MZEE MARUNGU AFARIKI DUNIA, NI PIGO JENGINE KWA ZFA NA WAPENZI WA SOKA
Muamuzi mstaafu wa Kimataifa Ahmed Mohd Awadh (Mzee Marungu)
amefariki dunia leo Jumanne Agost 22, 2017 ambapo Maziko yatafanyika nyumbani
kwake Shangani na kuzikwa leo saa 10 jioni Mwanakwerekwe.
Mbali ya kuwahi kuwa muamuzi wa kimataifa pia marehemu
alikuwa Kamisaa wa ligi za Zanzibar.
Juzi wapenzi
wa soka Visiwani Zanzibar walipata pigo jengine kufutia kuondokewa na Dokta wa
zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes” Dokta Abdallah Said
Mohammed “ Dokta Kuku” aliyefariki dunia Agosti 20, 2017 nyumbani kwake
Muembetanga mjini Zanzibar na kuzikwa jana Agost 21, 2017 kijijini kwao Fujoni Wilaya
ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema Peponi
Amiin.
Kwa taarifa Zaidi endelea kusoma Blog hii.
Comments
Post a Comment