JUUKO MURSHID KUTUA ZENJ KUUNGANA NA WENZAKE KAMBI YA SIMBA, NYONI NAE KUTINGA ZENJ KESHO AKITOKEA BURUNDI MSIBANI

Mlinzi wa kati wa Simba Mganda Juuko Murshid wakati wowote kuanzia leo anatarajiwa kujiunga na wenzake kambini Visiwani Zanziabar kwaajili ya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga utakaupigwa Agost 23, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam.

Akizungumza na Mtandao huu Mratibu wa Simba Abbas Suleiman amesema Juuko yupo Dar es salam akitokea Afrika ya Kusini na leo Jumanne muda wowote ataungana na wenzake kambi hapa Zanzibar.

“Juuko yupo Dar es salam na muda wowote kuanzia Jumanne ataungana na wenzake hapa Zanzibar”.

Wakati huo huo mlinzi mpya wa Simba Erasto Edward Nyoni nae akitarajiwa kuungana na wenzake kuanzia kesho Jumatano ambapo anatokea Burundi msibani.


“Nyoni ataungana na wenzake kesho Jumatano mana alikuwepo Burundi kwenye msiba wa bamkwe wake na leo Jumanne atafika Dar es salam kisha kuja huku Zenj, alikwenda msibani baada ya kufiwa na bamkwe wake hivyo sisi tulimpa nafasi hiyo na karibu ataungana na wenzake”. Alisema Abbas.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS