HILIKA AIBUKA MFUNGAJI BORA LIGI YA ZANZIBAR
Mshambuliaji wa Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika ameibuka kuwa
mfungaji bora wa ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2016/2017 baada ya kufunga
jumla ya mabao 14 katika hatua ya 8 bora.
Hilika alianza dalili za kuwania ufungaji bora baada ya
kushinda yeye pia kwenye ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo alishinda
jumla ya mabao 19 katika kanda hiyo, hivyo ukipiga hesabu 19 na 14 utapata 33
ambayo ndio idadi ya mabao aliyofunga msimu huu wote tangu ligi ilipoanza kanda
mpaka kufikia hatua ya 8 bora.
Nafasi pili imekamatwa na Mwalim Mohd wa Jamhuri aliyefunga
mabao 10 katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora.
Mtandao huu umepiga stori na mshambuliaji huyo na kutaka
kujua amejisikiaje kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo ambapo
amefurahishwa mno na kusema kuwa ni lengo lake kuwa mfungaji bora na katimiza.
“Nimefurahi sana kwani niliweka lengo hilo lakini nawashukuru
viongozi wangu wote pamoja na wachezaji wangu kwani bila ya ushirikiano wao
siwezi kufanikiwa kwa chochote”. Alisema Hilika.
Mpaka sasa hakuna zawadi yoyote iliyotangazwa na Chama cha
Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kwa mfungaji bora wala kwa bingwa wa ligi hiyo
atapatiwa zawadi gani huku wadau wengi wakihimizwa kujitokeza kuwapa hamasa
vijana hao ambao wanafanya makubwa na mazuri katika soka la Zanzibar.
Mfungaji bora wa msimu uliopita wa mwaka 2015-2016 ni Hakim Khamis
“Men” alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa ubingwa wa ligi
hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu
wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa msimu huo.
Comments
Post a Comment