YANGA SC YAFIKA UNGUJA LEO USIKU KUCHEZA NA MLANDEGE, KESHO ASUBUHI PEMBA KWAJILI YA MPAMBANO WAO DHIDI YA SIMBA

MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga wamewasili kisiwani Unguja leo saa 5 za asubuhi wakitokea Jijini Dar es salam ambapo leo saa 2:00 za usiku watacheza mchezo wa kirafiki na Mlandege SC mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Amaan.

Yanga wamefikia katika Hoteli ya Lail-Noor ambayo ipo Maisara Mjini Unguja.

Kesho asubuhi Yanga wataondoka kisiwani Unguja na kwenda Kisiwani Pemba kuweka kambi kujiandaa na pambano na mtani wake, Simba katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa Agost 23, 2017 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam.
 
Kushoto ni Haji Mwinyi Ngwali "Bagawai" kati ni Abubakar Khatib Haji "Kisandu" na kulia ni Abdallah Haji Shaibu "Ninja"

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS