SIMBA NA MLANDEGE HAPATOSHI LEO USIKU

Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, leo Alhamis watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne.

Simba walicheza mechi mbili walipokwenda Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate, kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salam na mwisho kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0.

Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita ya Agost 13 walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan ambapo leo watakipiga tena na Simba.



Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS