MPIRA WA KIKAPU WILAYA YA MJINI WAANDAA MASHINDANO MAKUBWA YALODHAMINIWA NA KAMPUNI KUTOKA MAREKANI
Chama cha Basketball Wilaya ya Mjini (UBA) kinatarajia kuanzisha
mashindano ya Mpira wa Kikapu kwa Wanaume yananayotarajia kuanza rasmi Septemba
9, 2017 katika viwanja vya Gymkhana Mjini Unguja na katika ufunguzi huo siku
hiyo kutapigwa mchezo kati ya timu ya POLISI dhidi ya MBUYUNI.
Katibu wa Basketball wilaya ya mjini Saidi Ali Mansabu
amesema mashindano hayo wamepata wadhamini kutoka kiwanda cha kutengeneza Jezi
cha UTA ambacho kipo Marekani.
“Mashindano yetu tunatarajia kuanza Septemba 9, 2017 ambapo
tumepata wadhamini kampuni moja ya kutengeneza Jezi inaitwa UTA ipo Marekani,
wametudhamini Jezi na mahitaji mengine katika Mashindano haya, nawaomba wadau
wajitokeze kwa wingi kwasababu haya ni mashindano makubwa sana kwa vile
wadhamini ni wenye mpira huu”. Alisema Mansabu.
Jumla ya timu 14 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo
ambayo yataanzia kwa hatua ya makundi kwa kupangwa makundi mawili, kundi A na
kundi B ambapo timu nne za juu kwa kila kundi zitatinga hatua ya robo fainali
kisha moja kwa moja kupatikana timu nne za nusu fainali kisha kucheza timu
mbili kucheza fainali.
Miongoni mwa timu zilizothibitisha kushiriki ni Polisi,
Mbuyuni, Stone Town, Africa Magic, Betras, Zan Kwerekwe, Ranger, New West na
Nyuki.
Comments
Post a Comment