwa na wakati mzuri tangu asajiliwe na timu hiyo
ambapo amecheza michezo mingi kuliko mpinzani wake wakati huo Oscar Joshua
ambapo kwasasa anampinzani mwengine Gadiel Michael aliyetoka Azam FC baada ya
Joshua kuachwa.
Mzee Haji amesema anaamini mazoezi
ndio kila kitu na mpira ni mchezo wa hadharani si mchezo wa kusifiwa katika
Magazeti hivyo muhimu kocha wao ndie anaejua nani atamrizisha na kupelekea
kumpanga.
Amesema anajua Mwinyi ametoka
Zanzibar kwaajili ya soka tu hivyo anaamini mwanawe atafanya vizuri kama
ataendelea kujituma mazoezini na kuendeleza kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
“Mimi ndie baba mzazi na meneja wa
Mwinyi, najua msimu huu kuna changamoto kubwa kwa mwanangu lakini naamini
ataendelea kucheza kikosi cha kwanza Yanga, muhimu kuzidi kujituma mazoezini na
pia aendeleze nidhamu, mpira ni mchezo wa hadharani, najua changamoto nyingi na
wala asishuhulikie sana taarifa za kwenye mitandao ya kijamii, namtakia kila la
kheiri washinde Jumatano dhidi ya Simba”. Alisema Mzee Haji.
Jana Jumapili Yanga walikamilisha
michezo yao ya kirafiki huko Kisiwani Pemba baada ya kuifunga Jamhuri bao 1-0
huku Mwinyi Haji akingara sana katika mchezo huo baada ya kufunga bao dakika ya
5 na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kabisa.
Comments
Post a Comment