KESHO NI ZAMU YA SIMBA NA MLANDEGE
Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya
kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, kesho Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za
usiku katika uwanja wa Amaan.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani
hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa
kirafiki kufuatia kucheza michezo minne.
Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini
kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1
na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa
siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam na mwisho kuwafunga Mtibwa
Sugar 1-0.
Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita ya Agost 13
walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan ambapo kesho watakipiga
tena na Simba.
Comments
Post a Comment