DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA KESHO ALHAMIS, HAKUNA KUONGEZA SIKU-KATIBU ZFA

Dirisha la uhamisho na usajili rasmi linafungwa kesho Alhamis Agost 17 majira ya saa 6:00 za usiku ambapo Makocha na Viongozi wengine wa Vilabu wamezidi kuwa bize kutafuta wachezaji wanaowahitaji ili kuziboresha timu zao katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018.

Akizungumza na Mtandao huu katibu mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema usajili unafungwa kesho Agost 17 na wao ZFA hawatoongeza siku wala muda ukifika wakati uliopangwa zoezi hilo litapigwa kufuli.

“Ni kweli zoezi la uhamisho na usajili linafungwa kesho Alhamis saa 6:00 za usiku na wala hatutarajii kuongeza siku wala saa, muda ukifika zoezi hilo litafungiwa”. Alisema Tedy.

Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kilitangaza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 kufunguliwa July 17, 2017 na kumaliza kesho Agost 17, 2017.

Zoezi hilo ni kwaajili ya Maraja yote kuanzia ligi kuu soka ya Zanzibar, ligi daraja la kwanza Taifa, la Pili Taifa hadi ligi za Madara ya Wilaya.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS