AJIBU AANZA MAKALI YAKE ZENJ, AFANYA VITU SI MCHEZO YEYE NA KAMUSOKO

Kikosi cha Yanga kilichoanza mchezo wa jana
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Ajib jana ameonesha kiwango cha hali ya juu kabisa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege uliopigwa saa 2 za usiku katika uwanja wa Amaan ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mbali ya kuonesha uhodari wake wa kuuchezea mpira Ajibu pia alifungua akaunti yake ya mabao baada ya kufunga bao lake la kwanza dakika ya 50 katika historia ya klabu yake hiyo mpya tangu ajiunge nayo akitokea Simba.

Bao hilo la Ajib ni msaada mkubwa wa Kiungo wa wakimataifa wa Zimbabwe Thabani Kamusoko ambae alipiga shuti kali na Ajib akamalizia.

Bao jengine la Yanga lilifungwa na Emanuel Martin dakika ya 73 ambapo ni bao lake la pili katika msimu huu kuanza kufuatia kushinda bao la ushindi Yanga walipoifunga Singida United 3-2.


Kikosi cha Yanga kimeondoka  kisiwani Unguja asubuhi ya leo Jumatatu kwa Ndege na kwenda Kisiwani Pemba kuweka kambi kujiandaa na pambano na mtani wake, Simba katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa Agost 23, 2017 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salam.
Kikosi cha Mlandege kilichoanza mchezo wa jana

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS