TAIFA YA JANGOMBE YAIPIGA NEGRO KWENYE MCHEZO WA KUTEST MITAMBO

Timu ya Taifa ya Jangombe (Wakombozi wa Ngambo) wamefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Negro FC katika tamasha la Negro day mchezo uliopigwa jana usiku katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Taifa yamefungwa na Said Kipara pamoja na Abdallah Mudhihir “Mido”.

Aidha katika mchezo huo timu zote zilipata fursa ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ambapo Taifa watashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar wakati Negro watacheza ligi daraja la pili taifa.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS