KAPINGA ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA MAJESHI, AZIDI KUWAPA HAMASA YA KUTWAA UBINGWA
Wanamichezo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wametakiwa
kuzidisha nidhamu, upendo, umoja na mshikamano katika kuhakikisha wanapata
mafanikio katika Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati ya
mwaka huu ambayo yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia Agost 26, 2017.
Wito huo umetolewa na mkuu wa operesheni, mafunzo na michezo ndani ya jeshi la
wananchi wa Tanzania Brigidia Jeneral Alfred Kapinga alipotembelea kambi ya
timu hiyo ambayo ipo Migombani Jeshini Mjini Unguja.
Alisema nidhamu na upendo ndio silaha kubwa ya mafanikio,
hivyo anaamini wakiendelea kutunza watafanikiwa kubeba ubingwa katika
mashindano hayo.
“Mulichaguliwa wengi sana lakini mumechujwa na sasa mumebakia
nyinyi, naamini nidhamu, upendo,
umoja na mshikamano ndio silaha kubwa ya mafanikio yenu, endelezeni naamini
mutabeba ubingwa mimi sina wasi wasi na nyinyi”. Alisema Kapinga.
Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati
mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia Agost 26 ambapo timu za Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa Miguu, mpira wa
Kikapu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete na Riadha.
Comments
Post a Comment